Dada "poa" wa Buguruni Malapa. Kuna sheria dhidi ya ukahaba!?

Ipyanah

Member
Jul 15, 2009
98
37
katika wiki mbili zilizopita, kulikuwa na tafrani kidogo kati ya wale dada poa wanaoishi maeneo ya Buguruni Malapa, na uongozi wa msikiti wa jirani. Malalamiko ya wale dada ni kuwa, kuna kundi la vijana wana wapiga "wageni/wateja" wao, pale wanapo toka kwenda kuwaona kwenye vyumba vyao, vijana hao inasemekana wametumwa na uongozi wa msikiti.

Swali langu ni nani alaumiwe katika fujo zile, wale wakina dada for their "quality" services mpaka sehemu ile, inafamika kwa vitendo vyao na sehemu zingine nchini... au serikali kwa kutopambana vya kutosha na matendo ya ukahaba mpaka wananchi wanajichukulia sheria mkononi??
Na je kuna sheria yoyote dhidi ya ukahaba??
 
Unaweza ukakuta hata wewe unalaumiwa kwa kutolipa kodi kuiwezesha serikali yetu kuweza kutoa huduma kwa jamii.issue iko deep. Nawashauri viongozi wa msikiti wapeleke issue police badala ya hivyo walivyofanya ( kama ni kweli).
 
Unaweza ukakuta hata wewe unalaumiwa kwa kutolipa kodi kuiwezesha serikali yetu kuweza kutoa huduma kwa jamii.issue iko deep. Nawashauri viongozi wa msikiti wapeleke issue police badala ya hivyo walivyofanya ( kama ni kweli).

Ila niliwahi kufuatilia kidogo hii ishu nikaambiwa eti baada ya kuona hawa makahaba wanasambaza condoms mpaka karibu na msikiti..viongozi wa msikiti ule walienda police na kupewa RB ya kumkamata yeyote atakayeonekana kushiriki ktk hiyo biashara...Nadhani uliyoona ni harakati ya kuwakamata.
 
Back
Top Bottom