Daktari Mkuu, mpe mgonjwa Rufaa

Daktari Mkuu, mpe mgonjwa Rufaa

Hapakaztu

Member
Joined
Apr 7, 2023
Posts
6
Reaction score
9
Habari Watanzania,

Wenzangu, ni dhahiri kabisa kwa sasa huyu mgonjwa Tanzania yupo hoi hoi bin taabani tunamuomba daktari mkuu anayemhudumia sasa akubali ampe rufaa kwa specialist mapema asubuhi ya mwaka 2025.

Hii itakuwa salama kwake daktari ili mgonjwa asije mfia mikononi mwake ikizingatiwa na jinsi yake atawaharubiwa na wengine naona uamuzi mzuri kwake ni kumpa rufaa mgonjwa kwa specialist.

Asante Daktari mkuu kwa kumhudumia mgonjwa huyu tafadhali usiangalie faida ya pesa za mgonjwa anazo lipia huduma katika kituo chako tafadhali 2025 mpe rufaa akikufia mikononi mwako jua kabisa ndugu za wagonjwa vizazi na vizazi hawatakusamehe na baada ya kifo cha mgonjwa hautaishi kwa amani maana ndugu wa marehemu watakusimanga na kukutwezwa daktari.

Tafadhali mpe rufaa mgonjwa kwa ajili ya faida za wengi asante kwa huduma yako nzuri.
 
Back
Top Bottom