Dada yangu fanya haya kwa mume wako

Dada yangu fanya haya kwa mume wako

Ushauri mzuriii kabisa.
Wanaozingatia haya yote, ndoa zao Ni zenye Furaha kabisa. Ila sasa hayo huwa nayaona kwenye Maigizo tu.
Nikimpata mdada wa hivo leo leo natangaza nia ya kuoa.
 
Vichwa vya panzi hawa wanamke umewawekea vitu ving mno hawawez Ku kalili
 
Ahsante kwa kuyaeleza vizur ila sidhan kama kizazi hichi kinayaweza hayo yote
 
Kaka sijui/sidhani kama kuna mwanamke wa sasa anaweza haya.
Ningempata mwanamke wahivi hata mali nisingehitaji maana yeye angekuwa zaidi ya chochote, ningemjali kila dakika, ningempa kila kilicho ndani ya uwezo wangu, ningemthamini ningemjali ningemheshimu na kumlinda kama nafsi yangu.
 
HAA
Hahaaaaaaaa angefafanua kwa wanaume wa mbinguni tu sio duniani[/QUO

kinachoboa daily ni threads za wanawake tu,yaan zoteee zinahimiz kumsujudia tu mwanamume kha msituchoshe jaman wanaume wenyewenhawana jema hawa pyee
 
Ushauri mzuriii kabisa.
Wanaozingatia haya yote, ndoa zao Ni zenye Furaha kabisa. Ila sasa hayo huwa nayaona kwenye Maigizo tu.
Nikimpata mdada wa hivo leo leo natangaza nia ya kuoa.


easy sn haayo lakin mm napishan na hapo kunyekekea nyenyekea daily hapo mimi hapana ila nami ni mmoja wao wenye ndoa nzuri tena naipendaa tu sijawah juta ila sikunyenyekei aic na sijui
 
Hakuna wa dizaini hii kwenye kizazi hiki cha kobra
 
.
1. Muite kwa jina lake la utani
2. Muache atumie mamlaka yake kama kichwa cha nyumba.
3. Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani.
4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira. Unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumueleza kwanini ulimkosea pale hasira zinapokua zimemuisha.
5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.
6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya hivyo.
7. Waheshimu wazazi wake.
8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia.
9. Msuprise kwa chakula akipendacho, hasa kipindi kile anapokuwa na msongo wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.
10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie chakula mume wako ukiwa nyumbani.
11. Mkaribishe kwa kumkumbatia anapotoka kwenye mihangaiko yake. Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.
12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka wote kwenda kwenye warsha mbalimbali.
13. Mpigie simu na umwambie kwamba unampenda na umemkumbuka
14. Muamshe asubuhi na umpe romance kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe na hata jishughulisha na wanawake wengine siku hiyo.
15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
16. Mwambie ni kiasi gani una bahati kuwa nae kama mume wako.
17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.
18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu wako katika maisha yako.
19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu.
20. Tengenezeni utaratibu wa familia nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja kila asubuhi na usiku kabla ya kulala.
Mungu abariki ndoa yako. Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya kweli leo na daima.
Na wasio serious na mahusiano wanaokupotezea muda wako wajikatae kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya kutimiza kusudi la Mungu kwako.
Umeolewa???
 
Wapo lkn wachache, walau 80% yakitimizwa basi ndoa zitaimarika sana
 
Yaani unataka mwenzako awe malaika wkt wewe ni shetani, thubutu yetu shetani kwa shetani malaika kwa malaika mwenzske.
 
Back
Top Bottom