MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Suala Katiba mpya limekuwa agenda ya muda mrefu la lakini pamoja na umuhimu wake kwa taifa, kwa kiasi kikubwa limebebwa na Chadema pamoja na wanaharakati wanaokiunga mkono chama hicho cha kisiasa.
Kupata Katiba mpya ni jambo muhimu, lakini Chadema imesau kwamba, suala hilo siyo jambo dogo kama wanavyofikiria, na kwamba Katiba ni mali ya wananchi wote na siyo kipaumbele cha chama hicho kwa maslahi ya kuchukua mamlaka.
Chadema inataka mabadiliko ya Katiba kwa maslahi ya kukamata Dola, imeshindwa kuwaelimisha wananchi kuhusu hata hii Katiba ya sasa ambayo wanasema ina upungufu. Watanzania walio wengi hawajui hata vipengele ambavyo wanasiasa hao wanasema vina kasoro au vinahitaji kuboreshwa kwenye Katiba iliyopo, lakini Chadema wameruka vihunzi na kutaka Katiba mpya badala ya kuwaeleza kwa mapana vipengele vyote vya sasa.
Katiba mpya ni nzuri na muhimu, lakini inaweza isiwe suluhisho la kudumu kwa kuwa tumeshuhudia hata kwa jirani zetu hapo Kenya, ambao wanayo Katiba mpya, wanayo Tume Huru ya Uchaguzi, lakini bado wameendelea kupiga kelele kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii na kisiasa.Malalamiko kuhusu uchaguzi usio huru yameendelea kuwepo, maandamano ya kupinga Serikali yanaendelea kila wakati, pengine wakidai maisha bora.Kwa maana hiyo, wakati mwingine siyo Katiba inayoleta changamoto, bali miongozo mizuri yenye kuleta maendeleo kwa wananchi kujikwamua kiuchumi ndiyo inayotakiwa.
Kuhusu uwekezaji katika bandari, Chadema pamoja na wanaharakati wengine wamekuwa wakizua mijadala mirefu ya kupinga uwekezaji huo, licha ya Serikali imekwishasema mara kadhaa malengo, nia na madhumuni ya kuingia makubaliano ya uwekezaji baina yake na Dubai kupitia kampuni ya DP World, kwamba inataka kuona ufanisi katika Bandari hiyo ambayo ni kitovu cha uchumi wa Taifa.
Kwamba, kwa hali ya sasa ufanisi ni mdogo licha ya jitihada zilizokuwa zimefanyika kabla.
Lakini pamoja na ufafanuzi unaotolewa mara nyingi, suala hilo limebebwa na Chadema kama agenda yao kubwa, na mbaya zaidi wanapotosha ili tu kuwavutia wananchi wawaunge mkono.
Ukiwauliza Chadema kuhusu sababu zao za kupinga uwekezaji huo nini wanashindwa kutoa majibu stahiki na hata vipengele wanavyovitaja kwamba vina kasoro tayari vimekwishafafanuliwa na Serikali kwa marefu na mapana, lakini hawataki kuukubali ukweli na wanaendelea kupotosha.
*Ukweli ni kwamba Chadema wanatamani sana kuona Rais Samia anashindwa katika vita hivi vya uwekezaji, lakini mioyoni mwao wanatamani pia kama haya anayoyafanya ndiyo wangekuwa wanayafanya wao, kwa sababu wanafahamu fika ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam ni ushindi wa kiuchumi kwa Taifa na ni sifa ya hali ya juu ambayo CCM itavunia kwa kusimamia suala hilo ambalo pia litaisaidia CCM kuendelea kukubalika zaidi na wanananchi na kuendelea kuwa imara kisiasa nchini.