Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,158
- 9,184
Imebidi nikae chini nifikiri juu ya yanayojiri kutoka huko bondeni Afrika Kusini na mustakabali wa uhusiano wetu na hawa wenzetu wa Sauzi.
Nimewalinganisha Cyril Ramaphosa na Jacob Zuma katika kuongza Afrika Kusini na kuwalinganisha uongozi wao na Tanzania kwa ujumla.
Tulikotoka i ndwele lakini lazima tugange yajayo.
Kati ya viongozi wawili wa Sauzi niliowataja ingalau Jacob Zuma anajua kuwa kuwepo kwake pale alipokuwa Rais ni kwa juhudi za waafrika wenzake, wakiwemo waTanzania.
Mugabe aliwahi kusema mzigo mzito Zaidi katika kuikomboa afrika Kusini ulibebwa na Tanzania.
Wapigania uhuru walijengewa makambi, wakapewa passports za Tanzania na kiujumla waliishi kama vile vijana wetu wanavyoishi katika makambi ya JKT au Zaidi, tena kwa miaka au miongo kadhaa.
Zuma aliishi Tanzania.
Ramaphosa hakuwahi kuishi nje ya Afrika Kusini, na namkumbuka miaka ya 70's na 80's alikuwa kijana simple wa kupiga makelele majukwaani.
Mimi namkumbuka vizuri na madevu yake kama Bushiri.
Kuna tetesi kuwa Ramaphosa alifadhiliwa vizuri na makaburu kufika hapo alipo ili asimamie matakwa yao.
Hatushangai leo from a simple guy kawa ni Tajiri mkubwa mwenye makampuni ya biashara.
Mtazamo wa Ramaphosa unalingana sana na mtu aliyefadhiliwa na makaburu.
Kuna clip imeiona wakati wa kampeni yake ya Urais naye ali wahi kulitaja tatizo la wahamiaji walioingia Zauzi kama tatizo la wasauzi.
Mimi sina maneno na kuwachukulia hatua wahamiaji haramu maana hata Tanzania tunao.
Lakini hili la kuwachoma moto, kuwapiga na kuchoma biashara za wahamiaji, wengine Mbao ni wahamiaji halali, that's a political crime.
Serikali ya Ramaphosa ingweza kuwa kusanya hao wahamiaji haramu na, kma tunavyofanya Tanzania, na kuwapeleka makwao kistaarabu.
Lakini Ramaphosa si Mtanzania wala sim mtu ana uhusiano wa kindugu na watanzania na waafika wengine, yeye ni mSauzi first.
Serikali yetu ya 60's ili wafadhili waafrika wa Afrika Kusini walipokuwa wanateswa na serikali ya kiaburu.
Leo wameshika serikali, na serikali hiyo inakamata Ndege za serikali iliyowakomboa.
Wananchi waafrika wenzao Sauzi wanapigwa au kuteswa na kuuwawa, mpaka unajiuliza , hivi ni hawa binadamu tulikuwa tunakesha JKT na kuimba
"kaburu matata hiya….hiya... Kaburu matata hiya …….hiya...…"
" Kruger naye ….. tutamkata……...Kruger naye tutamkata……."
Was all that in vain?
Mwalimu na Mandea must be turning in their graves.
Kweli tenda wema uende zako!!!!
Ramaphosa kama alibariki kuuwawa kwa wasouth wenzake kwenye ule mgodi wa dhahabu, anajari nini kuhusu waafrika wengine?
He thinks he can fix the economic problems of SA by creating another fiasco like the one that killed his fellow country men. He is lying to himself. He would not be able to move even an inch by creating chaos. After kicking out foreigners, the next move will be himself to get out of that seat.
On the other hand, waafrika wengine tunacholazimisha SA nini? Tujenge nchi zetu. Tuwaondoe hawa wasouth wanaojifanya eti expatriates wa migodi na maeneo mengine. Lets make it hard for them legally. Sio kuuana kama wanavyofanya