... daktari aliyejulikana kwa jina moja tu la Rehema, mwajiriwa wa hosipitali ya Bugando aliyekuwa pia akifanya kazi hospitali ya Sekouture na ni shangazi wa mtuhumiwa, alipoteza ushahidi wa mtuhumiwa ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya Fidelis Lyimo.
Taarifa zaidi zinasema ilipofika asubuhi, kaka wa mtuhumiwa alifika hospitali (Bugando) asubuhi na mapema kudai apewe gharama za matibabu ili amtoe mgonjwa, wakati manesi wanajiandaa kumpatia ndipo akatokea dada wa mgonjwa na hali ikabadilika, yule mkaka alipoulizwa akadai hamjui Fidelis.