mwacheni77
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 763
- 209
Katika mechi ya Villarreal na Barca,mashabik wa Villarreal walionesha kitendo cha kibaguzi kwa kumtupia ndizi beki wa Barca, Dan Alves.
Ujasiri alioufanya alichukua ile ndizi akaimenya na kuila akapiga kona bahati nzuri ikamgusa beki wa Villarreal na kuwa goli.
Nimefurah maana kitendo hicho hakijamtoa mood ya mchezo.
==========
Ujasiri alioufanya alichukua ile ndizi akaimenya na kuila akapiga kona bahati nzuri ikamgusa beki wa Villarreal na kuwa goli.
Nimefurah maana kitendo hicho hakijamtoa mood ya mchezo.
==========
Beki wa pembeni kutoka nchini Brazil na klabu ya Barcelona, Dani Alves ameushangaza ulimwengu wa soka, kufuatia shukrani alizozitoa dhidi ya mashabiki wa klabu ya Villareal waliomtupia ndizi akiwa uwanjani usiku wa kumkia hii leo huko El Madriga.
Katika hali isiyotarajiwa Daniel Alvesa alifanya hivyo mara baada ya mchezo kati ya Barcelona na Villareal kumalizika huku Barca wakipata ushindi wa mabao matatu kwa mawili.
Alves, amesema kurushiwa ndizi akiwa uwanjani kwake anakichukulia kitendo hicho ni cha kawaida na anaamini wanaofanya hivyo ni mashabiki wenye upeo mdogo wa kufikiria ambao bado wanahitaji usaidizi wa kubadilishwa kimawazo.
Amesema ameishi nchini Hispania kwa miaka 11 na mara kadhaa wachezaji wenye asili ya bara la Afrika wamekua wakikutana na vitimbi kama hivyo, ambavyo vinaashiria ubaguzi wa rangi hali ambayo amesisitiza ameshaizoea.
Hata hivyo beki huyo mwenye umri wa miaka 30, kwa kuonyesha hajali masuala ya ubaguzi wa rangi, alidiriki kukata kipande cha ndizi aliyorushiwa uwanjani na kukila huku sehemu iliyo baki akiitupa pembezoni mwa uwanja wakati akijitayarisha kupiga mpira wa kona.
video hii hapa chini.
<strong>
Last edited by a moderator: