lonyorengai
Member
- May 12, 2008
- 71
- 35
Wadau naomba tujadili hili kwa mapana zaidi. Barabara zinazojengwa na manispaa zetu kwa sasa zina kiwango duni kwa mfano katika manispaa ya Kinondoni, Kijitonyama barabara ya Akachube, Kipande cha Sinza Uzuri, na nyinginezo nyingi ambazo hata mwaka hazijamaliza lakini tayari zimeumuka na mahandaki pia yamejitokeza. Kimsingi huu ni ufujaji wa fedha za walipa kodi na pia kuna kila dalili za teni pasenti kwa kuwa siamini kwamba madiwani na mameya hawaoni ubovu huu wa barabara kiasi cha kuzikubali.
Hii inatokea katika maeneo mengi ya nchi yetu kama Arusha, Dodoma n.k.
Siasa katika miradi kama hii itatupeleka shimoni. Mheshimiwa Jerry Slaa, naomba majibu yako!
Hii inatokea katika maeneo mengi ya nchi yetu kama Arusha, Dodoma n.k.
Siasa katika miradi kama hii itatupeleka shimoni. Mheshimiwa Jerry Slaa, naomba majibu yako!