Daftari la wapiga kura kizungumkuti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daftari la wapiga kura kizungumkuti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Oct 31, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Imekuwa sasa ni kawaida Watanzania kulalamika lakini kwa hili la daftari la kupigia kura serikali ina jidanganya na kama si kujidanganya basi inajikaanga yenyewe kwa mafuta yake.Daftari hili ni bora lisitumike inapotokea uchaguzi,utafutwe utaratibu mpya wa kuwaorodhesha wapiga kura kuliko kiini macho kinachofanywa kwa makusudi ilihali kuna uchakachuaji mkubwa wa majina.

  Nitatoa mfano mdogo wa malalamiko yangu kuhusiana na daftari hili katika uchaguzi uliopita wa madiwani katika kata mmoja ya Mwawaza.Takwimu za wapiga kura zinaonyesha wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 3089,waliopiga kura 1,303 wasiopiga kura 1,786.kwa mantiki hiyo basi waliopiga kura ni asilimia 42.18%,wasio piga kura asilimia 57.82%.

  Hatari iliyoko hapa ni kuchaguliwa viongozi ambao si chaguo la wengi.Hatuwezi kuliachia suala hili likapita hivi hivi bil kulisemea.Kuna haja ya kuachana na daftari hili ambalo hakuna siku limewahi kutoa angalau takwimu zikaonyesha zikafikia robo tatu ya wapiga kura walioandikishwa.Hali hii ndo maana imekuwa ikipigiwa upatu wa ushindi wa simple majority.

  Ukitazama matokeo ya uchaguzi huu ninao uzungumzia utaona matokeo kama ifuatavyo,mgombea wa CCM amepata kura 791 akifuatiwa na mgombea toka CHADEMA aliyepata kura 599 na wa TADEA kura 1.Kimahesabu kutokana na wapiga kura walioandikishwa utaona kuwa mgombea wa CCM amepata kura asilimia 25.61%,wa CHADEMA kura asilimia 19.39% na mgombea wa TADEA asilimia 0.03%.Kwa asilimia hizo hapa kweli katika nchi inayojinasibu inafuata utawala bora na kudumisha demokrasia ya vyama vingi utasema ni sawa?

  Inatulazimu kupiga kelele kwa nguvu zote kuhakikisha dhuluma hii ya makusudi dhidi ya wananchi inafutiliwa mbali vinginevyo tuitangazie dunia kuwa mfumo wa siasa wa vyama vingi hatuukubali ili dunia nzima ituelewe kuliko uhuni unaofanywa kwa makusudi ilihali daftari hili lilitumia pesa nyingi sana za walipa kodi wa nchi yetu.

  Hatari ya kuwa na viongozi wasio chaguliwa na wengi ni kuwaburuza wananchi na kuamua kujilimbikizia mali kwa utashi na dhamira ya mioyo yao.Nawaombeni wadau na wazalendo wa nchi hii ndani JF kuliangalia kwa umakini suala hili na kila mmoja achangie nini cha kufanya kunusuru uhuni huu unaofanyika.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tume ya uchaguzi iluhusu vitambulisho vya taifa navyo vitumike.
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Pamoja na vitambulisho vya utaifa kutumika tunabidi serikali iwe mkweli kwa wapiga kura wake.Yamekuwepo matukio mengi ya uvunjivu wa amani kama kununua vipalata ya kupigia kura na kuwarubuni wapiga kura kwa vijisenti kutokana na ugumu wa maisha na kudhulumu haki yao ya kupiga kura ikiambatana na vujo za makusudi zinazofanywa na wafuasi wa vyama vya siasa kwa utashi wao tu kwa kuwa nio wenye dola na hakuna hatua zinazo chukuliwa.
   
 4. A

  Ame JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Dawa ni kwa viongozi wa upinzani kuingiza (shinikiza) sheria ya kupiga kura ni lazima (wajibu kwa raia) asiyefanya hivyo ashitakiwe ili mahakama iamue kama alikuwa na sababu za msingi za kutokupiga kura..Nchi ninayoishi hii sheria ipo nadhani hii itapunguza hii tabia ya watu kuuza shahada zao na pia ita weka wazi hiyo magic ya wenzetu waliyoi-ivumbua kwa gafla mno 2010 ambao watu wengi hawakupiga kura...
   
 5. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Kitu kingine ni kuivunja TAKUKURU,mambo yote haya yanafanyika wana shuhudia ukuiliza wanasema wenye nchi wameamua sisi mbavu zetu ndogo kazi yetu ni kutekeleza kile tunacho amriwa na wakubwa.Polisi nao ni mashuhuda wakubwa wa matukio haya lakini hakuna hatua yeyote.
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tukiweza kulipinga daftari hili hakika tutashinda vita vya uchakachuaji wa matokeo pia tukiweka sheria na kuiachia mahakama isimamie bila kuingiliwa hakuna atayecheza na akili za mwenzake
   
Loading...