Daktari na Mbunge ni yupi mwenye umuhimu sana katika jamii?

Bora Mwl anayemuelimisha mwangu mpaka anamfundisha kufikia Tabibu (Dr)
Hivi MaDr mbona kuwaona tu tunawalipa na rushwa juu hilo Daftari ni 1,000/ hizo bilioni 20 za mwaka mmoja tu wa nyongeza tuitoe wapi tukate hela ya JWTZ ? Au Mtanzania alipe 100,000/ kununua daftari?
Jamani MaDr hela HAKUNA kwa nini msi-sign off tubaki na manesi na maMedical Assist MUNGU atatulinda na Mgomo huu wa kisiasa usio na chembe ya ubinadamu
Dr Uli ugua pole
 
lkn tukubaliane kwamba mwanasiasa anapewa ana nafasi yake katika jamii na dokta naye ana yake.bila siasa hakuna demokrasia,bila siasa kuna vita,kama somalia na bila utulivu nchi haiwezi endelea na bila dokta afya haipatikani.ila nikasumba kuwa kwavile wabunge sheria wanazitunga wenyewe basi wamekuwa wakijipendelea wao kwanza alafu wengine baade,kwahiyo haki haitendeki,ila wakumbuke haki ya mtu haidhulumiki
 
WanaJF. Nashindwa kuelewa kwa nini dunia haiko fair kiasi hiki, inakuaje majitu failures (Div IV na O) yawe ndiyo yenye maamuzi makubwa kuliko learned people?
Hakuna mwanasiasa hata mmoja kwenye sayari hii mwenye record ya kuwa mwenye akili bora kati ya wahitimu wote unaowafahamu, isipokuwa kubebwa na kupelekwa.
Walichonacho ma Dr. Kipo kichwani mwao siyo funguo kwamba watanyang'anywa na kupewa mtu mwingine, ni uwezo wao ambao upo ndani yao.
Mgogoro wa maDr. Na serikali unanikumbusha jinsi ambavyo juha anavyojaribu kumpa vitisho mwerevu. Kama zile khadithi za zamani za Abunuwasi.
Tafiti sahihi zimeonyeshwa kwamba, Wakati tukiwa shule tunasoma wanafunzi :

  1. wale wanoongoza darasani ama wenye uwezo mkubwa wa akili darasani huwa wanaelekezwa kusomea Udakatari na uinjinia,
  2. wale wa waoshika nafasi za katikati huwa wanaelekezwa kuwa wahasibu, watawala, na masoko,
  3. wale wanaofeli akina Div. IV and kushuka chini ndiyo huwa wabanagiza kwenye ualimu, siasa,na ukarani. Ambao baadae hubabaisha na kuwa watawala kama hawa tulionao waona leo.
Muundo huu hauko fair wale failures ndiyo wanaopata nafasi ya kuwatawala wenye uwezo kiakili na na wataalamu.

  1. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee dharau?
  2. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee Udhaifu?
  3. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee ufisadi?
  4. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee madini yetu na mitaji yetu kuondoka hali tukifurahia?
  5. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee watawala badala ya viongozi?
  6. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee badget zisiyoeleweka?
  7. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee kauli za akina Pinda?
  8. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee Gilba na safari nyingi za nje ?
Wabangaizaji (Wasanii) chaka lao ni uongo na uzushi na kukimbilia vyombo vya habari ili wasikike, wahurumiwe, wasifiwe na waonekane kama wao ni wanachapakazi (tunao mawaziri wengi tuu wa design hizi)
Shule iliwashinda wakakwama kidato cha nne ama hata darasa la saba, lakini kwa vile sasa wamepata kujipenyeza wanajitahidi kujustfy kuwa na wao wamesoma kwa kuupenda UDr. Wa uzamili hata kama ni wa kupewa kwa heshima wasizostahili.
hawachelewi kukimbilia digree za uzamili ili waitwe DR. kisa tuu wanapenda wawe na akili ambazo hawana.
Jamani nyinyi wasanii, sis wananchi tunajua kwamba nyinyi mlishindwa shule na ndiyo maana mkapita mlango wa nyuma kufikia hapo mlipo. HHeshimuni taaluma kwa maana yale ambayo nyinyi mlishindwa wenzenu waliyaweza na ndiyo maana wapo hapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu.
Kusoma ni kazi ngumu sana na ndiyo maana nyinyi mlichemsha, kusoma ni gharama kubwa sana ndiyo maana watoto wa wakulima mmebangaiza kufika huko mliko.
Basi angalau jambo dogo tuu mnalotakiwa kulifanya, wasikilizeni Madr. Hawa badala ya kutumia vyombo usanii wenu kuwagombanisha na wananchi. Walichonacho nyinyi hamna na wala hamtaweza kukipata kwa vyovyote.
Punguzeni kutegemea INDIA, SOUTH AFRICA, KENYA,UK ili muwwezeshe maDk. Wetu. Haipendezi hata kidogo na wmnatujengea hasira sana wananchi kama hamjui. Msione vinaelea jamani vimeundwa

