Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume

Inawezekana sana kwa mwanaume kupata UTI:-
•kujamiina na mwanamke mwenye UTI bila kinga.
•Vyoo vichafu hasa vya umma
•Kuvaa chupi chafu kwa muda mrefu
au ku-share hizi underpants na aliepata hai bacteri.

ni shidaaah
 
U.T.I ni urinary Track Infection

so urethral sijui ndo iko infected au epididymis sikumbuki vizuri biology yenyewe ya division 5

it is either through sharing toilet , choo hakisafishwi vizuri ( dettol na harpic is effective)

Redioni na kwenye magazeti kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu huu ugonjwa. Kirefu sahihi cha UTI ni URINARY TRACT INFECTION. Siyo TRACK. Wapotoshaji wakubwa ni hawa wanaojiita madaktari wa matibabu mbadala, matapeli wakubwa sana. Wengine wanaenda mbali na kusema ati UTI inaweza kutibiwa kwa kupata dawa mara moja tu. UTI ni ugonjwa wa wote, wanaume na wanawake. Ila wanawake wanaugua mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

Ukweli ni kwamba hakuna daktari wa matibabu mbadala anayeweza kutibu UTI.

Tatizo lipo kwa serkali kupitia kwa wizara ya afya kuwaruhusu hawa wapotoshaji/matapeli kujitangaza. Radio wanazozitumia zinajali pesa tu.

UTI isipotibiwa haraka ina madhara makubwa sana, hasa kwa wanawake.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa matapeli wa matibabu hivi karibuni, sasa hivi UTI umekuwa ugonjwa common sana kuliko uhalisia.

Kama uko Dar na unahisi una UTI, nenda MUHAS kaonane na Dr wa idara ya Microbiology, au nenda idara ya Internal Medicine. Tatizo ukiwa mikoani.

Hawa matapeli wanatumia vibaya uelewa mdogo (ignorance) ya wa TZ walio wengi.
 
Redioni na kwenye magazeti kuna upotoshaji mkubwa sana kuhusu huu ugonjwa. Kirefu sahihi cha UTI ni URINARY TRACT INFECTION. Siyo TRACK. Wapotoshaji wakubwa ni hawa wanaojiita madaktari wa matibabu mbadala, matapeli wakubwa sana. Wengine wanaenda mbali na kusema ati UTI inaweza kutibiwa kwa kupata dawa mara moja tu. UTI ni ugonjwa wa wote, wanaume na wanawake. Ila wanawake wanaugua mara nyingi zaidi kuliko wanaume.

Ukweli ni kwamba hakuna daktari wa matibabu mbadala anayeweza kutibu UTI.

Tatizo lipo kwa serkali kupitia kwa wizara ya afya kuwaruhusu hawa wapotoshaji/matapeli kujitangaza. Radio wanazozitumia zinajali pesa tu.

UTI isipotibiwa haraka ina madhara makubwa sana, hasa kwa wanawake.

Kwa sababu ya kuongezeka kwa matapeli wa matibabu hivi karibuni, sasa hivi UTI umekuwa ugonjwa common sana kuliko uhalisia.

Kama uko Dar na unahisi una UTI, nenda MUHAS kaonane na Dr wa idara ya Microbiology, au nenda idara ya Internal Medicine. Tatizo ukiwa mikoani.

Hawa matapeli wanatumia vibaya uelewa mdogo (ignorance) ya wa TZ walio wengi.

spelling mistake nayo ni upotoshaji hee makubwa ,

anyway ciproprakcin nadhani na maji mengi yanasaidia kusafisha kibofu cha mkojo
 
Naskia hata walaji Wa tigo na wanaambukizwa sana uti!!sasa kama dogo nae ni team tigo aka jicho muadharishe sana pekupeku kwenye lile shimo ni hatari kwa afya yake
 
ndugu wa humu naombeni msaada njia zinazopelekea mwanaume kupata huu ugonjwa wa U.T.I maana kuna mdogo wangu amepima leo urine kaambiwa ana huoo ugonjwa. Je mwanaume anawezaje pata U.T.I .? Karibuni nyoteee kwa michango yenu.

MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTI)


Neno U.T.I si geni masikioni mwa wengi, kwani ni wengi leo utawasikia "naumwa U.T.I". Japo si wote hulitumia kisahihi. Wengine wana tatizo ambalo ni tofauti na U.T.I, lakini anaweza akaenda hata duka la dawa na kuomba apatiwe dawa za U.T.I. Leo nimeona tubadilishane elimu juu ya hili tatizo, angalau kila mmoja awe na uelewa U.T.I ni nini hasa, inasababisha na nini, na ni jinsi gani anaweza kujikinga.

