Dada zetu Mna Mambo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dada zetu Mna Mambo!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 26, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,208
  Trophy Points: 280
  Msema kweli hakika, huyo mpenzi wa Mungu,
  Kalamu nimeishika, nilisemalo ni langu
  Beti ninaziandika, mzisome dadazangu,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

  Dada zetu mwatutega, twategwa tukategeka,
  Mikogo mnayomwaga, twajikwaa twaanguka,
  Na nyuma mkigeuka, toba! Tunanusurika,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

  Mkilegeza sauti, wagumu wanayeyuka,
  Mtu mzima na suti, kiwewe kinamshika,
  Chini akija kuketi, miguu yatetemeka,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo.

  Hasa mnaponong’ona, mwatupandisha presha,
  Tunabakia kuguna, na milio ya kutisha,
  Na tukiwa tumenuna, wadada mwatuchekesha,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Nguo zinavyowabana, mwatusukuma dhambini,
  Twamuomba Maulana, tutoke majaribuni,
  Wa dada mna hiana, mwajua mwafanya nini,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Mara mnatukonyeza, mwapiga jicho kwa vile,
  Twabaki twajiuliza, ana nini dada yule,
  Tukija twajibamiza, twalishwa chenga za Pele,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Mwajua kutuchombeza, kama samaki na chambo,
  Magoma tukiyacheza, kama ndege na ulimbo,
  Wenzenu mwatumaliza, mkitingisha majambo,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Mwajua kututuliza, mwauma na kupuliza,
  Tena mnatuliwaza, twalala twapitiliza,
  Kweli mnatushangaza, twabaki twajiuliza
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Mengi tunawakosea, machozi tunawaliza,
  Matusi twawatolea, na maneno ya kubeza,
  Mengi tunawatendea, twatenda bila kuwaza,
  Dada zetu mna mambo mambo yenye vijimambo!!

  Mwisho mnakimbilia, kwa mwingine kutulia,
  Mapenzi kutafutia, vidumu mwajipatia,
  Mioyo ikitulia, kimoja mnazamia,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Wengine mwavumilia, na miaka inapita,
  Watoto kutukuzia, kumbe mioyo yajuta,
  Na siku ikifikia, na ninyi mbele mwapeta,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Ukweli nawaambia, bila nyinyi tumekwisha!
  Tunakaa twajutia, na mawazo tunakesha,
  Ulabu twafakamia, machungu kuyaondosha,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Dada zetu twawapenda, Bila ninyi tunakonda,
  Kila siku zikienda, twajuta tunayotenda,
  Msiache kutupenda, twapenda mnavyopenda,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Vidole vinaniuma, kalamu naiachia,
  Nililotaka kusema, hilo nimewaambia,
  Hivyo kutama natama, miye nawabarikia,
  Dada zetu mna mambo, mambo yenye vijimambo!

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  kweli ni nimekukubali MMM umshairi mzuri
  kweli kaka yetu una mambo, mambo yenye vijimambo.
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji una mambo yenye vijimambo
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 10,995
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MMM! Upo juu! Anzisha bendi kwn baadhi ya WanaJF 2takuunga mkono.
   
 5. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni siku nyingi hujakumbuka jukwaa letu hili. Nitarudi
   
 6. F

  FredKavishe Verified User

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I salute u mwanakijiji
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,534
  Likes Received: 21,016
  Trophy Points: 280
  Jamani ile button ya thanx irudishwe haraka mno.......
  Duh....
   
 8. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,339
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hakika hiki ni kilio cha mtu mzima....................................
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Tusingekua na mambo na vijimambo msingefurahia maisha.

  ASANTE MMKJJ.
   
 10. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,632
  Likes Received: 2,527
  Trophy Points: 280
  Hongeraaaaa!!
   
 11. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,285
  Trophy Points: 280
  Yani mwanakijiji hakika ww ni multipurpose, huwa nashndwa hata kukutengenezea taswira how do u look? Hebu tupia picha yako basi mkuu.
   
 12. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  HALOOOOOOOOOOOOOOOOO mwana KIJIJI ONCE MORE!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hongera MKJJ kwa shairi nzuri.... uko juu kila eneo....................
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,092
  Likes Received: 2,969
  Trophy Points: 280
  Man weakness but not all of us!!Man still man til da end!!
   
 15. Kadada

  Kadada Senior Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 137
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 60
  Ahsante sana Mwanakijiji hapo kweli umetupatia dada zako, Big up
   
 16. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli uloyasema,wala hujadanganya kitu,wafanya waume kuhema,kama miti kwenye misitu,wanajua kutetemesha,wakuache hauna kitu,kweli wadada wana mambo,makubwa kuliko mfano
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwafanya makusudi enhe! Aksante mwankijiji!
   
 18. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
   
 19. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,786
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  hapo kwenye nguo za kubana tu hapo. Siku hizi unaona Mdada anatembea utafikiri yupo uchi lakini kapakwa Rangi nyeusi. kumbe kapiga mavazi meusi ya kubana
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,221
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Alafu we Mkirua mpaka kuandika unaandika kwa Kirua?!Embu hapo kwenye MwanKijiji ongezea A!!

  Hahahh hatufanyi makusudi wala nini!
   
Loading...