#COVID19 Dalili zingine za Omicron

Labda hapo pa kutapika na kuharisha.
Nimekulia Nyanda za Juu Kusini. Mafua ya aina hiyo nimeumwa sana enzi hizo nikiwa Rungwe Secondary!
Ilikuwa inanichukua karibu wiki nzima kupona. Mdomo unakuwa mchunguu!! , kichwa kuuma, mwili, Koo kuwasha ndivyo usisema likiendana na kupigwa chafya mfulizo!(1980-1983)
Si kila mwenye dalili hizi ni mgonjwa wa omicron, bali dalili za omicron ni hizo.
 
Hizo dalili zote ni for sure..na ukitaka uone Omicron noma uwe na vijiMalaria,Uti or Typhoid yaan kigonjwa kingine cha ziada tofauti na yenyewe utakubali mziki wake mbona.

Mm Jana na Leo ndio nimepata nafuu wiki mbili karibu zote hizi nilikuwa hoi,nikasema sasa 2022 itanikuta juu mbinguni kwa Mungu.

Ushauri ukijiskia homa,mafua kikohozi,mwili kulegea na kuchoka pamoja na kutumia tangawizi limao na vitunguu Swaum ila nenda kwanza kapime magonjwa mengine ya kawaida.

Unaweza kupambana na Omicron pekee Malaria ikapita na ww sababu akili yako yote utaielekeza kwenye gonjwa moja kumbe una shida nyingine pia.
Pole sana mkuu kama ulijaribu kupatwa na omicron.
 
Watanzania wishalipita huko kwenye Omiricon kwa sasa tunasibiri kirusi kipya
Ni kweli kabisa kipinda cha Disemba Miji mingi upepo huo wa homa za ajabu na mafua zilitupata Mungu amejalia
Watanzania tujipe moyo, hili gonjwa km lilishatupitia hebu tuangalie January, February na March huenda tukavuka
 
Back
Top Bottom