Tunategemea India, South Africa na Kenya kwa sababu mbili nchi yetu haina vifaa kwenye mahospitali na pili madaktari wa siku hizi wana elimu za kuunga unga sio mabingwa kama madaktari wa zamani enzi zetu tunasoma bila division one mwanafunzi haendi Muhimbili kusoma udaktari na mwenye division two PCB alienda pharmacology lakiini siku hizi madaktari hata divisheni ya tatu wanaenda kwenye vyuo binafsi au unakuta walifeli form four wakaenda kuwa Medical Assistant ambayo ni Clinical Officer siku hizi kisha wakaomba kusoma udaktari tena.

Kwahiyo hoja yako kuwa madaktari ni vichwa darasani sio kweli hao ni madaktari wa zamani nina jamaa niliwaacha form four hawakuendelea form five maana walikuwa na divisheni ya tatu wakaenda kusoma Clinical Officers baadaye wakaenda Bugando kuchukua degree ya udaktari na leo hii ni madokta pamoja na udaktari wao na mimi nilienda kusoma uchumi heshima nyingi maana wanajua niliwamwaga darasani. sasa basi taaluma haimaanishi mtu fulani alikuwa mkali sana bali ni division of labor and speciallization mfano huyo rafiki yangu daktari aliyeunga kwenye mtihani wa form four biology alipata C wakati mimi nilipata B na chemistry alipata D wakati mimi nilipata B bahati mbaya mie udaktari hakukuwa wito wangu ingawa baba yangu alikuwa daktari nilienda form five Tambaza kwa EGM maana PCB haikuwa chaguo langu na kama lingelikuwa chaguo langu ningelichaguliwa maana Physics nayo nilipata C na nilikuwa na division one point 14.
 
mimi sitakujibu. Nadhani si busara kulinganisha vitu visivyowiana.
Mbunge ni Mtanzania YEYOTE mwenye umri wa miaka 21+, akili timamu na anayejua kusoma na kuandika; kisha akachaguliwa au kuteuliwa kuingia mjengoni.
Udaktari ni TAALUMA, tena RARE PROFESSION.
Pima mwenyewe.
 
unaulizwa swali gani?
mtafute kigwangala umuulize kama alipo amua kuwa mbunge na kuacha udk aliamua kuwa bora au duni
 
unaulizwa swali gani?
mtafute kigwangala umuulize kama alipo amua kuwa mbunge na kuacha udk aliamua kuwa bora au duni

...unaweza kwenda kuwa daktari Kenya, France, etc. lakini huwezi kuwa mbunge hapo Taveta.
 
...unaweza kwenda kuwa daktari Kenya, France, etc. lakini huwezi kuwa mbunge hapo Taveta.

mkuu sioni points hapo kufanya kazi nje sio sababu ya ubora wa kazi ni kutokana na mahitaji tu huko huendako, pia unaweza kwenda kuwa muosha vyombo,barmaid hotelini ulaya, marekani, italy, lakini ukashindwa kuwa mbunge ubungo kama hauna sifa, nafikiri ni vyema kutenganisha professionals na hizi kazi ambazo hazina mwenyewe bora tu watu wakuhisi una akili timamu.
nataka nikuakikishie sio kila dr anauwezo kuwa expert nje ya nchi, vilevile hakuna profession ambayo watu wake hawatoki nje ya nchi kama ma expert, kama unajua nijulishe nami nifahamu
NI VYEMA KUWAFANYA MA-DR WAKAWA NA PEACE OF MAIND ILI WAHUDUMIE WATU VYEMA.
 
