DAKTARI AOMBA RUSHWA LAKI NA NUSU, wanawake laivu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAKTARI AOMBA RUSHWA LAKI NA NUSU, wanawake laivu...

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ubungoubungo, Sep 29, 2012.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kuna kipindi cha wanawake laivu niliona siku moja, kuna ushuhuda wa mama mmoja alihojiwa hadi kiria akatoa mchozi.....kwa wale walioona na kusikia watakumbuka hili, ndo nilijiuliza hawa madoctor mbona hawana huruma?...mama mjamzito hadi alifikia kupata fistula, hadi leo hii, kwasababu ya laki moja na nusu. maelezo yalikuwa hivi....

  1. MAMA alikuwa mjamzito, akaenda muhimbili, alipofika doctor akampima akasema kuwa asubiri kidogo mtoto ashuke.

  2. mama alipoona mtoto ameshuka akamwita doctor na nesi, lakini walipokuja uchungu ukawa umepungua, si unajua uchungu huwa unakuja na kuondoka wakati mwingine.

  3. ikafika kipindi doctor akamwambia mama aende nyumbani tu kwasababu uchungu wake hata zaa leo, au labda alete laki moja na nusu ili amzalishe...that means kulikuwa na possibility kuzalishwa laini si kwa mkono mtupu, laki na nusu.

  4. mama alikuwa hana pesa hiyo, laki na nusu, ikabidi aondoke tu aende home. alipofika kwenye daladala, uchungu ukamkamata tena, akajifungua mle kwenye daladala..sijui yalikuwa magari ya mbagala siju wapi..nimesahau.

  5. maisha yakaendelea, lakini kuanzia siku hiyo, wakilala tu bila kujijua mama alikuwa anastukia godoro limelowa. akikaa akisimama anakuta kiti kimelowa mkojo...mwanzo alikuwa hajui, alipoenda hospitali akakutwa amepata fistula, tena si ya kibofu cha mkojo tu, ni kwamba hadi ya rectum...utumbo mpana umechanika pamoja na kibofu hivyo kinnyesi pia kinatokea kwenye vvagina pamoja na mkojo mfululizo.

  6. sijui ni kwasababu gani, yule mtoto alikaa miezi kadhaa akafariki, labda kutokana na kukosa huduma nzuri siku ile anajifungua mabarabarani mbele za watu na kwenye daladala. akawa amepoteza mtoto aliye mzaa kwa shida ya kukosa laki na nusu, na laki na nusu ikawa imemsababisia apate fistula ya haja kubwa na kibofu. hadi leo hii bado anaumwa fistula, na mtoto alishakufa.

  7. hii ndo hali halisi, laivu bila chenga ya wanawake wetu wanapoenda huko hospitali.

  8. kiria alienda hadi kwa doctor kumhoji, doctor alimwambia kuwa amemsahau yule mama hamkumbuki, mama kang'ang'ania kuwa "doctor umenisahau wakati uliniomba laki na nusu na kunirudisha home kwasababu sikuwa nayo?...wanabishana, doctor amemruka na akasema kama alikosea pengine ilikuwa kwasababu ya uchovu au ni makosa ambayo mwanadamu yeyote anaweza kuyafanya bila kukusudia ila hakumwomba laki na nusu.

  9. nesi anaulizwa anasema, yap, alitakiwa ajitahidi, mkono mtupu haulambwi au la angeenda hospitali za kulipia huko, hakuna vya bure siku hizi, mbona mkienda hospitali za binafsi mnatoa hela nyingi hata iyo laki na nusu ndogo? nesi alifunguka ajabu hadi nilijiuliza alikuwa haoni kamera?

  WHAT DO YOU THINK ABOUT THIS, na hawa ndo watu wanaoogoma na kutelekeza watu wafe, kumbe rushwa wanapokea sana na madawa yetu wanaiba sana...think about it, angekuwa ndo mke wako ingekuwaje? ungejisikiaje? utu wa mwanamke uko wapi hapa, hivi hata kama jamani wamekasirishwa ndo wafanye hivi kwa wamama wajawazito ambao wako nusu kuishi nusu kifi? kwani hata madoctor hawakuzaliwa na mwanamke? hawa jamaa ..duh...
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kiria tunaomba tuwekee ile clip hapa tuisikilize.
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ngumu kumeza!
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  acha nesi afunguke maana wamekataa kuwaongezea mishahara! Haya ndio madhara ya migomo baridi.
   
 5. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Kipindi kimemaliza Kazi yake. Kinachofuata? Nani wa kumchukulia hatua nani??
   
 6. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walipewa kanga,kofia, na pesa sasa mnalia nini?
   
