VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Dada yangu na kada mwenzangu mwandamizi wa zamani wa CCM, Sophia Simba unapaswa kufanya uamuzi. Uamuzi wa kuchagua moja: kuomba msamaha na kurejea CCM au kuhamia chama kingine au kubaki kimya bila chama.
Nimesikia na kusoma mahali kuwa umesema utakuwa mkereketwa mwaminifu wa CCM. Ukereketwa ni nini? Unabakije kuwa mkereketwa wa chama kilichokufukuza uanachama kwa kukisaliti (kuonesha kukosoa maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu)? Msaliti anabaki vipi?
Dada Sophia Simba, nakujua na naijua historia yako ya kichama. Nakujua tangu enzi zile ulipokuwa Katibu Muktasi (Secretary) huko Dar es Salaam. Najua jinsi ulivyojijenga taratibu hadi kufika ulipofukuziwa. Najua kuwa UWT umeitangaza na kuiimarisha. Hupaswi kubaki bila kuamua.
Ninazo taarifa kuwa Balozi Emmanuel Nchimbi atasema neno hivi karibuni. Kwa misimamo yake, hulka yake na 'ungoni' wake, Nchimbi ataweka wazi msimamo wake juu ya kubaki au kutoka CCM. Hawezi kubaki vuguvugu kama wewe. Najua umeumia kuona unafukuzwa na kiongozi wako Nchimbi akipewa onyo kali.
Dada Sophia Simba, ni ima uombe msamaha na usubiri miaka miwili kurejeshwa chamani-CCM au uamue kujiunga na wengine au ukae kimya bila 'ukereketwa' wowote. Kwa level uliyofikia ndani ya CCM (kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu), hupaswi kubaki huelewekieleweki.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)