Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,259
Tukiacha malalamiko ya huyu dada nadhani Wizara yetu ya Afya inatakiwa ifanyiwe marekebisho makubwa sana.
Kwanza kuna kukomoana kati ya madaktari waliosoma Tanzania na wale waliosoma Ulaya ya Mashariki. Miaka ya nyuma viongozi wengi wizara ya Afya walikuwa madaktari wasaidizi au clinical officers. Hawa watu walipotaka kujiendeleza hawakupata nafasi za kusomea udaktari kwenye chuo pekee cha udaktari Tanzania kwa enzi hizo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, tawi la Muhimbili. UDSM ilikuwa strict sana katika admission hivyo hawa watu hawakuthubutu kabisa kwenda kuomba kuingia Muhimbili hivyo wakapata nafasi za kwenda kusoma kwenye vyuo vidogo vya Ulaya ya Mashariki na Cuba. Wengi waliporudi wakaja kuchukua nafasi nyeti wizara ya Afya na kujenga chuki dhidi ya graduates wa vyuo local au vile vya Afrika ya Mashariki.
Hawa jamaa ambao kwa kawaida hupendelewa kuitwa MD Russia wamekuwa wakipeana upendeleo huku wakiwatenga MD Dar. Wamekuwa wakitumia lugha ya kirusi kupeana mikakati makazini. Na hakika zaidi ya asilimia 90 si wazuri katika shughuli za kuhudumia wagonjwa.
Ukiacha umuhimu wa Wizara ya Afya kujijenga vizuri ili iweze kusaidia watanzania, pia iwe makini katika kufuatilia watu waliosoma nje ya nchi kama kweli wana sifa wanazozipeleka hapo wizarani. Tumeshawahi sikia baadhi ya watu walioenda kusoma Urusi na China, kwamba wakifika kule huwa hawasomi kwa kuwa ni lazima watafaulu (Hakuna serikali itatoa msaada wa kusomesha watu wako kumi halafu ikaja baada ya miaka sita ikisema wengine tisa walifeli, lakini huyu mmoja pekee ndio kafaulu; hivyo wakitoa misaada kwa watu kumi hakika hao watu kumi watamaliza shule), na wengine huacha chuo ila baada ya muda wao wa masomo kuisha huja Tanzania wakiwa na vyeti feki kwamba tayari wameshamaliza chuo. Bahati mbaya TCU haijaingia kuthibitisha uhalali wa wafanyakazi wa Afya wengine wanaua watanzania kwa kuwa wamekosa elimu.