Hilo ndio tatizo la madaktari wanadhani na kujiona kuwa wao ni muhimu kuliko watumishi wengine wote.Watumishi wote wa umma ni muhimu kila mtu kwa nafasi yake.Wote ni muhimu.Hiyo waliyonayo madaktari ni SUPERIORITY COMPLEX
chagua kimpja kati ya mbunge na daktari nani muhimu?usitueleze upuuzi wako
 
Tunategemea India, South Africa na Kenya kwa sababu mbili nchi yetu haina vifaa kwenye mahospitali na pili madaktari wa siku hizi wana elimu za kuunga unga sio mabingwa kama madaktari wa zamani enzi zetu tunasoma bila division one mwanafunzi haendi Muhimbili kusoma udaktari na mwenye division two PCB alienda pharmacology lakiini siku hizi madaktari hata divisheni ya tatu wanaenda kwenye vyuo binafsi au unakuta walifeli form four wakaenda kuwa Medical Assistant ambayo ni Clinical Officer siku hizi kisha wakaomba kusoma udaktari tena.

Kwahiyo hoja yako kuwa madaktari ni vichwa darasani sio kweli hao ni madaktari wa zamani nina jamaa niliwaacha form four hawakuendelea form five maana walikuwa na divisheni ya tatu wakaenda kusoma Clinical Officers baadaye wakaenda Bugando kuchukua degree ya udaktari na leo hii ni madokta pamoja na udaktari wao na mimi nilienda kusoma uchumi heshima nyingi maana wanajua niliwamwaga darasani. sasa basi taaluma haimaanishi mtu fulani alikuwa mkali sana bali ni division of labor and speciallization mfano huyo rafiki yangu daktari aliyeunga kwenye mtihani wa form four biology alipata C wakati mimi nilipata B na chemistry alipata D wakati mimi nilipata B bahati mbaya mie udaktari hakukuwa wito wangu ingawa baba yangu alikuwa daktari nilienda form five Tambaza kwa EGM maana PCB haikuwa chaguo langu na kama lingelikuwa chaguo langu ningelichaguliwa maana Physics nayo nilipata C na nilikuwa na division one point 14.
Hao madokta bingwa wa huko unakosema wanadivision one unavyofikiri?mi nafikiri tatizo ni vifaa tu,bajeti kubwa ingepelekwa afya na sisi tungekuwa hatuna haja ya kwenda india,Dr Bake ni muhindi?
 
I meant Udaktari ni profession (popote), lakini Ubunge ni ujanja wa mjini tu, ndani ya mipaka. Hivyo ujanja ujanja usitufanye tudharau professions.
 
mkuu sioni points hapo kufanya kazi nje sio sababu ya ubora wa kazi ni kutokana na mahitaji tu huko huendako, pia unaweza kwenda kuwa muosha vyombo,barmaid hotelini ulaya, marekani, italy, lakini ukashindwa kuwa mbunge ubungo kama hauna sifa, nafikiri ni vyema kutenganisha professionals na hizi kazi ambazo hazina mwenyewe bora tu watu wakuhisi una akili timamu.
nataka nikuakikishie sio kila dr anauwezo kuwa expert nje ya nchi, vilevile hakuna profession ambayo watu wake hawatoki nje ya nchi kama ma expert, kama unajua nijulishe nami nifahamu
NI VYEMA KUWAFANYA MA-DR WAKAWA NA PEACE OF MAIND ILI WAHUDUMIE WATU VYEMA.

Je kwani ubunge ni taaluma,umeshawahi kusikia mbunge amekuwa expart kutokana na ubunge,au kunasehemu mtu alipewa ubunge kutokana na experience yake ya kuwa mbunge,lkn doctor anaweza kuwa expart kutokana na taaluma yake je ni yupi hasa wakumthamini, anayetumia mdomo wake kwa kuongea bila vitendo au yule anayekwenda maabara na vifaa,
 
Hivi ni kitu gani kinachofanya wabunge kulipwa mshahara usiopungua milioni kumi ,(10,000,000) ,hebu mnaojua tufafanulieni hapa na tukilingansha na hawa waliogoma ambao ni madaktari ,ili tuongeze upeo wa kuona ,angalau serikali kama muajiri au wabunge si waajiriwa wa serikali ? Naomba kuwasilisha hoja ambayo naamini na wengine watapenda kujua ,sababu za mshara wa wabunge kuwa na mshahara uliovuka mipaka.
 
....wao ni katika orodha ya viongozi...
....wao ndio wanafikiri juu ya nchi hii...
....wengine ni watendaji tu...
 
kila mmoja ana umuhimu wake; kilicho kosekana ni balance ya maslahi. ila kwa upande mwingine dokta ana haso sana hadi kufikia hapio alipo tofauti na ubunge kwani wengine wapo mjengoni sababu ya umaarufu na vijisenti.
 
Back
Top Bottom