Dali Mpofu: Kijana aliyevunja ndoa ya Nelson Mandela

Dali Mpofu: Kijana aliyevunja ndoa ya Nelson Mandela

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,634
Reaction score
112,473
Nelson Mandela baada ya kutoka gerezani, kila mtu alipenda aone shujaa huyo pamoja na familia yake, akiwemo mkewe kipenzi Bibi Winnie Madikizela Mandela aliyetaabika kwa muda wote wa miaka 27 akipambana na makaburu wakati mumewe akiwa kifungoni -wakiishi maisha ya furaha, amani na upendo.

Lakini ni bahati mbaya sana na jambo la kusikitisha kuja kuona miaka miwili tu baada ya kuachiwa kwa Mandela ndoa yao inavunjika, Baada ya kuoana waliishi miaka miwili na pia baada ya kuachiwa kutoka kifungoni waliishi tena miaka miwili tu.

Mandela na Winnie walioana hapo June 14, 1958, lakini walikaa pamoja kwa muda usiozidi miaka miwili Mandela ndipo akafungwa kifungo cha Maisha jela. Kwa kipindi chote hicho cha miaka 27, Bibi Winnie Mandela aliishi maisha ya misukosuko akipigana na utawala wa Makaburu hali iliyomfanya kuwa ?Sugu na mwishowe akatumbukia katika wimbi la ulevi, kukata tama pamoja na uhalifu wa kuteka nyara hali iliyomtumbukiza katika kesi mbaya ya mauaji. Alibadilika kabisa kutoka kuwa msichana mpole wa kijijini, aliyekuwa mwenye haya, mpaka kuwa? Mwanasiasa moto wa kuotea mbali na mwenye jina kubwa.

Skendo iliyokuja kutibua ndoa yao ni tuhuma za uhusiano haramu, baina ya Bi Winnie Mandela na kijana wakili, mfanyakazi katika kitengo cha mahusiano ya jamii cha chama cha ANC aliyejulikana kama Dali Mpofu miaka 30 wakati huo huku Winnie akiwa na miaka mara 2 yake, kitengo ambacho pia ndicho Winnie alikuwa akifanya kazi.

Dali Mpofu- pamoja na Julius Malema walikuwa mmoja kati ya mawakili waliokuwa wakimtetea Bibi Winnie Mandela katika kesi yake iliyokuwa ikimkabili, na uhusiano huo inadaiwa ulianza kipindi hata kabla Mzee Madiba hajatolewa gerezani.

Lakini katika kujitetea upande wa Winnie ulidai kuwa tuhuma hizo zilikuwa ni njama za Makaburu kutaka kumdidimiza Winnie, kwani hata ndiyo maana walimwachia Mandela huru baada ya kumnunua afanye yale waliyoyataka wao. Julius Malema mwenyewe akimtetea swahiba yake Dali alitamka-Daudi mpofu asingeweza kulala na maa yake.

Lakini pia Mzee Mandela mwenyewe alikuwa na ushahidi mzito wa barua iliyonaswa ikitoka kwa Bi Winnie kwenda kwa huyo mpenzi wake Dali Mpofu, barua ambayo ndani yake Bibi Winnie Madikizela Mandela alikuwa akilia wivu kwa Mpofu kulitelekeza penzi lake kwake ambalo lilikuwa limemnogea kiasi cha kukaa zaidi ya miezi 6 ndani ya nyumba pasipokusemezana na mumewe Mzee Madiba. Ilikuwa aibu kubwa.!

Ikabidi ndoa ivunjike, kila mtu akaishi kivyake na hapo ndipo Mzee Madiba alipoamua kuvuta kifaa kingine, Graca aliyekuwa mjane wa rais Rrais wa Msumbiji Samora Machel.
 

Attachments

  • 1447182317974.jpg
    1447182317974.jpg
    7.9 KB · Views: 1,453
Kumiss hiyo kitu kwa miaka kadhaa ni janga. Sio rahisi kuwa mbali na mwandani wako kwa muda mrefu halafu ukute jamaa hawagegedi, labda pawe na walakini.
 
Kumiss hiyo kitu kwa miaka kadhaa ni janga. Sio rahisi kuwa mbali na mwandani wako kwa muda mrefu halafu ukute jamaa hawagegedi, labda pawe na walakini.

Teh...tehh....😀
 
MI naomba kueleweshwa, Ina maana mzee Madiba hakua anaruhusiwa kumg g da Winnie akimtembelea kule gerezani kwa sababu sheria za wenzetu nasikia ukiwa na pesa, famous unawezafanya hayo gerezani
 
Mandela ameachiwa huru 1990, hii ina maana kuwa miaka miwili baadaye ni 1992.

''Dali Mpofu- pamoja na Julius Malema walikuwa mmoja kati ya mawakili waliokuwa wakimtetea Bibi Winnie Mandela katika kesi yake iliyokuwa ikimkabili, na uhusiano huo inadaiwa ulianza kipindi hata kabla Mzee Madiba hajatolewa gerezani.''

Malema amezaliwa 1981 hii ina maana kuwa mwaka 1992 alikuwa na miaka 11 tu.

Julius Sello Malema born 3 March 1981 age 34 ;Dali Mpofu Born: September 26, 1962 (age 53)
 
Back
Top Bottom