mwendo wa kibongo tu ukiona kinachokuvutia na wewe unaiga unagonga kopi na kupiga seli tena kwa kuwa hukuhangaika kutunga chochote unafaidika kuliko muhusikasamahani una copyright kutoka kwa M.M. Mwanakijiji au ndo kibongo bongo..BASATA muu wapi?...
Vidole vinaniuma, kalamu naiachia,
Nililotaka kusema, hilo nimewaambia,
Hivyo kutama natama, miye nawabarikia,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!
Dada zetu mwatutega, twategwa tukategeka,
Mikogo mnayomwaga, twajikwaa twaanguka,
Na nyuma mkigeuka, toba! Tunanusurika,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.
Dada zetu twawapenda, Bila ninyi tunakonda,
Kila siku zikienda, twajuta tunayotenda,
Msiache kutupenda, twapenda mnavyopenda,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!
Wengine mwavumilia, na miaka inapita,
Watoto kutukuzia, kumbe mioyo yajuta,
Na siku ikifikia, na ninyi mbele mwapeta,
Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!
Mwanakijiji Hongera kwa shairi zuri umenikumbusha vituko vya Mwanameka!!
tatizo la mwanamke siyo kupenda ila kukuheshimu....................ndiyo shughuli.......................kwetu kupenda ndiyo kazi kubwa kweli........tuasemayo mara nyingi wala hayapo moyoni...............................we are born liars..........so gals watchout when I tell you I love you very much........in fact I mean that I want to ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,you very much..................................[/QUOTE]
kheee yamekuwa hayo tena, asante kwa taarifa RUTA
Mwanakijiji nashindwa hata kuku-define. Umeshehena utaalam wa kila aina. Inawezekana hata naniii ni mtaalam vilevile nini??