Daktari na Engineer nani analipwa zaidi

Umefikaje kwenye hiyo conclusion? Analipwa zaidi katika terms zipi? Mshahara wa Kitanzania? Tutajie scale zao wakiajiriwa hapa serikalini.
nilipiga mahesabu ya kufanya kazi nje ya mshahara. huko kwenye kulipwa kwa mshahara nitaje nani analipwa zaidi, mawazo hayo huwa sipo kabisa. nilishahama kwenye ulimwengu huo.
 
mkuu hata certified MD anayejielewa hayupo masikini. sema tu kwa hao wawili, kinachowaumiza ni ulevi tu. madoctor na mainjinia wanakunywa sana pombe.
Sio wote mkuu, wapo waadilifu sana na maisha yao yako poa sana
 
Mfanya biashara analipwa kuliko hao wote mkuu!
umesahau kuwa kwamfano daktari aliyejenga dispensary pia anafanya biashara. zaidi ya yote, ujue hakuna biashara inayolipa kama biashara ya kuuza huduma/services. hapa namaanisha injinia na daktari, mwanasheria, auditor etc akipata tenda moja wewe mfanya biashara kuja kupata faida ya lumpsum kama hiyo utakesha. na hapohapo tukiwa mainjinia, madoctor etc tukipata hela tunafanya na biashara vilevile, hivyo tupo sambamba.
 
Huwezi pata jibu la kutosha. Daktari au Engineer Wa muda gani kazini ? Anayefanya kazi taasisi gani? Mwenye level gani ya elimu? Anayefahamika na kiongozi gani?.....
 
umesahau kuwa kwamfano daktari aliyejenga dispensary pia anafanya biashara. zaidi ya yote, ujue hakuna biashara inayolipa kama biashara ya kuuza huduma/services. hapa namaanisha injinia na daktari, mwanasheria, auditor etc akipata tenda moja wewe mfanya biashara kuja kupata faida ya lumpsum kama hiyo utakesha. na hapohapo tukiwa mainjinia, madoctor etc tukipata hela tunafanya na biashara vilevile, hivyo tupo sambamba.

Wala!!....Enterprenuership ni fani inayojitegemea!....ukiona daktari au enginia akifanya biashara ujue hizo ni mbwembwe tu na wala siyo enterprenuership!!....Sifa kubwa ya enterprenuership ni kuwa full commited in term of time,skills,money e.t.c sasa hao madokta na mainginia wanapata mda saa ngapi wa kuwa full commited in term of time???
 
Hivi dangote ni injinia au dokita!?
hahaha, hesabu tz au africa yote kuna madangote wangapi? najua tz tunaye mmoja baba tifan. tunachoongelea hapa ni average ya watu hasa wa middle class na kuendelea, sio hao mabilionea. ukitaka kufikiri kidangote, hata shule hautaenda. chukua watz mil. 40, angalia kwa wale waliosoma ni kada gani imefanikiwa zaidi kuliko zingine.ndicho tunachoongelea.
 
Aise uko vizuri kweli kweli, la saba ushaanza kuwazia mshahara!!...hii inaonyesha una malengo makubwa sana maishani...kwa ushauri tu ni kwamba fanya taaluma ambayo una interest nayo...pesa siyo kila kitu na pesa inakujaga tu bila kujali umesomea taaluma gani, na hakuna formula kwamba taaluma flani ndo inalipa kuliko nyingine, inategemea na opportunities ambazo ziko kwenye taaluma yako, kwa muda huo na katika sehemu uliyoajaliwa. Unaweza kuwa journalist ukapiga pesa kuliko hata engineer au daktari. Au unaweza kusomea udaktari halafu ukawa unalipwa laki 8, wakati mwenzako engineer analipwa 10m, au unaweza kuwa engineer unalipwa 1m wakati dr analipwa 5m na ana muda wa kufanya kazi za nje na zikampa pesa kibao.
 