U.T.Is, ni kifupisho cha Urinary Tract Infections, ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo. Kama linavyojieleza, kwamba maambukizi ni lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo ndipo tunaita ni U.T.I, na si pengine popote. Una uchafu unatoka ukeni, hiyo ni kitu kingine tofauti nk. Tunapozungumzia njia ya mkojo, ni kutoka eneo la nje hadi kwenye kibofu, na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.
Kama maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo(ikihusisha na figo pia), inaitwa Lower Urinary Tract Infect. Na ikihusisha eneo la juu ya kibofu, inaitwa Upper Urinary Tract Infection.


Tatizo hili huwapata wote, wanaume na wanawake. Lakini huwapata zaidi wanawake kutokana na tofauti za kimaumbile. Hii ni kwa sababu kuu mbili, i)njia ya haja ndogo ya mwanamke iko jirani zaidi na njia ya haja kubwa ambapo vijidudu vingi visababishao U.T.I ndipo vinapoishi, ii) mrija wa mkojo (urethra) wa mwanamke ni mfupi ukilinganisha na wa mwanaume, hivyo kufanya iwe rahisi kwa maambukizi kufika kwenye kibofu kwa mwanamke kuliko kwa mwanaume.
Visababishi


Tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bacteria ambao makazi yao ya kawaida utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa, mfano Escherichia coli na wengineo. Pia, linaweza likasababisha na fungus' na visababishi vingine, japo ni mara chache sana.
Vihatarishi na Njia ya Maambukizi


a)Kwa wanawake
Kujamiiana hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi
Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia
Ujauzito mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi


b)Kwa wanaume
Matatizo ya tezi ya kiume
(prostate) mabapo husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha mkojo vizuri na kuruhusu bacteria kujenga makazi
Kutotahiriwa, ambapo nyama ya mbele inaweza kuhifadhi bacteria wasababishao U.T.I
Kujamiiana kinyume cha maumbile huingiza kirahisi bacteria walio njia ya haja kubwa kwenye njia ya mkojo
Kujamiiana bila kinga na mwanamke ambaye ana maambukizi ukeni
Kuwa na VVU ambapo hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi
c)Kwa wote
Kutokunywa maji na vinyaji kwa wingi kunywa maji mengi husababisha mkojo kuzalishwa kwa wingi, na kukojoa mara kwa mara na hivyo kusafisha njia ya mkojo
Kuwekewa mirija inayosaidia kutoa mkojo nje inaweza pia kukaribisha maambukizi
Matatizo ya figo na mengine kwenye njia ya mkojo yanayoweza kuziba njia ya mkojo
Kisukari ambapo hudhoosha kinga ya mwili na pia kuharibu mfumo wa figo wa uchujaji


Dalili za U.T.I
a) Kwa eneo la chini la njia ya mkojo
i. Hali ya kujisikia kutaka kukojoa muda wote
ii. Maumivu, au hali ya kujisikia kuchoma choma wakati wa kukojoa
iii. Kukojoa mara kwa mara na mara zote mkojo ni mdogo
iv. Mkojo unaweza kuonekana una ukungu, na mara nyingine unatoa harufu kali
v. Maumivu ya nyonga kwa wanawake
vi. Maumivu ya rektamu(rectum) kwa wanaume
vii. Na mara nyingine damu kwenye mkojo
b) Kwa eneo la juu la njia ya mkojo
i. Maumivu ya tumbo(hasa eneo la juu kwa pembeni chini ya mbavu)
ii. Homa kali
iii. Kutetemeka na kujihisi baridi
iv. Kichefuchefu na /au kutapika
Vipimo na matibabu
Mara nyingi kipimo cha mkojo kinaweza kuonyesha tatizo.
Matibabu ni antibiotic baada ya daktari kubaini tatizo
Madhara yatokanayo na U.T.I isipopata tiba sahihi
Inaweza ikasababisha maambukizi makubwa ya figo (pyenephritis) ambayo yanaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa figo na hivyo kutishia maisha
Kwa wajawazito inaweza kuhatarisha maisha ya wote mama, na motto aliye tumboni
Bakteria wanaweza kuingia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhala mengine
Inaweza kusababisha shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo


Tiba mbadala nyumbani kabla ya kumwona daktari
Unaweza kutibu, ama kupunguza tatizo nyumbani kabla ya kumwona daktari pale uonapo dalili ya awali ya U.T.I, ambayo ni maumivu na kuchomachoma wakaji wa kukojoa. Fanya yafuatayo
i. Kunywa maji mengi hasa saa 24 za kwanza baada ya kuona dalili. Hii itasaidia kuzalisha mkojo kwa wingi na kusafisha njia ya mkojo
ii. Kojoa mara kwa mara na hakikisha ni hadi mkojo unaisha ili kibofu kiwe tupu
iii. Kwa maumivu ya mlango wa mkojo, oga na kuosha kwa maji ya moto, kutapunguza maumivu
Njia za Kujikinga na U.T.I


