Dalili gani inaonesha kwamba una-force mahusiano?

Hahahaha kuna MTU aliweka thread akaeleza vizuri kabisa last week nadhani, wacha nijaribu kama nitakumbuka bàadhi

Moja, hapigi simu wala text hadi uanze wewe
Pili, ukiona siku ameanza yeye kukutumia SMS na very rare kukupigia simu basi ujue anataka pesa

Tatu, mapenzi yanakua ya moto moto ukiwa na pesa, au akijua una dalili ya kupata pesa, wacha ziishe sasa

NNE, anaweza akakuaga then unnamkuta ONLINE hata SAA nane usiku

Tano, mkitoka mna-spend unnecessarily na hawezi hata kuuliza au at least kuwa na huruma

Sita, anapenda yeye siku zote issues zake tu ndio ziwe attended promptly yaani hana hata staha kuwa na wewe hebu kajifanyie hiki

Saba, hawezi kukutambulisha kwa rafiki zake hata siku moja, au akifanya hivyo anafanya kwa masiala sana

Nane, hawezi kukununulia hata handkerchief ya buku, yaani ile ya kuzugia tu kuwa na wewe umepokea kitu kutoka kwa mpenzi wako.

Tisa, siku zote yeye ni MTU wa kulalamika tu, jambo dogo tu atalikuza na kukimbiliaa kusema kuwa MUACHANE! yaani mkitofautiana kidogo tu anakimbilia kukwambia muachane

Kumi, siku zote wewe ndio unayeomba msamaha hata kama kosa ni lake, yaani hawezi kukubali kosa kamwe.

Kumi na moja, yuko busy na simu hata mkiwa pamoja au anazima simu mkiwa wote na endapo atapokea anajibu kwa kifupi au anajibu kwa Ku"fake" sana yaani unajua tu hii simu hii.....

Kumi na mbili, haruhusu uende kwake bila appointment, yaani hataki surprise na ukifika hataki ukae sana.

Ushauri, Acheni Umalaya tafuta Mchumba umuoe au akuoe hutapata hizi mambo
 
Licha ya kutuma tuma texts zisizojibiwa kila wakati, dalili gani nyingine inaonesha kwamba una force Mahusiano?
Kupiga simu nyingi 😂!

Kanuni ya 6 ibara ya 2 ya katiba ya mabaharia inasema Missed calls mwisho ziwe mbili zenye tofauti ya dakika 10 au zaidi! Sio unampigia mtu simu 12 kwa mpigo tulia acha usumbufu!
 
Ukiomba mzigo ghafla ana bridi
Unamtumia kifurushi cha sms af mnachat sms 10 tu kesho tena unaambiwa sms zimeisha.
Unaambiwa usiku mwema saa 2 af ukipiga saa 4 simu inatumika hizo ndy sababu zilizofanya niwe single.
😅 Hii ni Module ambayo kila baharia lazma aipitie kabla ya ku graduate Masters ya Ubaharia! Ni topiki ngumu kama hesabu za Log ama Calculus!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom