Daktari na Engineer nani analipwa zaidi

nilipiga mahesabu ya kufanya kazi nje ya mshahara. huko kwenye kulipwa kwa mshahara nitaje nani analipwa zaidi, mawazo hayo huwa sipo kabisa. nilishahama kwenye ulimwengu huo.
Duh! Ndugu waniangusha. Utafikaje conclusion kwa kitu kisichopimika? Kwanza hapa wanauliza nani anayelipwa zaidi, sio kipato nje ya mshahara. Hata kama wanauliza kipato cha kila nje ya mshahara, umefikaje kwenye generalisation kama hiyo? Hivi Nikikuuliza Daktari na Wakili yupi analipwa zaidi, utaweza toa jibu sahihi?
 
ngoja nipite kimya maana hapo kwenye kiraji pagumu...najisikia furaha kuwa engineer
Nyingi ndio inaanzia kiasi gani? Ndogondogo zinaanzia kiasi gani? Engineer wangapi wanalipwa kwa mkupuo? Madaktari wangapi wanalipwa kidogokidogo?
 
usiwaze kulipwa mshahara, tunaangalia fursa za kujiajiri ndiko kunakoingiza hela. daktari anaweza kuacha kuajiriwa akaanzisha dispensary ikamwingizia faida ya milioni kumi kila mwezi au zaidi. icho ni kima cha chini. injinia anaweza kupata tenda moja tu kwa miezi sita au kwa mwaka, ikamfuta machozi yote. nasikitika kutosomea udaktari, nilisoma sheria kwa kulazimishwa, na ninaifanya kazi ya sheria pasipokutoka moyoni, pamoja na kwamba katika law firm yangu naweza ingiza hela nyingi sana kwa mwezi kuwapita wote madoctor na mainjinia. kesi moja au tatu tu inanifuta machozi, bado wateja wa kudumu wanaoingiza kwenye account kila mwezi hata kama hakuna kilichofanyika.
Hahahaa acha nicheke mie,unaleta story za kusadikika kwa hawa madr wanaohaha na kuandamana kila siku.Mi nasubir mgomo wa maengineer siku waje sema maisha magumu na mishahara midogo,nahisi magufuli atafukuza wote haooo
 
mkuu hata certified MD anayejielewa hayupo masikini. sema tu kwa hao wawili, kinachowaumiza ni ulevi tu. madoctor na mainjinia wanakunywa sana pombe.
Yani kweli wewe ndo mwanasheria na kuandika andika utoto humu,kama umeingia kwenye hizo fani za afya tulia usijipe moyo humu na uongouongo wako wakitoto.Afu unapata wapi uwezo wa kufafanua vitu wakati hujafanya hata research.KASOME AFYA UPEWE NA MEMBERSHIP ID YA MAANDAMANO KUDAI NYONGEZA YA MISHAHARA
 
Nan analipwa zaidi kati ya daktari na injinia
Hilo swala la mshahara mdogo wangu inategemeana anafanya kazi wapi mfano serikali kuu Tabibu analipwa mshahara mkubwa zaidi ya Muhandisi ila Wahandisi wengi hawajiliwi serikali kuu niwachache kwa sababu wengi wanakua katika Mashirika ya Umma kama TPDC TBS TBA TANESCO TANROAD TOBACCO MAMLAKA YA MAJI MAMLAKA YA BANDARI NHC TTCL huku ndo wanalipa vizuri na ndo Wahandisi wengi wanafanya kazi hivyo wanakua na mishahara mikubwa kuliko Matabibu kwa sababu Matabibu wengi wanafanya kazi chini ya serikali kuu ndo maana ukiangalia wakitaja viwango vya ulipaji wananza na Matabibu Wanakuja Wauguzi na Walimu....Wahandisi hua hawawataji sababu kazi zao nyingi ziko mamlaka ukiwakuta serikali kuu sana ni Halimashauli.
 
Yani kweli wewe ndo mwanasheria na kuandika andika utoto humu,kama umeingia kwenye hizo fani za afya tulia usijipe moyo humu na uongouongo wako wakitoto.Afu unapata wapi uwezo wa kufafanua vitu wakati hujafanya hata research.KASOME AFYA UPEWE NA MEMBERSHIP ID YA MAANDAMANO KUDAI NYONGEZA YA MISHAHARA
unabishana na mwanasheria wakati mwenzio ubishi ni kazi yangu ya kila siku. tutakesha.
 
Duh! Ndugu waniangusha. Utafikaje conclusion kwa kitu kisichopimika? Kwanza hapa wanauliza nani anayelipwa zaidi, sio kipato nje ya mshahara. Hata kama wanauliza kipato cha kila nje ya mshahara, umefikaje kwenye generalisation kama hiyo? Hivi Nikikuuliza Daktari na Wakili yupi analipwa zaidi, utaweza toa jibu sahihi?
wangeuliza "who earns better than the other" ungejibuje? ungejibana kwenye mshahara peke yake au na marupurupu na ushenzi mwingine wa mtaani unaoingiza hela? kwa kawaida, kupata pesa ni akili ya mtu tu. kuna wengine mainjinia lakini vichwa vyao havijakaa vizuri wanabaki tu kuitwa injinia jina, ila hajiongezi. tuseme tu hivyo ili kukata mzizi wa ubishi.
 
Nan analipwa zaidi kati ya daktari na injinia
Mie nafikiri kulipwa zaidi ni issue ya mtu binafsi...

Mfano wewe ukiwa unaipenda kazi yako lazima utaifanya vizuri na mwisho wa siku lazima utalipwa handsomely....

Nafikiri na kuwaza kwa kina; no attachment
 
Kwa salary scale ya Tanzania (serikalini) daktari ana mshahara mkubwa kuliko Mhandisi!

By small chance, angalau Mhandisi mmoja out of 100; anaweza kuwa tajiri sana kuliko daktari yeyote.

By average, madaktari wana uwezekano wa kuwa na maisha mazuri sana (sio matajiri sana as above) kuliko Wahandisi.

Wote wawili wakiwa na akili za kiujasiriamali, daktari ataanza kutengeneza pesa since Day 1 wakati Mhandisi anaweza kuchukua hata miaka!

Hata kama Mhandisi inaweza kumchukua miezi kadhaa au miaka kutengeneza first money; lakini kazi moja tu inaweza kufunika kazi za miaka 10 zilizofanywa na daktari.

Ni rahisi sana kwa daktari kuji-establish lakini Mhandisi anahitaji kazi ya ziada na connection.

Kama unaridhika na average life-- nyumba mzuri (sometimes zaidi ya 1), gari (magari) mzuri, biashara za hapa na pale, mke mzuri and all that... kuwa Daktari.

But kama unaota kuwa na mipesa mingi, fikiria kuwa Mhandisi and Inshallah, Mwenyezi Mungu atakuongoza! However, if you are not lucky na ni kiwango chako cha uvumilivu ni chini ya 70%; basi usione Mungu kakuonea baada ya ndoto yako ya kuwa na mihela mingi kugeuka kuwa kuwa ya kuishi kwa kubahatisha!

Kama unaishi Japan, hurry up... kasomee Uhandisi lakini kama unaishi Tanzania; Uhandisi si taaluma ya kukimbilia angalau kwa sasa to the next 5 years!

Kama bado upo O Level zikangatia yafuatayo:

PCB sio combination ya kukimbilia...! Kwavile tofauti ya Mwanafunzi wa Uhandisi na Udaktari ni Hesabu; fahamu kwamba ni rahisi sana tena sana kufaulu Mathematics kuliko Biology! Kwahiyo kama biology huwa unafaulu kiujanja ujanja, then don't go for PCB na wala usiende PCB kwa kuikwepa M from PCM! Unaweza kusoma PCM kisela lakini PCB unatakiwa kuwa mnoko!
 
usiwaze kulipwa mshahara, tunaangalia fursa za kujiajiri ndiko kunakoingiza hela. daktari anaweza kuacha kuajiriwa akaanzisha dispensary ikamwingizia faida ya milioni kumi kila mwezi au zaidi. icho ni kima cha chini. injinia anaweza kupata tenda moja tu kwa miezi sita au kwa mwaka, ikamfuta machozi yote. nasikitika kutosomea udaktari, nilisoma sheria kwa kulazimishwa, na ninaifanya kazi ya sheria pasipokutoka moyoni, pamoja na kwamba katika law firm yangu naweza ingiza hela nyingi sana kwa mwezi kuwapita wote madoctor na mainjinia. kesi moja au tatu tu inanifuta machozi, bado wateja wa kudumu wanaoingiza kwenye account kila mwezi hata kama hakuna kilichofanyika.
Malipo ya huduma za sheria yanatisha . Is there a law governing the amount claimed, awarded and ultimately
received by advocates for services rendered in all civil matters ?
 
wangeuliza "who earns better than the other" ungejibuje? ungejibana kwenye mshahara peke yake au na marupurupu na ushenzi mwingine wa mtaani unaoingiza hela? kwa kawaida, kupata pesa ni akili ya mtu tu. kuna wengine mainjinia lakini vichwa vyao havijakaa vizuri wanabaki tu kuitwa injinia jina, ila hajiongezi. tuseme tu hivyo ili kukata mzizi wa ubishi.

Sasa hilo litakuwa swali jipya. Na who earns better inategemea na mazingira. Lakini karibu kila sehemu engineer ana mapato less ukilinganisha na daktari (sio kila engineer atakuwa na kampuni ya ujenzi na si kila daktari ana hospitali).

Ukiangalia US, daktari anaongoza kwa kipato, engineer hata hamkaribii. Soma hapa The 30 highest-paying jobs in America

Ukienda UK, utakuwa madalali ndio wana kipato zaidi, hata hivyo daktari anamzidi engineer. Soma hapa What are the UK's highest paid jobs of 2015?

Na ukienda Canada vivyo hivyo, daktari analipwa zaidi.

Kwa hiyo pointi ni kwamba sehemu nyingi waki assess nani analipwa zaidi daktari huwa juu ya engineer, lakini pia huwezi ukafanya generalization kwani mazingira yanatofautiana.
 
Kwa serikali ya magufuli ya kuelekea uchumi WA kati. Kada itakayo kuwa na HELA ni injinia watapata kazi nyingi. Dodoma inajengwa, viwanda, biashara ya mawasilano inazid Kukua lazima mainjia wapige pesa. Kwa Sasa wote wana maisha sawa Kwa wale wanaotegemea mshahara. Ni rahisi Kwa Injinia kutoka kimaisha hasa akipata deal. Daktari asiye jiongeze unakuta anaishi maisha ya kawaida Sana Gari moja.
 
Kama unaongelea madaktari wa type Ya Juma Mwaka ....Hakuna Engineer anae wasogelea kimapato kwa hapa kwetu wale wengine kina Hamis nafikir siasa ndo iliwapa Mpunga .....ila Nafahamu Vijana wengi Tanroad wanavimba inshort we hv more Young doctors in middle class than Young Engineers
 
Dr wa nn?
Engineer wa nn?
Wamesoma chuo gani na wapi?
Wana ishi Bara/nchi gani?
Maswali haya ukjibu utapata majibu saafi sana toka kwa wadau!
 
Sasa hilo litakuwa swali jipya. Na who earns better inategemea na mazingira. Lakini karibu kila sehemu engineer ana mapato less ukilinganisha na daktari (sio kila engineer atakuwa na kampuni ya ujenzi na si kila daktari ana hospitali).

Ukiangalia US, daktari anaongoza kwa kipato, engineer hata hamkaribii. Soma hapa The 30 highest-paying jobs in America

Ukienda UK, utakuwa madalali ndio wana kipato zaidi, hata hivyo daktari anamzidi engineer. Soma hapa What are the UK's highest paid jobs of 2015?

Na ukienda Canada vivyo hivyo, daktari analipwa zaidi.

Kwa hiyo pointi ni kwamba sehemu nyingi waki assess nani analipwa zaidi daktari huwa juu ya engineer, lakini pia huwezi ukafanya generalization kwani mazingira yanatofautiana.
mkuu tunaongelea tz, hapa tupo tz hatupo ulaya. wewe unasoma ukafanye kazi ulaya?hahaha
 
mkuu tunaongelea tz, hapa tupo tz hatupo ulaya. wewe unasoma ukafanye kazi ulaya?hahaha
Hiyo ya kuongelea TZ itabidi uianzishie thread yake, mwanzilishi wa hii thread hakuweka mipaka unayoileta sasa. JamiiForums imevuka mipaka. Kuna watu wako SA, UK, US, KQ n.k.

BTW kuna utafiti wowote umeufanya TZ mkuu zaidi ya hisia au takwimu za kisiasa? Huwezi sema daktari, wakili au engineer aliyepo Tanzania analipwa zaidi kama hakuna chombo kinachokusanya takwimu.
 
Back
Top Bottom