Wala!!....Enterprenuership ni fani inayojitegemea!....ukiona daktari au enginia akifanya biashara ujue hizo ni mbwembwe tu na wala siyo enterprenuership!!....Sifa kubwa ya enterprenuership ni kuwa full commited in term of time,skills,money e.t.c sasa hao madokta na mainginia wanapata mda saa ngapi wa kuwa full commited in term of time???
hizo ni theory mnazofundishwa madarasani mkuu. nenda kwa daktari aliyemaliza tuseme muhimbili miaka yake saba, uone unachokikuta pale.

1. kabla ya kumuona utatakiwa kutoa fee ya kueleweka

2. utanunua dawa toka kwenye duka lake palepale

3. akitaka kukufanyia upasuaji au matibabu yeyote atakutajia kiwango. mfano, upasuaji private kama mkeo ana mimba ujiandae laki si chini ya saba. kwa siku anapokea wajawazito wangapi? fikiri.

4. ukilala kwenye wodi yake, utalipia kitanda kwa siku kama vile upo hotelini/lodge.​

sasa hiyo unaiita ujasiriamali au sio ujasiriamali? au wewe unafuatilia kila mstari uliopo kwenye vitabu ulivyosoma badala ya kuja kwenye uhalisia? kuna doctor anayetoa matibabu kwa msaada? kuna injinia anakujengea barabara au mtambo kwa msaada? si unatoa advance kwanza kabisa mkuu?
 
Inakuwaje mtu makini kama wew unatoka nje ya mada mkuu!
Nimefanya makusudi mkuu kwa sababu siku hizi utakuta mwanafunzi eti anaenda kusoma somo fulani kwa sababu lina hela sana kwa mfano kuna rafiki yangu anapigania kwenda kufanya kazi TRA kisa 'kuna hela sana' wakati lengo la elimu ni kuikomboa jamii na dunia nzima kwa ujumla!!.....mimi lengo langu nilitaka kumkumbusha dogo kuwa kama anataka hela aingie kwenye biashara na siyo kwenda kusoma ili afanya kazi TRA or whatever ili aibe kodi za wananchi kama tulivyokuwa tunashuhudia kwenye nchi hii kwa miaka mingi!!
 
Hizo hela anazozipata kwenye issue kama hizo ni hela ya madafu tu huwezi kucompare na mtu ambae amejicommit kwenye biashara!!
 
Nimefanya makusudi mkuu kwa sababu siku hizi utakuta mwanafunzi eti anaenda kusoma somo fulani kwa sababu lina hela sana kwa mfano kuna rafiki yangu anapigania kwenda kufanya kazi TRA kisa 'kuna hela sana' wakati lengo la elimu ni kuikomboa jamii na dunia nzima kwa ujumla!!.....mimi lengo langu nilitaka kumkumbusha dogo kuwa kama anataka hela aingie kwenye biashara na siyo kwenda kusoma ili afanya kazi TRA or whatever ili aibe kodi za wananchi kama tulivyokuwa tunashuhudia kwenye nchi hii kwa miaka mingi!!
Nia yako ni njema, ungemshauri kuwa ni vyema asomee anachokiweza na kilichopo moyoni zaidi ya kusoma kwa ajili ya maslahi mazuri
 
Aisee engineer. Anahela uwiiiii kuna madogo unafanya nao kazi wana diploma tuu ila hela wanaochukua ni ndefu Hadi unawaonea wivu ukiangalia wadogo
 
mkuu hata certified MD anayejielewa hayupo masikini. sema tu kwa hao wawili, kinachowaumiza ni ulevi tu. madoctor na mainjinia wanakunywa sana pombe.
Aiseee umenena yani doctor wote ninaojuana nao ni walevi hatari
 
mkuu hata certified MD anayejielewa hayupo masikini. sema tu kwa hao wawili, kinachowaumiza ni ulevi tu. madoctor na mainjinia wanakunywa sana pombe.

ngoja nipite kimya maana hapo kwenye kiraji pagumu...najisikia furaha kuwa engineer
 
Daktari analipwa nyingi lakini kidogo kidogo kulingana na hospitali ngapi anatoa huduma lakini injinia analipwa nyingi kwa mkupuo mmoja
 
Back
Top Bottom