Dah, kweli tunatofautiana....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dah, kweli tunatofautiana.......

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TANMO, Feb 4, 2011.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kweli wanaume tunatofautiana, unakuta eti Mwanaume anampigia simu demu anapiga naye story kwa masaa manne hadi sita. Story zinazopigwa ni kuhusu Birthday, mahusiano, nguo za rangi gani zinavutia, sherehe gani unapendelea na kuhusu familia zenu mara Baba yangu ni mkali mara mama yangu hapendi kutazama Tv!!!

  Au mimi ndiyo nina matatizo kwa sababu siwezi kuongea na demu kwenye simu zaidi ya nusu saa unless tunongelea mambo yanayoeleweka, mara nyingi huwa naona bora kumpigia msela mwenzangu na tukazungumza hata kwa masaa mawili bila kuboreka kwa sababu ni mengi ya kuongelea na wakati huo huo kujifunza, kwa mfano:

  1. Siasa 2. wanawake 3. Manchester United 4. Wanawake 5. Chelsea 6. Wanawake 7. Kompyuta na elektroniki 8. Wanawake 9. Arsenal 10. Wanawake
  11. Biashara 12. Wanawake 13. Bundersliga 14. Wanawake 15. Muziki 16. Wanawake
  17. Magari 18. Wanawake............... 19. Masomo …………… na bado tukaahirisha mazungumzo kwa sababu ya muda au majukumu mengine.

  Inaweza kutokea mtu unashindwa kulala eti kisa jirani yako anapiga stori na "rafiki yake" (mwanamke) tangu usiku mpaka asubuhi, ukimwambia amtongoze huyo demu basi kieleweke, anadai dini haimruhusu kutenda dhambi. Baada ya muda demu anapata Bwana, unaona njemba inanyong'nyea eti ita-miss mtu wa kupiga naye story. My foot!!!!!!

  Kwenye hili suala kuna mtu lazima ana matatizo, aidha mimi au mtu wa aina hii….
   
 2. LD

  LD JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sijui sijakuelewa vizuri, ni unadharau hao unaowaita mademu kwamba hawana story za maana au??????
  Halafu mtu akiwa anapiga story na huyo demu haitoshi mpaka amefanya uzinzi au??

  Daaaaa ngoja niache, manake sio lazima kuchangia kila thread, nitasoma maoni ya wengine. Kwa heri.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Sijamdharau mtu bibie..
  Ila tafakari vizuri utanielewa tu....
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Juzi mimi na wewe tuliongea masaa sita kwenye simu unakumbuka hadi nikachelewa kulala nikalala saa 9 usiku
   
 5. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ila inategemea kwa muda huo mnaongea nini kuna siku inabidi uongee kwa kirefu sana labda unamwelewesha kitu mwenzio na kuna siku hamna cha maana so ikizidi nusu saa si itakuwa kero?
   
 6. LD

  LD JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si ndio hapo halafu mi ndo zangu yani, nikikuta online hata sa saba tunakesha tu halafu ukinitongoza mi nakugonga huko huko kwene bluetooth.
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bila samahani babue...
  Hata mi naona sijaelewa, naomba nisitafakari
  Nitasoma tu mchango wa wengine.
   
 8. P

  Pokola JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  ... napita, naelekea kwenye mgomo UDSM nitarudi badae kidogo ...:laugh:
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mkuu hiyo kweli kabisa, mwindaji ni mwindaji tuu ukiona mtu anazunguka zunguka ujue domo zege anashindwa kuwa mwanaume halisi. mie nashindwa kumzoea mwanamke kinafiki yaani mpaka niombe kwanza akinitosa ndo anakuwa rafiki yangu tunaweza kuongea lkn eti urafiki wa kaka na dada wapi na wapi
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hao mademu unaowaongelea ni wapi haswa?Unaowajua wewe au wote in general?Maana nnavyojijua mimi japo si DEMU hua napiga hizo story za maana unazodai ni washkaji tu ndo unaweza kuongea nao!Na hatujawahi kuongelea sijui rangi za nguo na mengine uliyotaja hapo juu..tho nawajua watu wa hivyo!Nwyz punguza dharau..kwanza utajuaje kama hao washkaji wenyewe ndo hawataki kudiscuss mambo ya maana..waanzishe hayo mazungumzo alafu yakipotezewa ndo uongee..tena kwa kusema baadhi na sio kwa mkusanyiko!
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wewe mwanamke sasa unataka kuiniaibisha hapa, haya mambo ya KUGONGA unajua sio mazuri presha yaweza shuka, halafu kuna ishu inabidi tuzungumze nadhani Teamo atakuwa amekupa hint kama bado nitakushtua nikwambie
   
 12. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #12
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mama mchungaji nimepata mchumba nitamleta kwako kwa ajili ya counseling
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Nakubliana na unachokisema....
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehe sio unamleta bwana ila unajileta na wewe.. au we ndo huitaji?Embu nitambulishe fasta nifanye tathmini!
   
 15. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mkuu hilo ndo nalimaanisha hapa, siyo kuleta story kibao ambazo hazina kichwa wala miguu,,, halafu demu akichukuliwa na njemba nyingine mtu anaanza kunung'unika hovyo.
   
 16. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Okay tena unamjua vizuri ila usishangae nikikutajia jina lake
   
 17. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hapo penye nyekundu, nashukuru kwa kuniunga mkono...
  Penye Bold nashukuru kwa ushauri,
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tabia za watu kwenye jamii zinatofautiana wewe ukifanya hivi mwenzako anafanya vile kwahiyo hauwezi kulazimisha, mimi nina postpaid hayo masaa sita unayosema kwangu mimi ni madogo sana i can even talk for seven hours na maongezi yanakuwa ni ya aina tofauti so all in all we differ on what we do and i am used to it kwahiyo kuongea nusu saa huwa siwezi kabisa muda wa chini wa kuongea ni masaa manne au matano
   
 19. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Out of topic Great thinker...
  Ndo maana mkuu Invizibo aliweka opsheni ya kutuma PM...
  Au kama vipi anzisha thread yako, usiharibu vilivyoanzishwa na wenzako....
   
 20. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Ok, vizuri..
  Angalau umechangia mada...
  Nashukuru kwa mtazamo wako...
   
Loading...