Daktari feki aliyekamatwa Muhimbili aibukia tena Amana kutapeli watu. Huyu hapa akiwa amebananishwa

Daktari feki aliyekamatwa Muhimbili aibukia tena Amana kutapeli watu. Huyu hapa akiwa amebananishwa

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu,

Yaani huyu jamaa bhana hata kujieleza hawezi. Amejikanyaga sana.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana inamshikilia Daktari feki anayejulikana kwa jina moja Mussa aliyetaka kuwatapeli Wagonjwa katika Hospitali hiyo.

Mgonjwa mmoja aligundua kuwa Daktari huyo ni feki ndipo akaamua kuujulisha Uongozi wa Hospital ya Amana na Daktari huyo feki kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Aidha, Daktari huyu Feki aliwahi kukamatwa Mwaka jana August 30, 2023 akitapeli Wagongwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Soma pia: Daktari FEKI akamatwa Muhimbili

Hebu msikilizeni wenyewe hapa

 
Huyo sio mwajiriwa wa hapo ila sio daktari feki ,kazi ya udaktari hauwezi kuwa haujui kila kitu.
 
Feki wakiwa wengi wanawaharibia wasio feki kama ilivyotokea kwa waganga wa kienyeji.
 
IMG_0827.jpeg
 
Daktari Feki, kama ana qualification apelekwe akasomee udaktari, kama hana amiminiwe mvua kwa kuchezea maisha ya watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom