Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,839
- 10,070
Nafahamu fika naingilia makubariano ya watu, ila kwa jambo kama hili si sawa!
Anapika chakula, anafua nguo za watoto, baba na mama mwenye nyumba, kila siku kibarazani kunyoosha hizo nguo, usafi kuzunguka nyumba, kuteka maji maili mia zaidi ya ndoo kumi na tano kwa siku (na huo mpando), kuwapeleka na kuwafuata watoto shuleni, bado kuhudumia mkuyenge wa mdogo wake mama mwenye nyumba! Na mikazi mingine kibao!
Alfajiri ninapoamka asubuhi na mapema namkuta nje, usiku kwenye saa sita ndo muda wake wa kulala (alivyonieleza)
Bado mke wa boss amsurubishe kwa mabao, mangumi na mateke pindi atokapo kazini na hasira zake especially akute wanae hawajaoga! Au kitoto kimchongee mdomo kwa mama yake! Mchana kutwa, jua kali anaelekea sokoni kuemea!
Alivyonisimulia haya yote nimejikuta namwaga chozi!
Yote tisa:
Mshahara 30,000 kwa mwezi! Halafu 10,000 ni makato kwenda kwa dada yake aliyemtafutia kazi! Halafu ni ndugu wa damu eti!
Mtakufa kifo kibaya ninyi wahusika!
Nashindwa niwachukulie hatua gani!
Na ngoja nipate mahali sahihi pa kumpeleka akapata kazi ya maana, Nitamtorosha!