Daktari na Mbunge ni yupi mwenye umuhimu sana katika jamii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari na Mbunge ni yupi mwenye umuhimu sana katika jamii?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by combra, Jun 27, 2012.

 1. combra

  combra Senior Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ni mara kadhaa tumeshuhudia mgomo wa madaktari au kwa ujumla katika sekta ya afya na lengo la mgomo wao ni maslahi madogo lakini hakuna siku hata moja tumeshasikia kwa wabungu wanalalanika au kugoma kuwa maslahi ni madogo mara kadhaa wabunge wamekuwa wanalalamika wanapewa posho nyingi wanataka posho ipunguzwe.je maana hiyo mbunge ni mtu muhimu sana nchi hii kushinda daktari anayeponya maisha ya mwanadamu?tafakari
   
 2. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  bora daktari
   
 3. B

  Bob G JF Bronze Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa serikali Dhaifu kama ya ccm Mbunge ni muhimu, but kwa watu makini na waliona maamuzi ya watu Ni Daktari ni muhimu zaidi Mbunge 10,000,000/ na Dr shs 950,000/ watatumaliza hawa ccm. Ukicheka na Ngedele utavuna mabua
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Cha muhimu kila mtu apate stahiki zake tu.. kimsingi walimu nao ni watu muhimu sana ila ndio wanapewa almost nothing
   
 5. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Wanaogopa kuwalipa walimu mshahara mkubwa si unajua wako wengi eti nchi itafilisika.
   
 6. k

  kabindi JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 334
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inategemea na Nchi! kwa Tanzania Mbunge ni bora na that's why analipwa maslahi makubwa. Just imagine prof. Maji marefu mganga wa kienyeji na darasa la saba na wengineo kama hao wanawashinda Madaktari kwa maslahi yanayolipwa kutoka serikalini wakati doctor pamoja na kukaa darasani muda mrefu lakini kazi zao zina changamoto nyingi.
   
 7. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tATIZO NI KWAMBA SERIKALI HAIWATHAMINI WATAALAMU WAKE, SIO MA DAKTARI TU. NCHI HII UKIWA MTAALAM HALAFU UKAAJIRIWA JIANDAE KUADHIRIKA.NDIO MAANA UTAKUTA WATAALAMU WAKUBWA WANAACHA TAALUMA ZAO NA KWENDA KUGOMBEA UBUNGE. HAWA MA dR. WAMEJITOLEA KUDAI HAKI KWA NIABA YA WENGINE TUWAUNGE MKONO.
   
 8. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hili ndio tatizo kubwa bro>>>>yaani inatia hasira sn wanasiasa wanalipana vizuri aslafu wanajipambanua wao ni watawala na ukiangalia hata ionput yao kwenye taifa hakuna zaidi ya kujilimbikizia mali
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Katika katiba mpya wabunge kupata mshahara wa katikati yaani wastani ya mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Hii itawafanya wakumbuke watumishi wengine. Kama hutaki ubunge acha sisi tupo.
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Mimi naona tupige kura ya maoni kuchagua ni kipi kifutwe kati ya kada ya madaktari na wabunge/madiwani ili pesa zitakazopatikana zitumike kuboresha kile kitakachobaki. Yaani kura ikiamua bunge lifutwe basi pesa zote za bunge zipelekwe kuboresha kipato na mazingira ya kazi ya madaktari na kama watu wataamua kada ya udaktari ifutwe basi pesa zote zinazoelekezwa kwa madaktari zipelekwe kuboresha kipato na mazingira ya kazi ya wabunge/madiwani.
   
 11. ndinga

  ndinga Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na mimi ni mmoja wao
   
 12. ndinga

  ndinga Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huko Malawi mbunge ni mtu wa kawaida kabisa lakini hapa bongo mmh!!
   
 13. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kwangu mm bora mwalimu
   
 14. K

  Kiyoya JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  950000 tulinge! hii ni kabla ya kodi-take home ni 695,000
   
 15. M

  Murrah Senior Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabunge wote wakiondoka hatutafaham labda hazina kutakuwa na pesa kiasi. Dr aondoke siku moja malaiki Israel anakuwa busy sana. Kwa kuwa wabunge sio muhimu hawakai sehemu zao za ajira wako dom tu wanapunga upepo na kula uroda na wake au waume za watu magamba
   
 16. Ng'wanambula

  Ng'wanambula Senior Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hilo ndio tatizo la madaktari wanadhani na kujiona kuwa wao ni muhimu kuliko watumishi wengine wote.Watumishi wote wa umma ni muhimu kila mtu kwa nafasi yake.Wote ni muhimu.Hiyo waliyonayo madaktari ni SUPERIORITY COMPLEX
   
 17. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WanaJF. Nashindwa kuelewa kwa nini dunia haiko fair kiasi hiki, inakuaje majitu failures (Div IV na O) yawe ndiyo yenye maamuzi makubwa kuliko learned people?
  Hakuna mwanasiasa hata mmoja kwenye sayari hii mwenye record ya kuwa mwenye akili bora kati ya wahitimu wote unaowafahamu, isipokuwa kubebwa na kupelekwa.
  Walichonacho ma Dr. Kipo kichwani mwao siyo funguo kwamba watanyang’anywa na kupewa mtu mwingine, ni uwezo wao ambao upo ndani yao.
  Mgogoro wa maDr. Na serikali unanikumbusha jinsi ambavyo **** anavyojaribu kumpa vitisho mwerevu. Kama zile khadithi za zamani za Abunuwasi.
  Tafiti sahihi zimeonyeshwa kwamba, Wakati tukiwa shule tunasoma wanafunzi :

  1. wale wanoongoza darasani ama wenye uwezo mkubwa wa akili darasani huwa wanaelekezwa kusomea Udakatari na uinjinia,
  2. wale wa waoshika nafasi za katikati huwa wanaelekezwa kuwa wahasibu, watawala, na masoko,
  3. wale wanaofeli akina Div. IV and kushuka chini ndiyo huwa wabanagiza kwenye ualimu, siasa,na ukarani. Ambao baadae hubabaisha na kuwa watawala kama hawa tulionao waona leo.
  Muundo huu hauko fair wale failures ndiyo wanaopata nafasi ya kuwatawala wenye uwezo kiakili na na wataalamu.

  1. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee dharau?
  2. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee Udhaifu?
  3. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee ufisadi?
  4. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee madini yetu na mitaji yetu kuondoka hali tukifurahia?
  5. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee watawala badala ya viongozi?
  6. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee badget zisiyoeleweka?
  7. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee kauli za akina Pinda?
  8. Kwa ukweli huu kwa nini tusitegemee Gilba na safari nyingi za nje ?
  Wabangaizaji (Wasanii) chaka lao ni uongo na uzushi na kukimbilia vyombo vya habari ili wasikike, wahurumiwe, wasifiwe na waonekane kama wao ni wanachapakazi (tunao mawaziri wengi tuu wa design hizi)
  Shule iliwashinda wakakwama kidato cha nne ama hata darasa la saba, lakini kwa vile sasa wamepata kujipenyeza wanajitahidi kujustfy kuwa na wao wamesoma kwa kuupenda UDr. Wa uzamili hata kama ni wa kupewa kwa heshima wasizostahili.
  hawachelewi kukimbilia digree za uzamili ili waitwe DR. kisa tuu wanapenda wawe na akili ambazo hawana.
  Jamani nyinyi wasanii, sis wananchi tunajua kwamba nyinyi mlishindwa shule na ndiyo maana mkapita mlango wa nyuma kufikia hapo mlipo. HHeshimuni taaluma kwa maana yale ambayo nyinyi mlishindwa wenzenu waliyaweza na ndiyo maana wapo hapo kwa ajili ya kuokoa maisha yetu.
  Kusoma ni kazi ngumu sana na ndiyo maana nyinyi mlichemsha, kusoma ni gharama kubwa sana ndiyo maana watoto wa wakulima mmebangaiza kufika huko mliko.
  Basi angalau jambo dogo tuu mnalotakiwa kulifanya, wasikilizeni Madr. Hawa badala ya kutumia vyombo usanii wenu kuwagombanisha na wananchi. Walichonacho nyinyi hamna na wala hamtaweza kukipata kwa vyovyote.
  Punguzeni kutegemea INDIA, SOUTH AFRICA, KENYA,UK ili muwwezeshe maDk. Wetu. Haipendezi hata kidogo na wmnatujengea hasira sana wananchi kama hamjui. Msione vinaelea jamani vimeundwa
   
 18. W

  WEMBE WENGE Senior Member

  #18

  Punguzeni kutegemea INDIA, SOUTH AFRICA, KENYA,UK ili muwwezeshe maDk. Wetu. Haipendezi hata kidogo na wmnatujengea hasira sana wananchi kama hamjui. Msione vinaelea jamani vimeundwa.
   
 19. combra

  combra Senior Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lkn kumbuka wote wanaumuhimu katika jamii,ila tukumbuke nchi haitawaliki wa kuendelea bila siasa je kwanza tunakubaliana kwa hilo
   
 20. M

  Mwanamutapa JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 499
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kila nafasi ina umuhimu wake katika jamii ingawa tunaweza kusihi bila wabunge lakini kuishi bila madaktari haiwezekani sababu ya magonjwa kuwa mengi katika ulimwengu huu. kuhusu mshahara mbunge ni mwanasiasa haijalishi ana kiwango gani cha elimu maana yeye alichaguliwa na wanachi kwa kuwa ni mheshimiwa anastahili mshahara wa kuridhisha vivyo hivyo na daktari anastahili mshara wa kuridhisha kwa hiyo kinachotakiwa ni daktari kuongezewa mshahara na si mbunge kupunguziwa mshahara ili alingane na daktari.

  Katika nafasi za kisiasa elimu haingaliwi ili mradi umekubalika kwa wananchi ukatengeneze sera na kuongoza ndio maana tuna marais wengi wako au walikuwa na kiwango cha chini cha elimu lakini walikuwa watawala wazuri kuliko wenye elimu au pamoja na elimu zao ndogo walipewa dhamana ya kuongoza mataifa makubwa yenye wasomi wa hali ya juu mfano John Major Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza alikuwa na diploma ya accounting, Lula Da Silva wa Brazil darasa la tatu, Jacob Zuma darasa la nne, Milton Obote form six, ingawa baadaye alianza kuitwa dokta ya kutunukiwa, Mao Zedong form four, Fredrick Chiluba certificate ya accounting na wengine wengi.

  Kuhusu madaktari wana haki ya kudai nyongeza za mishahara kutokana na nature za kazi zao ambazo ni ngumu ila napenda kutoa wito kwa madaktari kwamba ingawa mna haki ya kudai nyongeza za mishahara inabidi kwanza muwe na
  utumishi kazini nimefika mahospitali ya serikali madaktari wengi hamfanyi kazi zenu mpo mpo mnaingia kusaini vitabu na kuondoka kwenda kwenye mahospitali binafsi au mnakuwepo tu maofisini mkisubiri rushwa. nina mfano hai wa ndugu yangu tulimpeleka hospitali ya Mwananyamara alikuwa anahara damu na kupungukiwa maji mwilini manesi na madaktari hawakutujali kabisa wala kuonyesha kuwa tuna mgonjwa mahututi anahitaji huduma za haraka matokeo yake baada ya masaa mawili mgonjwa alifariki pale mapokezi iilikuwa saa saba usiku wakati tumefika pale saa tano usiku

  Mgonjwa alifariki akiwa na umri mdogo sana miaka 19 tu baadaye nesi mmoja alituuma sikio kuwa mgonjwa wetu hakujaliwa kwa sababu hatukutoa rushwa hiyo ilikuwa mwaka 2008 sasa madaktari mnadai kuongezewa mishahara ya nini? kama huduma hamtoi kwanza? toeni huduma kwanza watu wazione ndio mdai nyongeza za mishahara kama huduma hamtoi wengi wenu nyongeza za mishahara ni za nini iwapo kipato mnaongeza kwenye hospitali binafsi na kusubiri rushwa? pamoja na hayo nawapongeza sana madaktari wengi wa hospitali za misheni wengi wao wanachapa kazi pia madaktari wachache wa hospitali za serikali, Maana serikalini madaktari wengi ni wababaishaji hawatoi huduma ni story nyingi kusubiri rushwa na kwenda nyumbani ndio maana huduma ni hafifu kule
   
Loading...