Cyprian Musiba: Yanga msicheze dabi, TFF inaongoza kwa upendeleo

Cyprian Musiba: Yanga msicheze dabi, TFF inaongoza kwa upendeleo

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,085
Reaction score
7,091
Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba, amesema Klabu ya Yanga inapaswa kusimamia msimamo wake wa kutocheza mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba, iliyopangwa kufanyika Juni 15, 2025.

Akizungumza leo Mei 6, 2025, jijini Dodoma, Musiba amesema Serikali haipaswi kukaa kimya huku viongozi wa soka wakiendekeza upendeleo, ushabiki na maslahi binafsi katika uendeshaji wa mchezo huo.

Soma Pia: Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Musiba amesisitiza kuwa anaunga mkono uamuzi wa Yanga kuendelea na msimamo wake wa kususia mechi hiyo, akisema ni hatua ya kulinda heshima ya mpira na uwiano wa haki miongoni mwa vilabu.

 
Huyo alishashindwa uchambuzi wa michezo tokea zamani, hana tofauti na Ambokile. Hawaujui mpira zaidi ya uchawa tu
 
Wewe kenge kama humjui bora utulize shanga. Musiba alikuwa mtangazaj na mchambuzi kwenye vituo vya habari vya Magic FM na Channel ten kipindi hicho na kina dr. Leak na Manara.
Sasa hapa kasema yeye ni mchambuzi mkuu?

Acha kukurupuka mkuu. Kwani mtu kutoa maoni yake ni lazima awe mchambuzi?
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;
JamiiForums1222824732.jpeg

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Malalamiko (Lia lia) SC.
4. Makelele SC.
5. Mipang'ang'a SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyang'au SC.
8. Manyaunyau (Mapaka) SC.
9. Mazumbukuku SC.
10. Mikia SC.
11. Mwakarobo SC.
12. Ngada SC.
13. Zuwena SC.
14. Kufa Kiume SC.
15. Kikanuni SC.
16. Panya Roads SC.
17. Bebwa Bebwa (Mbeleko) SC.
18. Bahasha SC
19. 5imba SC.
20. Ubaya Ubwege SC.
21. Manguruwe SC.
22. Objective Football SC.
23. Mazombi SC.
24. Kolowizard SC.
25. Visingizio(Visababu)SC.
26. Wekundu wa Msimbazi SC.
27. Mbuzi SC.
 
Tff wamefeli kuendesha soka la Tanzania .
Hili Sakata Yanga akiona hawezi kupata haki Kwenye taasisi za michezo akaenda Kwenye mahakama za kawaida kufungiwa na Fifa kwa Tanzania kutafuata.
 
Back
Top Bottom