 7. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  angekuwa mkeo au dadako ndo amepata fistula ungeongea haya unayoongea? au labda wewe ulipokuwa unazaliwa, maza ako ndo angepata fistula, ndo ungeishi na kukua ukiwa unaijua fistula ilivyo, na maneno haya yasingethubutu kutoka mdomoni mwako. hujui ulitendalo. hata kama watakuwa walipokea kofia na vitenge, au hata kama wangefanya chochote kila, our women don't deserve this kabisa. they really do not have to be treated that way. by the way, kuwa ccm au cdm ni uamuzi tu wa mtu, na hatupo vitani hapa, sio kwamba ukiona mtu yuko ccm basi unaomba mabaya yamkute hata apate shida kama iyo ndo furaha yako,....sidhani kama siasa za chuki kama wewe zitasaidia. zaidi ya yote usikute huyo mama ni mwanachadema au cuf, na wala si mwanasisiemu. angekuwa ameshafaidika na ccm angekuwa na laki na nusu atoe ili mtoto wake apone na asipate fistula. ukifuatilia utakuta hajafanya chochote kusapoti ccm na pengine ni mpiganaji mmoja wapo huko uswahilini.
   
 8. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Tusidanganyane hapo, si mlisema mgomo umeisha? Madaktari wameamua kunyamaza maana hata serikali yao imesema haina kitu cha kuongea nao. Msiwalalamikie madokta bali ilalamikieni serikali (yetu) ndiyo inayoua. Ni nchi gani mmesikia madokta wanadharauliwa kama bongo? uzeni mali zenu nendeni Regency, tena mtawakuta haohao mnaowakandia muhimbili, lakini wanajituma kwa sababu hawaendi majumbani mwao migongo imejikunja na kukanyagana ndani ya daldala baada ya kuona wagonjwa kedekede kama wa muhimbili. Mlishangilia JK akizodoa madokta, chekeleeni sasa matokeo ndo hayo.
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ubungoubungo, sielewi kwa nini inakuwa rahisi sana kwetu wananchi kuwalalamikia madaktari, wauguzi, nk..wakati tunajua Uzembe ulipo!
   
 10. f

  filonos JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  hiyo ni chamdor tu sikuizi wazazi wanaambiwa lete vifaa vyako ikiwa pamoja na PAMBA nk..ukienda kwa choo wanakibia hao MANES the bado dk1.kujufungua unaambiwa lete vifaa vyako kwakua hauvioni wanakuambia lete 30000/tukuletee wanakupa walivyoiba kwa mwingine ni MLADI wa maisha yao hiyo ni TZ...
   
 11. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Bado, na mipira ya nkononi na bomba la chindano upeleke au wafwa. Ndo walikuwa wanayakataa madokta hayo wakakadiwa madongo na wabong wakishangilia oooh na manjinia na walimu na nini chijui? Chonga mbele kuyataka wenyewe! Ukiyavulia nguo maji yaoge tu.
   
 12. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kusema kwamba madoctor wanafanya hivyo kutokana na uzembe wa selikali, si sahihi. tunakubali kabisa kuwa huduma au vitendea kazi ni vichache sana, lakini mshahara wa doctors tz, ukilinganisha na mishahara ya watz wengine ni average tu. si mbaya si nzuri sana. wanatakiwa kuridhika nacho na napinga kwa nguvu zote kwamba wao tu ndo wapendelewe kuliko fani zingine, pamoja na kwamba mshahara wao hata hivyo ni mkubwa kuliko wa wengine.

  RUSHWA NI TABIA YA MTU BINAFSI ILIYOKO MOYONI MWAKE, hata wakipewa milioni tano kwa mwezi, rushwa watakula tu, maadamu wana roho zao mbaya, vifo vya wangojwa vitatokea tu. hii issue ilitokea sio leo, ni mwaka mmoja ulishapita hata kabla hawajaanza hiyo migomo ya mgogoro na serikali. hivyo usiingize kabisa hi issue na matatizo haya ya juzi...

  kwa wale walioishi muda kidogo, hakuna ambaye hajui kuwa, ukienda hospitali za serikali lazima utoe rushwa ndo utahudumiwa vizuri na manesi au doctor. UTU NI KITU CHA MUHIMU SANA, hata kama umegombana na mtu, usimalizie hasira zako kwa mwingine. kama wao wanaona hawalipwi vizuri, asingemsababishia yule mama matatizo ya maisha vile...na kumpotezea mtoto wake wakati yeye doctor watoto wake wanapumua na kufurahia home....imagine kama mamake doctor au dadake ndo angepata fistula kwa kukosa laki na nusu? hivi kuna asiyejua kuwa sector ya hospitali ndo yenye rushwa kuliko hata mahakamani na polisi?.....cha ajabu, watu wengine wanawatetea madoctor wa aina hii, wakirusha lawama kwa serikali na kuwasafisha madotor. subirini wake zenu na dada zetu wapate fistula, ndo mtajua kuwa hawa madoctor ni mahanithi au la. na ashukuru mungu huyo mwenye mme alikuwa mtu wa uswahilini, mtu mwingine unamfanyia mkewe hivyo, lazima akutoe roho...wasifikiri wao ndo wametushika sana sisi wananchi viganjani mwao kwasababu wanatuchoma sindani...
   
 13. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu nadhani hapo juu ndio ulipokosea..

  1. Kuna kitu kimoja wananchi tunapaswa tukitambue, Sera za Afya na Utekelezaji wake ni vitu tofauti kabisa...mfano mama mjamzito na watoto walio na umri wa xhini ya miaka mitano huduma za afya ni BURE..lakini je, ndivyo inavyofanyika?

  -Leo hii ukimwambia mama anunue pamba,aje na nguo(prefrbly khanga) au atoe pesa ili anunue duka jirani(pharmacy) lillilo karibu na hospitali anaona unataka kuchukua pesa yake...!! ni wimbo huo huo katika kuchangia damu, gloves nk.

  as i quoted above, hawa tunaowaambia hivyo(katika quote) ndio unategemea wao wenyewe hao hao wafanye hiyo kazi?..Usishangae naye akikutusi kwa kutofanya kazi!!

  Mkuu Ubungoubungo napata shida sana kuelewa mtu anapokwenda Benki kuweka/kutoa pesa halafu kukawa na shida ya Mtandao, halafu yeye(mteja) aanze kumlalamikia Bank teller au Accountant n.k!
  Above all awatukane hao B.tellers kwa shida hiyo.

  Tunaweza kuwa tuna complaints(actually Genuine complaints) lakini tukikosea channel sahihi ni kukosea kila kitu,mkuu.
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  yaani hata kuku anayegongwa kila siku na jogoo hawezi kuwa na akili ya uelewa kama ya kwako. sasa umeongea nini hapo? kuchangia huduma kwa hizi shilingi alfu tano etc kunalingana vipi na mama ambaye amepata uchungu na anaombwa laki moja na nusu.....hivi unaijua laki moja na nusu wewe kwa mtanzania wa uswahilini ilivyokubwa? hiyo kwake anaweza kulipa chumba karibia mwaka mzima....daktari hapokei mshahara? daktari ananunuaa yeye vifaa? hiyo laki moja na nusu alikuwa anataka ya nini? kama yeye anaona selikali haimlipi vizuri kwanini asiache kazi waje wale wanaopenda kutoa huduma ili wawahudumie wananchi...halafu amesoma kwa kodi ya huyohuyo anayeombwa laki moja na nusu.....unapoongelea ATM na sijui bank teller, hivi wewe ni doctor nini manake naona kama akili zanu ndo kama za watu wa aina hiyo....ndo maana mnapasua kichwa badala ya mguu. unataka sisi tuilalamikie serikali na si madoctor? is that what you mean? ni ilalamikie serikali kwasababu doctor anayepokea mshahara na malupulupu na nyumba ya kukaa ameomba rushwa laki moja na nusu halafu kwasababu mwanamke masikini yule hakuwa nayo amepoteza mtoto wake aliyekaa tumboni miesi 9 na kupata fistula ya mkojo na kinnyesi?.....nyie madoctor mbona mna roho mbaya kiasi hicho? mwogopeni hata Mungu basi na mjue mko hapo na nafasi zenu kwa neema ya Mungu, kuna wengi wanatamani iyo nafasi yenu hawaipati, zaidi ya yote mjue mmesoma kwa kodi za wananchi masikini rudisheni hata fadhila tu basi hata kama hamna utu. udoctor wenu una faida gani sasa kama mnaua wagonjwa waliowasomesha? natamani ningekuwa karibu na wewe uongee hivi ningekuzaba kibao na ungesahau hata kuiba madawa hapo ofisini ya kuyapeleka kule kwenye pharmacy yako. nyambafuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mabadiliko ya nchi hii yanatakiwa sana 2015.Achana na kofia, khanga, fulani, bootle opener, kalamu, etc. Hivi ni vitu na si maisha yako. Maisha yako mtanzania yapo mikononi mwako kwa kura 2015. Mwenye kutaka kuokoa nchi hii anza kampeni za nyumba kwa nyumba, jirani kwa jirani na kupitia simu pigia ndugu zako. You are a change, make it happen!! Just started!!
   
 16. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sawa sawa mkuu kwa matusi, kejeli na ujinga(kutokuwa na ufahamu) wa hali ya juu uliouonyesha kutatibu hiyo fistula.
   
 17. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Acha kutetea ujinga mkuu,hii tabia hawajaanza jana tu baada ya mgomo amekuwa nayo kwa muda mrefu tu na hata wakilipwa milioni 20 kwa mwezi hawawezi kuiacha tabia hii hawa watu!!
   
 18. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  watakaosoma comments zetu ndio watakaojaji nani ana ufahamu na nani alikimbia umande shule.
   
 19. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inauma sana, wenye hiyo clip tafadhali itupieni humu nasi tufanyie mambo.
   
 20. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naendelea kusisitiza mambo hayo yote mmeyataka wenyewe,kulalamika tu.
   
Loading...