Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

Dada yake MBOWE aikacha CHADEMA ajiunga na CCM!!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Wakati Mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CHADEMA na hatimae kujiunga na CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)

DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.
Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai Chadema wanafanya propaganda za kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka Chadema, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

"Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya Chadema na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,"alisema Mbowe.

Alisema, "kuwapo kwangu Chadema siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia."

"Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia Chadema, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi," alisema.

Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya Chadema, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali Chadema ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea.

Chanzo: HABARI LEO
 
Dada yake Mbowe kajitambua, ameona haiwezekani akili ndogo iongoze akili kubwa.

Hongera sana Grace Mbowe.

Kama nyumbani wanamkataa Mbowe, kulikoni.
 
Amejitambua kuwa yeye hawezikuwa msukule.

Inawezekana Mbowe alitaka ampeleke kwenye vurugu akaona upuuzi.

soon vijana wengi watajitambua pia
 
Nini sasa? So umeona news ndio hiyo tu gazeti zima!!

Nilichoandika Kamanda ni kile kilichoandikwa na Gazeti. Lakini pia hii ni sawa na kusikia kuwa MBWA kamngata mtu na ukasikia MTU kamngata mbwa je hapo habari ni ipi?
Siku zote tumezoa kusikia au kuona mbwa akimngata mtu, lakini siku ukisikia au ukiona mtu kamngata Mbwa, lazima utashangaa sana!!
Kwa hiyo km habari hii iliyoandikwa na gazeti hili la Uhuru kongwe la Chama chama Pinduzi ni ya kweli basi lazima ionekane ndio habari kuu ktk gazeti hilo.

Ila binafsi siamini hili gazeti la uhuru kwani lipo kichama na kipropaganda zaidi. Ngoja tusubiri tutajua ukweli muda sio mrefu!!
 
Kimsingi Chadema ni chama cha kifamilia hilo lipo wazi wala haliitaji PhD kulitambua.

Mmiliki wa Chadema ni Mtei, na Mwenyikiti wa Chadema ni Mbowe, ambaye ni mkwe wa Mtei,

Kuna uwezekano mkubwa wa kimaslahi ndani ya familia ndiyo maana Grace Mbowe, kuamua kuondoka Chadema na kwenda CCM.

Tutasikia mengi pindi Grace Mbowe, atakapofunguka zaidi.
 
Kimsingi Chadema ni chama cha kifamilia hilo lipo wazi wala haliitaji PhD kulitambua.

Mmiliki wa Chadema ni Mtei, na Mwenyikiti wa Chadema ni Mbowe, ambaye ni mkwe wa Mtei,

Kuna uwezekano mkubwa wa kimaslahi ndani ya familia ndiyo maana Grace Mbowe, kuamua kuondoka Chadema na kwenda CCM.

Tutasikia mengi pindi Grace Mbowe, atakapofunguka zaidi.
Umeulizwa mbona kwenye ishu zinazohusu unga mbona huwa unalala mbele? Mbona kwa kamanda Esta wasira hukushangaa? Au akinya kuku.......,..!!
 
Jamani mbona ni haki yake kikatiba? MMesahau Makongoro aliwahi kuwa upinzani wakati Mwl. Nyerere (Baba mzazi akiwa CCM), tunalikuza saana hili jambo, ila inaleta picha kuwa kweli CCM mnaigopa CHADEMA. Hivi mnataka kutuaminisha kuwa ukoo woote wa Dr. Slaa wako CHADEMA? au ukoo wa Mh. Nyerere wote wako CCM? suala la kuingia chama chochote ni utashi wa mtu, hivyo Grace ameamua tumtakie mema huko alikoenda
 
Wakati Mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CDM na hatimae kujiunga na CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)

Kutakuwa kuna fungu la mgao kapigwa panga xaxa kaona "inatosha" kama vipi bora awe gamba tu.
 
Huyo Mama ni Mfano wa Kuigwa na Wanawakle wengine wa Tanzania wanaodanganywa kwenda kwenye maandamano waache majukumu ya kujenga uchumi wa Familia. Chadema wanadharau sana wanapojenga hoja.
 
Wakati Mwenyekiti wa taifa CHADEMA mh Freeman Mbowe na baadhi ya Wabunge wakihojiwa na jeshi la polisi mkoani Iringa kwa kile kinachodaiwa na jeshi hilo ni kupitiliza muda wa kuhutubia ktk mkutano uliofanyika siku ya jumamosi, Dada yake na Mbowe GRESI MBOWE,ameamua kuikacha CDM na hatimae kujiunga na CCM!!

SOURCE; Gazeti la Uhuru (Radio Free Afrika)

CHADEMA sio mali ya mtu,ni mali ya wa Tanganyika na wa Zanzibar,ajabu ipo wapi kama kaamua kuondoka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom