Dada anamuendea mwanaume kwa mganga

Dada anamuendea mwanaume kwa mganga

Joined
Jan 9, 2013
Posts
39
Reaction score
30
Hbari zenu wanajamii forum kuna rafiki yangu mmoja yupo katika wakati mgumu sana baada ya x wa boyfriend wake kugoma kukubali matokeo kwamba wameachana kwani mdada analazimisha kuendelea na mwanaume wakati mwanaume tayari ameshapata mpenzi mwingine ambaye ni rafiki yangu na uhusiano ulivunjika zaidi ya miezi sita iliyopita na huu uhusiano mpya unakaribia miezi mitatu hivi ,mbaya zaidi huyo dada aliyeachwa amechukua likizo kazini na ametangaza kwamba anaenda kwao kigoma kuhakikisha anamrudisha mwanaume kwenye himaya yake kwa njia yeyote ile .sasa rafiki yangu amechanganyikiwa maana binafsi yake haamini uchawi ila ana hofu huyo dada huko kwao kaenda kumrudishaje mwanaume ,mawazo yenu jamani ni muhimu isije kawa kaenda kuloga

Asanteni
 
aachane na huyo jamaa tuu.
alafu uhusiano wa huyo jamaa na ex wake ulidumu miaka mingapi??
 
Kwenye mapenzi hakuna hata kidogo uchawi wa dawa. Uchawi unao wewe mwenyewe mwanamke mwilini, ukiutumia vizuri mwanaume habanduki ng'o.
 
asante kwa ushauri wako ila inashangaza mtu unawezaje kungangania mapenzi mpaka unachukua likizo kazini ili ukamloge mtu mrudiane je hapo patakua na penzi au kubaka??
 
inasemakana hawakukaa hata mwaka maana dada alikua na tabia za ajabu ajabu kaka wa watu akaamua kubwaga nyanga sasa dada amegoma kukubali ukweli @ JF SENIOR EXPERT MEMBER
 
Amwamini Mungu tu, kwani ndio muweza wa yote!!
 
Kwenye mapenzi hakuna hata kidogo uchawi wa dawa. Uchawi unao wewe mwenyewe mwanamke mwilini, ukiutumia vizuri mwanaume habanduki ng'o.


wee kumbe inajua mapenzi ni nini
 
Hbari zenu wanajamii forum kuna rafiki yangu mmoja yupo katika wakati mgumu sana baada ya x wa boyfriend wake kugoma kukubali matokeo kwamba wameachana kwani mdada analazimisha kuendelea na mwanaume wakati mwanaume tayari ameshapata mpenzi mwingine ambaye ni rafiki yangu na uhusiano ulivunjika zaidi ya miezi sita iliyopita na huu uhusiano mpya unakaribia miezi mitatu hivi ,mbaya zaidi huyo dada aliyeachwa amechukua likizo kazini na ametangaza kwamba anaenda kwao kigoma kuhakikisha anamrudisha mwanaume kwenye himaya yake kwa njia yeyote ile .sasa rafiki yangu amechanganyikiwa maana binafsi yake haamini uchawi ila ana hofu huyo dada huko kwao kaenda kumrudishaje mwanaume ,mawazo yenu jamani ni muhimu isije kawa kaenda kuloga

Asanteni

Hiyo hofu tu ndiyo itakayomrudisha jamaa kwa demu wake wa zamani. Sasa hivi huyo rafiki yako kila atakachofanya mwanaume atakuwa anaona kama 'amelogwa'... Hii itafanya uhusiano wao usiwe wa amani, na itawasababisha waachane, na jamaa atarudi kwa demu wake wa zamani...
 
Kama hofu imemjaa kiasi hicho kabla mbaya wake hajarudi toka Kigoma, hiyo ni dalili kuwa ameshakubali kuachia ngazi na hapo anaweza kumpa ushindi mkigoma ama wakakosa wote.

Anachotakiwa kufanya asitishe uhusiano wa kimapenzi (ngono) amrudie Mwenyezi MUNGU kwa kutubu makosa yake especially kuvunja amri ya sita (lakini kama ni mkiristu) na hapo atajiweka kwenye ulinzi imara dhidi ya nguvu za kishetani na muda huo waanze taratibu nyingine za kufunga ndoa takatifu ili hali wakiwa nje ya zinaa.
 
wao wenyewe sii ajabu wanavunja amri yake ya sita..ndio akiwa na matatizo amtafuteMungu tena loh"!!

hahaaah! Hata kama wapi katika dhambi namna gani wakimrudia Mungu hawezi kuwatupa.
 
inasemakana hawakukaa hata mwaka maana dada alikua na tabia za ajabu ajabu kaka wa watu akaamua kubwaga nyanga sasa dada amegoma kukubali ukweli @ JF SENIOR EXPERT MEMBER

hiyo JF SENIOR EXPERT MEMBER id ya nani??
 
Mwanamke mshirikina ni wakuepuka daaaah!
 
na wewe nenda Sumbawanga

eh kumbe sumbawanga ndo kuna walozi eeh???!!! mi namshauri iwe lesson kwake next time akipata mwingine awe na mapenzi ya kweli lazima itamlipa tu atapendwa tu...mapenzi ya dawa hayadumu remember eazy come eazy GO!
 
Mapenzi ya kweli hayalazimishi, kama anampenda mbona wangerudiana tena na kuendelea kula raha?
 
Hbari zenu wanajamii forum kuna rafiki yangu mmoja yupo katika wakati mgumu sana baada ya x wa boyfriend wake kugoma kukubali matokeo kwamba wameachana kwani mdada analazimisha kuendelea na mwanaume wakati mwanaume tayari ameshapata mpenzi mwingine ambaye ni rafiki yangu na uhusiano ulivunjika zaidi ya miezi sita iliyopita na huu uhusiano mpya unakaribia miezi mitatu hivi ,mbaya zaidi huyo dada aliyeachwa amechukua likizo kazini na ametangaza kwamba anaenda kwao kigoma kuhakikisha anamrudisha mwanaume kwenye himaya yake kwa njia yeyote ile .sasa rafiki yangu amechanganyikiwa maana binafsi yake haamini uchawi ila ana hofu huyo dada huko kwao kaenda kumrudishaje mwanaume ,mawazo yenu jamani ni muhimu isije kawa kaenda kuloga

Asanteni



Basi kaisha huyu. Watu wa Kigoma kwa mazingaombwe? Hawa na watu wa Mbeya na baadhi ya makabila kule kwetu Tanga ni vituko tupu.
 
Kwenye mapenzi hakuna hata kidogo uchawi wa dawa. Uchawi unao wewe mwenyewe mwanamke mwilini, ukiutumia vizuri mwanaume habanduki ng'o.

Hayajakukuta,
yakikukuta siku utajua kama uchawi upo au haupo!
 
huyo dada asiogope
wa kuloga hua hawasemi bana
mtu mzima hatishiwi nyau atii!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom