Dakika Sifuri.

vivian

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,805
Reaction score
1,228
Hivi watanzania tumefikia Kutojali muda kiasi hiki?

What the hell is Dakika Sifuri.

Ndio maana ukienda sehemu mbali mbali kupata huduma, ukiuliza bado muda gani unaambiwa Bado Kidogo.

''nitakutumia sio Muda''
''nisubiri kidogo''
''nakuja''
''nitafanya kesho''- hapa hausemwi muda gani.

Watanzania tunahitaji Elimu ya Muda.
 
If I may ask. . . what the hell is dakika sifuri? Ni msemo mpya ama?
 
narudi ndani ya dakika sifuri.
 
Nasikia sana watangazaji hasa wa vipindi vya muziki wa bongo fleva wanatumia sana hili neno, dakika sifuri.
 
Hii slang itakuwa Masaki, bado haijafika Tandale Mansion.
 
POPOBAWA anapita, dakika 0 atarudi.
 
Sekunde sifuri nitarejea naenda kupost barua kubwa.
 
Ni kweli tunahitaji elimu ya muda,hata kwenye mambo ya msingi sana wengi wetu hatuheshimu muda....!
 
ni sawa na 'in five....'?

Be back in five!
 
Ukiwa unamsubiri mtu ndio inakuwa kero zaidi.
Mtu yupo magomeni mataa unamsubiri k/koo anakwambia nipo fire hapa nipe dakika 0 nakuja, unaweza kununua ugomvi na kumtia mtu makofi kwenye daladala lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…