Daktari aliyebaka nje kwa dhamana


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,977
Likes
5,350
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,977 5,350 280
DAKTARI wa Hospital ya Marie Stopes tawi la Mwenge jijini Dar es Salaam, Paul Andrew (34), anayekabiliwa na tuhuma za kumbaka mgonjwa, amefikishwa mahakamani na kuachiliwa kwa dhamana. Daktari huyo ambaye ni mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu shtaka hilo la ubakaji mbele ya Hakimu Suzan Kihawa.

Mwendesha Mashitaka Inspekta wa Polisi, Nassor Sisiwayah, alidai mbele ya Hakimu huyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 26, mwaka huu, majira ya saa 7:00 mchana eneo Mwenge katika hospitali ya Marie Stopes.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa akiwa ni daktari wa hospitali hiyo, alitumia nafasi hiyo kumbaka mlalamikaji, Judith Keleth (30) bila idhini yake wakati akijitayarisha kumfanyia kipimo cha uchunguzi wa mimba cha Ultra Sound.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti aliyopewa.

Hakimu alimtaka Dokta Paul awe na wadhamini wawili ambao kila mmoja anatakiwa kusaini hundi la shilingi 500,000 kila mmoja.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi 9 mwaka huu. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4020846&&Cat=1
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
30
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 30 135
Tumeshazoea kusikia neno "Daktari" lakini ukichunguza unakuta wala sio daktari ila medical assistant au RMA au hata mtu wa maabara. Historia inatukumbusha watu wengi wa aina hiyo, hata mwaganga wa mifugo walishaandikwa hivyo "Daktari apatwa na mfadhaiko kwenye daladala" ukisoma contents - mganga wa mifugo.

Pia tumezoea kusikia kwamba "Fulani amebaka" kumbe mdai wa kubakwa amepiga hesabu kumharibia mdaiwa kwa sababu hawajakubaliana mambo fulani fulani, anamshikisha adabu tu. Hata Yusufu wa kwenye misahafu alifanyiwa hivyo na nke wa Farao kwa sababu tu Yusufu amekataa kummega mkewe Farao. Hata Muhimbili miaka ya 1980 mwanzoni inern mmoja alichomekewa kumbaka kilema aliyejifungua masaa macache tu, kumbe ikaja kujulikana manesi amemchomekea kwa sababu jamaa alikuwa anakataa kuwamega manesi naye alikuw handsome sana. Japo aliumizwa sana kwa kutimuliwa kazi na kufungwa miaka miwili alikujatoka na kurudishiwa cheti alichofutiwa na baraza.

Sio jambo la kawaida saa saba mchana kubakana hospitalini ambapo pako bussy kama sio mabishano yaliwafikisha kusemeana mibako. Labda ni kweli, wapo wataalam ambao ni kama popobawa. Labda alikuwa hataki kuchunguzwa na jamaa huyo? Alipoguswa tu akadai kubakwa? Hiyo ultrasound si ni lazima mgonjwa aache tumbo wazi?

Mwanamke asipotumia jinsia yake kwa busara huwa mwiba mbaya kwa wanaume, maana kubakwa ni neno atakalolitumia kujipatia umaarufu hata kama hakuna kitu kama hicho kimetokea. Don't argue with a woman in private places, daktari awe macho kuwa na msaidizi wa jinsia tofauti kila wakati awapo kazini.
 
K

kisikichampingo

Senior Member
Joined
Oct 28, 2009
Messages
129
Likes
3
Points
35
K

kisikichampingo

Senior Member
Joined Oct 28, 2009
129 3 35
DOCTOR-a person who has been trained in medical science, whose job is to treat people who are ill or injured.

Kubinika, kwani medical assistant akiitwa daktari, wewe inakuuma nini?
 
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
DOCTOR-a person who has been trained in medical science, whose job is to treat people who are ill or injured.

Kubinika, kwani medical assistant akiitwa daktari, wewe inakuuma nini?
Medical assistant itakuwaje Aitwe Dotor? umeona wapi? hata huko Ulaya hakuna kitu kam hicho Mkuu kisikichampingo Mtu anaitwaDoctor kwa kisomo chake alichosoma sio ovyovyo tu .
 

Forum statistics

Threads 1,237,666
Members 475,675
Posts 29,296,673