Dalaldala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dalaldala

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ameir, Feb 9, 2012.

 1. A

  Ameir JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 248
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mambo zenu wana Jf.. Nimeagiza Coster ili nianzishe bishara ya daladala, lakini kuna rafiki yangu mmoja kaikandia sana hiyo biashara na ananiambia haina faida kama watu wanavyofikiria.. Baadhi ya watu nilioongea nao wanasema hukosi laki moja kwa siku!! Ushauri kwa aliekua ana experience na hii biahsara..
   
 2. t

  tajirisana Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  biashara yeyote inatakiwa uplan kwanza kabla haujaanza vinginevyo utayumbishwa na maneno ya watu wa mjini wengine wanaweza kuwa wanakushauri vizuri ila wengine wivu kwa kununua gani. ukiyavulia maji nguo inabidi uoge tu
  kaa chini weka plan ya biashara yako ukizingatia unaangalia eneo lenye soko la abiria na gharama ni ndogo usisahau kuangalia kipengele cha kupigwa bao na wale wenye white white kwani maeneo mengine mpango huo sii kwa saana
  hapo unaweza kadiria faida au hasara
  ila mara nyingi sio biashara zote zinaanza na faida , nyingi hasara baada ya mda mfupi faida kubwa
  DONT GIVEUP
   
 3. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,716
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  mkuu huyo jamaa yako anakupenda ndiyo sababu kakupa ushauri huo.

  ushauri wangu kwako ni huu...take your time, ongea vizuri na huyo jamaa yako ili akupe maelezo ya kina, hapa JF hapatakutosheleza kwa maelezo.

  lakini kwa ufupi niseme yafuatayo:
  kaa chini wewe mwenyewe na computer yako ukifungua excel na kisha jaribu kutengeneza jedwali lenye kuonyesha cash flow(inflow ikiwa ni hiyo 150k yako kwa siku na outflow ikiwa ni potential expenses kama service, tyre changes, wearing out pasi na kusahau kuwaa hiyo 150k ni max, always utaletewa pungufu na sababu hazitoisha), pia angalia Pay Back period(yaani ni muda gani utatumia kurudisha pesa utakayowekeza huko)...kisha angalia faida itakayobaki na namna utaweza kujua kama itakulipa au laa.

  mkuu uzoefu unaonyesha kuwa si wengi wanojiingiza katika biashara hii hasa kwa sisi wa maofisini ambao hufanikiwa, usiwaige wapemba na waarabu, wao hawaajiriwi kama mimi na wewe, akiwa na basi moja basi ataendesha mwenyewe au kama ni zaidi basi mojawapo ataendesha mwenyewe, kwa staili hiyo ni rahisi kudhibiti ulaghai na utapeli wa madereva kwa matajiri wao.
   
 4. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni Kweli 55 sio biashara mkuu. But there is an opportunity ya kuitumia hiyo Double Coaster. Weka Kimara Town 1000= full AC na kwa time. Let us say inaondoka 12 asubuhi kuelekea town, saa 2 , saa 4 saa 6 na jioni saa 10 jioni inarejea na gari inakuwa na watoa huduma nadhifu, wasio na lugha za kejeri. Pia waweza kuwa na permanent customer ambao utawachukua kila siku na kuwa rtejesha. J1 Nusu siku na j2 unapumzika. Dereva ajiri na konda wake wasiwe day worker. Naamini italipa
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,296
  Trophy Points: 280
  Mi ninayo Nissan kubwa 1 na Nissan vipanya vitatu.
  Biashara ni nzuri Kama ukipata msimamizi!!!!
  Yaani unaweza ukaona ubahili kutoa hata laki 2 kumlipa msimamizi halafu ikawa inaku-cost zaidi ya laki 5 kwa mwezi.
  Maana madereva ni wajanja sana kwa kusingizia matengenezo mbalimbali ambayo mengine sio ya kweli.
  Mwanzo nilidhani ningeweza pia kama Wewe but baada ya muda nlikuja kukiona cha moto!!
   
Loading...