d-link wireless access point

d-link wireless access point

Davies_007

Member
Joined
Apr 22, 2010
Posts
59
Reaction score
0
Wakuu wa Kazi Mambo Vipi? Jamani Naomba Mnisaidie Akili na Mawazo Kidogo.
Nimefungiwa wireless Internet Sasa nataka Mpaka Office zingine waweze kupata Internet Nikapata wazo la Kufunga d-link wireless access point Sasa Naomba Mnishauri kama d-link wireless access point ni chaguo sahihi na Kama Mtu anajua price yake Naomba anijulishe Tafadhari
 
D-link ni nzuri ila linksys inakuja juu kwa sasa, bei sio gali sana hapa Arusha D Link DIR-600 Wireless 150 Router ni 78,000 sijui wewe upo wapi kama ni Dar itakuwa rahisi zaidi
 
Umetaja wireless D-LINK, inaonesha tayari umeshaamua kuweka hiyo. Wireless AP/Router zipo aina kibao, wireless (a),(b) ambazo outdated,(g) up to 54mb/s and (N) upto 300mb/s. D-link hata mimi naitumia sina matatizo nayo.
Ushauri: inategemea hizo office unazotaka ku-share nao internet zipo umbali gani same building? kama kuna kuta (walls) between your office na hizo office zingine basi tumia wireless N, speed kubwa na inakwenda mbali zaidi ya (g) na ni "future proof" pia ni compatible na (a)/(b)/(g) na N yenyewe. Kuhusu bei subiri walio maeneo yako watakupa ushauri. Maelezo mengine ingia kwenye website ya d-link, pia unaweza kuangalia Netgear, Belkin etc.
 
dlink ni nzuri ila inategemea ofisi namna ilivyokaa. wakati mwingine unaweza kuta partition za ofisi au material yaliyotumika inakulazimu kufunga zaidi ya moja ili kupata signal nzuri, nafikiri pia umewahi kufanya configuration maana security ni muhimu la sivyo wajanja watatumia kiulaini na ukifunga zaidi ya moja nakukumbusha kuweka kwenye channel moja na AP name moja ili moja pc ikipata signal zaidi ya moja itaweza kuunga zote kwa pamoja ili kupata signal nzuri
 
binafsi napendelea NETGEAR nafikiri ni more reliable na easy to configure,unaweza configure as bridge or repeater,but is litle expencive than d-link
 
D link ni nzuri kwa kiasi chake. sie hapa ofisini kwetu kuna kuta kama nne tano hivi. na inarusha mateke ile mbaya. ofisi yetu ni nyumba ya ghorofa tano na inapiga kutoka chini hadi juu from dawn till dask
 
D link ni nzuri kwa kiasi chake. sie hapa ofisini kwetu kuna kuta kama nne tano hivi. na inarusha mateke ile mbaya. ofisi yetu ni nyumba ya ghorofa tano na inapiga kutoka chini hadi juu from dawn till dask

Model gani kaka?
 
Back
Top Bottom