Kunywa maji na vinywaji kwa wingi kila siku. Hii itakusaidia ukojoe mara kwa mara na kutoruhusu bacteria kujenga makazi kwenye njia ya mkojo
Kojoa kila ujisikiapo mkojo na usiubane kwa muda mrefu


Kwa wanawake
Nenda ukakojoe mara tu umalizapo tendo la kujamiiana. Hii itasaidia kutoruhusu bacteria kuingia na kujenga makazi kwenye njia ya mkojo.
Badili pedi mara kwa mara uwapo hedhini
Epuka kujisafisha ukeni na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupilizia marashi ukeni, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu. Hizo huua bacteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bacteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi


Ujisafishapo baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha bacteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauliana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni kuwasaidia kujikinga na maambukizi


Kwa wanaume
Kuhakikisha maeneo ya ncha ya uume ni masafi mara zote, hasa ikiwa hujatahiriwa kuepusha kujihifadhi na kuzaliana kwa vijidudu visababishao maradhi.
Kondom wakati wa kujamiiana nayo ni kinga nzuri
Asanteni kwa kutenga muda wenu kupata elimu hii


Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 

Attachments

  • Male.jpg
    Male.jpg
    7 KB · Views: 2,468
  • UTI.jpg
    UTI.jpg
    13.3 KB · Views: 610
spelling mistake nayo ni upotoshaji hee makubwa ,

anyway ciproprakcin nadhani na maji mengi yanasaidia kusafisha kibofu cha mkojo

Wewe utakuwa mmoja wa matapeli wanaowaibia watu ati ni mabingwa/madaktari wa tiba mbadala. Mnajitangaza mko Buguruni na Kinondoni kwa manyanya. Acheni wizi. Na redio ziache kuwatangaza maana kwa kufanya hivyo zinawasaidia katika utapeli wenu.
 
Kushika/kuegemea ukuta wakati wa kupiga punyeto, anaweza pata vimelea ukutani akavihamishia uumeni.
 

MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO (URINARY TRACT INFECTIONS -UTI)






a)Kwa wanawake

• Kujamiiana –hii huweza kuamisha bacteria walio kwenye uume moja kwa moja, ama watokanao na maambukizi ya ukeni kuingia moja kwa moja njia ya mkojo
• Kuchezea ama kuchezewa na mikono michafu maeneo ya uke kunaweza kusababisha maambukizi
• Njia mbaya ya kujisafisha baada ya haja kubwa au ndogo inaweza kuhamisha bacteria walio ktk njia ya haja kubwa na kuingia njia ya mkojo
• Matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambao huua bacteria wa asili wa eneo la uke na kukaribisha bacteria wanaosababisha maradhi kuzaliana kwa wingi


Vifuatavyo pia vinaweza vikachangia

• Ujauzito –mara nyingi hushusha kinga ya mwili ya mjamzito
• Upungufu wa homon ya ya kike Oestrogen husababisha bacteria wasababishao U.T.I kuzaliana kirahisi




Ukiwa na Tatizo lolote Au swali lolote lile usikose kunitafuta Bonyeza hapa.
Mawasiliano

Mkuu MziziMkavu, je hapo kwenye RED unazungumzia ped aina ya HQ????
 
Last edited by a moderator:
Waganga wa tiba mbadala wamekuwa ni matapeli wakubwa wa kisasa. Wengi kama umegundua wameelemea kwenye magöjwa ya wanawake na magonjwa sugu. Wanajua wakikupiga gharama yeyote utatoa wakati ni matapeli wanaocheza na akili zako tu. Amkeni!
 
Wewe utakuwa mmoja wa matapeli wanaowaibia watu ati ni mabingwa/madaktari wa tiba mbadala. Mnajitangaza mko Buguruni na Kinondoni kwa manyanya. Acheni wizi. Na redio ziache kuwatangaza maana kwa kufanya hivyo zinawasaidia katika utapeli wenu.

ni maneno tu hata kwenye khanga yameandikwa, mdomo mali yako haulipii vocha mfyuuu kantangazeeeeeeeeee
 
Naskia hata walaji Wa tigo na wanaambukizwa sana uti!!sasa kama dogo nae ni team tigo aka jicho muadharishe sana pekupeku kwenye lile shimo ni hatari kwa afya yake

100% true coz hata watoto wachanga wengi wanaopata UTI ni kutokana na bacteria wanaotokea kwenye njia kubwa baada ya kujisaidia na kukaa muda mrefu bila kubadilishwa nepi
 
mkuu upo sawa kwambali ila ukwl wa mambo mwanaume kupata UTI huwa inaletwa na sex. kwa mwanamke inaltwa na kutawaza nakushea vyoo.kama unajhsi una infection pga azthromycene mg 250.
 
Back
Top Bottom