Dance 100 zawadi ndogo sana

Dance 100 zawadi ndogo sana

MamaBeata

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2013
Posts
325
Reaction score
112
Wadau samahani kama nitamkwaza mtu lakini binafsi sijapendezwa na zawadi zinazotolewa na shindano la dance 100 linaloendeshwa na channel 5 east Africa television.
Hebu fikiria washiriki wanatakiwa kuwa kundi la watu kuanzia 5-8. Mshindi anapata zawadi ya sh za kitanzania milioni tano. Wakigawana kila mmoja kwa kundi la watu watano kila mtu atachukua milioni moja. Na kama wako wengi zaidi kiasi kitapungua zaidi.
Nafikiri hii zawadi haiendani na effort iliotumika kwa washiriki. Kuna mazoezi yanayotakiwa kufanyika na pia gharama za sare nakadhalika. Yote hii uishie kupata milioni tano? Tena sio ya peke yako?
Najua watu wengine watasema kuwa group pia linapata faida nyingine ikiwemo promo ya kuwafanya wajulikane na wadau. Lakini bado washiriki hawatendewi haki. Mbona mashindano kama Bongo star search inatoa zawadi zinazoweza kubadilisha maisha ya Mshindi? Kwanini dance 100 watoe zawadi kiduchu wakati juhudi kubwa inahitahitajika ili ushinde?
 
Waandaaji watafute zaidi wafadhili ili pamoja na kuongeza zawadi kwa washindi isaidie vikundi vinavyoshiriki kwani hutumia muda wo na gharama kubwa. Mashindano haya yasaidie kuinua maisha ya vijana kwa kutumia vipaji vyao.
 
True, mimi nikifiria wale vijana wanavyojituma kugombea zawadi ambayo hata haina maslahi nawahurumia. Nalihurumia jasho lao.
 
Zawadi inatokana na mdhamini na attention ya shindano

mamaBeata una mwanao nini humo anashindana?
 
Zawadi inatokana na mdhamini na attention ya shindano

mamaBeata una mwanao nini humo anashindana?

Hapana ila huwa nafatilia kipindi naona kama zawadi ndogo ukiangalia maisha ya sasa hivi yalivyo juu
 
Hapana ila huwa nafatilia kipindi naona kama zawadi ndogo ukiangalia maisha ya sasa hivi yalivyo juu

Labda shindano halijawashika watu
hivyo wadhamini hawatoi pesa ya kutosha
 
Wadhamini sio wengi na pia haijapata umaarufu sana, ipo siku dau litapanda
 
Back
Top Bottom