Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 786
- 1,315
Upo msemo usemao kuwa VITA HAINA MACHO! Usemi huu unatokana na ukweli kwamba risasi zikishapigwa hazibagui nani anahatia na nani hana hatia. Machafuko yakisha fika hatua hii sirahisi tena kuyadhibiti. Yatazaa vicious circle ya visasi juu ya visasi kitakachofuata hatutakuwa na Tanzania tuliyoizoea tena.
Hakuna mtanzania mwenye utu na akili timamu ambaye hajaguswa na mauaji, kujeruhi na uharibifu wa mali uliofuatia Octoba 29. Ukitazama video clip zinazotembea kwenye mitandao, kiukweli mioyo inakufa ganzi. Huu ndio ukweli ambao hatuubishanii tena!
Swali kubwa ni tunatokaje hapo? Je, tukisema iwe jicho kwa jicho, tutaua wangapi? Tutajeruhi wangapi? Tutafunga wangapi? Na baada ya hivi visasi, wahanga wa visasi, wakiamua kujibu mapigo mwisho wake utakua ni nini? Ndugu zangu kosa halisahihiswi kwa kosa, giza halifukuzi giza, hivi ndivyo Martin Luther King, mpigania haki za watu weusi maarufu alivyotufundisha.
Ni kweli makosa yamefanyika, na kama tukiwa wakweli wadau wote wa matukio yale wanachakulaumiwa, kuanzia serikali, vyombo vya dola, waandamanaji, na vyama vya upinzani. Katika hali hii ndipo inakuja hoja ya Bwana Yesu, "Asiye na dhambi na awe wa kwanza kurusha jiwe" Yohana 8:7.
Mm nadhani tunaokataa maridhiano tujifunze kwa majirani zetu Rwanda, utulivu walionao sasa ni matokeo ya campaign nzuri ya maridhiano iliyoitwa "Ndi Umunyarwanda" Kadhalika South Africa, baada ya utawala dhalimu wa ubaguzi wa rangi kilichoituliza nchi yao ni Truth and Reconciliation Commission (TRC) iliyoongozwa Archbishop Desmond Tutu.
Tukiamua kama serikali ni ngangali basi wananchi ni ngunguli, tutazika ndugu zetu, tupata walemavu wa kutosha, biashara zitafilisika na miondombinu mingi itaharibika. Katika hali hiyo nani atakuwa ameshinda?