Dai la mafao NSSF, tumshauri mwenzetu

Mr_Uronu

Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
33
Reaction score
24
Kama Nilikuwa member wa NSSF baadaye nikawa member wa PSSSF, nawezaje kupata mafao yangu ya NSSF hali ya kuwa nimeshaondoka huko na pesa yangu haiongezeki Wala Haina faida nami.?

Kama nikitaka kuiwekeza pesa yangu kwenye mifuko ya thaman Kama vile UTT-AMIS kwa maendeleo ya wategemezi wangu kwa mpango wa baadaye inawezekanaje.?

Naombeni msaada kwenye hili.
 
Unapotuma maombi ya kutaka fedha zako za NSSF mfumo hautakiwi kusoma kuwa upo kwenye ajira ambayo muajiri wako anakupelekea fedha zako NSSF, kama ulitaka fedha zako baada ya kupata ajira mpya ulitakiwa uhakikishe muajiri wako mpya anazuia kwanza kupeleka michango yako NSSF mpaka lile ombi lako linapomaliza kushughulikiwa na pesa zako kutoka. Kwa sasa hakuna namna namna utaweza kupata tena hizo pesa labda michango isiende NSSF na ukae hiyo miezi mitatu tena kisha utume maombi upya
 
Mpe pole sana jamaa yako, kwa sasa hakuna kinachoweza kufanyika yeye kupata hiyo hela ya NSSF. Kilichotokea hapo mwajiri wake mpya (serikali) alipopeleka tu michango yake PSSSF, mifumo ikasomana na jamaa akaonekana kuwa tayari ana ajira, hivyo hayuko tena elligible kulipwa fao la kutokua na ajira. Njia pekee hapo ni yeye kufukuzwa kazi na mwajiri wake wa sasa, otherwise hiyo ni mission impossible!
 

kweli kaka lakini kwa sasa yupo serikalini na anahudumiwa chini ya mfuko wa PSSSF..

NSSF for private sector
PSSSF for Government sector
 
yeah sure, ahsante
 
Samahani, hivi inachukua muda gani mtu kupata pesa zake tangu siku amethibitisha kwa kuweka finger print ?
 
Wakuu, mm nina balance flan NSSF na nina mwaka sasa sina ajira. Mwajirwa wangu mim ndio nilivunja mkatabaa. Nimekaa baada ya mkataba kuisha (ingawa sikuwa tena kazin) nilirudi kumuomba anipe barua ya end of contract au terminatio lakin hanipi ushirikiano.


Anayeweza kunisaidi/kuniunganisha nipate pesa yangu naomba tuongee DM.

10% nitakupa
 
Kama document zako zimenyooka ni ndani ya wiki 1 hadi 2 tu. Wakifanya uzembe uzembe inaweza fika wiki 4; ila si zaidi ya hapo, ikizidi hapo ujue kuna shida mahali.
Uzembe tayari umefanyika, tarehe 05/10 ilitimia wiki 4 tangu alama ya vidole iwekwe.

Je ni hatua gani inaweza kuchukuliwa ili malipo yafanyike kwa haraka zaidi ya kuambiwa na kujibiwa "DAI LAKO LINAFANYIWA KAZI SUBIRI UTALIPWA TU KWANI UNA HARAKA GANI AISEE?"

Ukiangalia kwenye portal bado ipo kwenye ile stage ya "CLAIM PROCESSING" kwa zaidi ya wiki nne sasa.

wtf!
 
Aombe NSSF wapeleke michango yake PSSSF..Na kwa kuwa yupo PSSSF ambao ni mfuko chini ya GOVT maana yake yeye ni mwajiriwa wa kudumu..Akae kwa kutulia mpaka muda wa kustahafu
 
Aombe NSSF wapeleke michango yake PSSSF..Na kwa kuwa yupo PSSSF ambao ni mfuko chini ya GOVT maana yake yeye ni mwajiriwa wa kudumu..Akae kwa kutulia mpaka muda wa kustahafu
Umejibu post gani ?
 
Mwanza wametuweka toka jumatatu then wakaja kutupa laki 2 na nusu za usumbufu hapa lini MCHUZI tutegemee?
 
Hapo kwa utaratibu wao ni hadi ufikishe miaka 60, hutakiwi kusomeka uko PSSF ili NSSF wakulipe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…