Daktari Anapomfokea Waziri Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari Anapomfokea Waziri Mkuu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 16, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Hali kama hii inaweza ikatokea Uingereza lakini huenda ikawa ni vigumu sana kutokea Tanzania, Daktari mmoja wa nchini Uingereza aliliingilia tukio la waziri mkuu kupiga picha na mgonjwa hospitali kwa kuwa wapiga picha hawakufuata kanuni za kuzuia maambukizi ya maradhi hospitalini.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Daktari bingwa wa kufanya operesheni za viungo, David Nunn, alimuacha waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron na naibu wake, Nick Clegg, wakiwa mdomo wazi baada ya kuvamia tukio la waziri mkuu kupiga picha na mgonjwa na kuwafokea wapiga wake kwanini hawafuati kanuni za kuzuia maambukizi ya maradhi hospitalini.

  Tukio hilo lilitokea kwenye hospitali ya Guy’s hospital jijini London ambapo kanuni zilizowekwa zinamtaka mtu anayeingia kuwatembelea wagonjwa awe amevaa shati la mikono mifupi au akunje shati lake kuifanya mikono yake kuanzia kwenye kiwiko iwe wazi.

  "Kwanini wengine tunaambiwa tuvae kama hivi halafu hawa hawafuati kanuni?", alisema dokta Nunn kumuambia waziri mkuu na wapiga picha.

  Huku akipigwa butwaa kwa muda, waziri mkuu aliwaamuru wapiga picha na video watoke nje ya hospitali hiyo.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.


  <span id="lblFull" style="display: inline-block; width: 469px; ">[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...