CWT yasisitiza mgomo upo palepale Jumatatu tar 30/07/2012

Mwanzisha mada malengo yako ni nini hasa kwani hueleweke bayana mgomo ni kesho una madhara au hauna kwani nini tujifiche nyuma ya keyboard na kuanza kupredict mambo yajayo kwani wewe ni yule aliyefariki?
Tusubiri tuone hiyo kesho mgomo upo ama la na kama upo una madhara ama vinginevyo tuache hizi bla bla labda kama unavuja jasho kwa nguvu ya chochote mfuko kuwatetea watu flani uwe wazi..
 
uliyeanzisha uzi hujui unachosema ni kama umetumwa tu na kwa hasira na ungenikuta nimepiga viroba ningekutukana sana.
 
nani alikwambia shule zikifungwa mwalimu nae anafunga? Na nani alikuambia kwamba mgomo unakikomo? Acha kufikiria kwa kutumia masaburi ww
 

Nimeona nisichangie niwape nafasi wengine.......jipange
 
hivi wewe kibaraka ushawaona walimu ni vilaza??kumbuka walimu wa sasa tumesoma..tumeenda shule tuna degree zetu bana,who ar you kutusemea walimu??acha upuuzi bana,,walimu mishahara haitoshi na hata kama cwt wangekua wabovu na mafisadi lakini kwa hili tuko pamoja nao,,akitokea mtu kama wewe mwenye akili maji basi walimu tunakupuuza kwa nguvu zooote,,kwa taarifa yako walimu we are more than serious and we ar breathing fire,,,,tunagoma j3 kuanzia saa 1.30 asb.vitisho,dhihaka na utapeli hautasaidia kwani kwa hili walimu hao unaosema wako vyuoni ndo wakwanza kuliunga mkona...wewe bado unataka nilipwe mshahara wa 273,000 kwa mwezi??inisaidie nini?tumeomba madaraja huu mwaka wa 3 since tumegraduate bila msaada,,jamani watanzania hamtuonei huruma??mbona sisi tunawajali watoto wenu??hapana watanzania siasa zimezidi na sasa mmeziingiza mpaka kwenye maisha ya watu hata wasio husika...mungu tusaidie mgomo wetu uwe wa kihistoria na hapo kila mtu ata draw an example kwa walimu...
hatuko tayari kutahiriwa bila idhini yetu ,,mtuache na moto mtauona
 
Walim wakigoma nipigwe ban milele hawawez hawa, kwanza afisa elim atapewa maangizo kuhakikisha waalimu wote wanahudhulia na kupeleka majina ya waliogoma. Tusubiri.
 
mgomo wa walimu ni njia iliyobuniwa kudhoofisha mgomo/madai ya madaktari.jumatatu mahakama inawapiga stop jumanne wote kazini.
Mkoba na mgaya ni wasanii mno!
 

Sasa unataka kutuambia umuhimu wa walimu kwa serikali upo tu hata pasipo wanafunzi? Kama ingeona hivyo si madai yenu yangetimizwa hata bila mgomo. Kwa nini mgome basi.
Tatizo mna huruma, uoga na usnitch; kamwe msitarajie utekelezaji wa madai yenu kwa mwendo huu.
Na kama mmevutana kwa muda mrefu hivyo bila kulianzisha, mnaamini mtafanikiwa kupachimba kwa muda mrefu bila kikomo?
Acha Uvivu ana nia tu ya kuwasihi muwe strategic, kuikabili serikali yenye kujiita sikivu. Likizo kamwe hamtaweza kuitikisa serikali.
 
acha ujinga mgomo wa walimu uko palepale,,sensa ni ajira mpya na hayupo mwalimu hata mmoja aliyeteuliwa bali walimu wameomba kwa mkurugenzi kama raia wengine,,usituvunje moyo kwa elimu na upeo wako mdogo j3 saa 1.30 tuko nyumbani kupumzika kama kawaida,,,,wewe na mkeo mwende mkafundishe nanyi mlipwe 273,000
 
Kwanza TZ ni nchi yao pia, sasa wanamgomea nani???!!! Kikwete? CCM? Watafute njia nyingine na siyo mgomo.

watafute njia gani? waambie njia gani? wanadai maslahi yao acheni wadai maslahi yao kama wewe upande wako mambo yanakwenda smooth basi kaa kimya wakati ukifika na wewe utanyanyuka na kudai ya kwako. Watanzania tupunguze unafiki, usije ukaona kwamba wewe unapata leo basi mambo yatakuwa shwari siku zote hebu fikiria una watoto na ndugu zako wanaishije? Sisi ndo tumewasaliti hata ndugu zetu vijijini sababu ya ubinafsi na unafiki.
 

Kuna vitu bado hukuviangalia ambavyo vina mantiki, kama je huu mgomo una mantiki?na pia hayo unayosema kuwa ndo wanayodai walimu ni ni kama umbeya , ina maana hapo CWT hakuna wasomi wa fedha wanaoweza kukukokotoa kufikia mshahara kwa mazingira ya sasa?si kweli mi nafahamu wapo na hawadai kama unavyoeleza, acha kupotosha.Kuhusu ni lini wamefanya timimg ya kuanza mgomo;ni kwamba ni alhamisi tu walipoona inapasa kufanyika hivyo, wasingesubiri tena mpka katikati ya muhura, hata hivyo mgomo huu hauna kikomo kama ilivyoelezwa.Mi kimsingi naasa ni vyema kuchambua mantiki ya mgomo ni yapi?.je ni sahihi walimu kugoma kudai masilahi yao?kuna mwafaka wowote ambao serikali imeutoa kuondoa kero za madai hayo? kama hakuna basi mantiki ya mgomo yapo.Na pia kuhusu ubadhrifu , hayo unayoyasema unaoushahidi wa hayo ama unataka kuunganisha na dhamira yako ya kutumika kuonyesha serikali ni sahihi kukandamiza walimu?
 
Naona walimu mnafikiri huu uzi upo kipropaganda zaidi, ndo yale kwamba wengi hamtaki ku-think outside the box. Hapa tayari mnaamini mgomo wenu utakuwa na effect.
Sawa kwa sasa mnaonekana mna machungu, lakini jueni kuwa mkiwa na machungu ni rahisi pia kwenda kichwa kichwa bila kufikiria na hatimaye kuangukia pua.
Na masnitch wa kwanza watakuwa hao hao waliowahamasisha, ikiwezekana tumieni mbinu ya kupangua uongozi kila mnapowashakia.
 

Mwalimu mwenzangu, naomba unielewe vizuri....na sio kuwa mimi natumika vibaya no plse. Mimi naunga mgomo kwa 100% lakini wanachokosea CWT ni timing ya mgomo. Kumbuka kuwa ikama ya walimu wa A'Levels TZ plus ikama ya wakufunzi wa vyuo vya Ualimu bado haiwezi kuifikia ikama ya walimu wa shule za msingi wote TZ au kufikia ikama ya walimu wa secondari wa O'level za Gvts zote.

Sasa primary zinafungwa, sekondari...O'level zinafungwa zote kuanzia tarehe 03.08.2012 , Sasa je hilo kundi litatia nguvu ipi ku-push mgomo uwe effective wakati wapo likizo hata kama hawaendi kuandikisha SENSA?

Nadhani umesoma Pyschology kuna kitu kinaitwa Motivation..how to motivate your student in the classroom....huwa tunasema a teacher should use timed reinforcement so as to be so meaningful by motivating student...!

Sasa CWT wamekosea timing ya Mgomo huu....kwanini wasingeweka early june, au kuanzia wiki la kwanza la kufungua shule...za msingi na sec ambapo hapo moto wake ungekuwa ni wa Petroli?

@ gfsonwin nadhani sasa umenielewa vizuri sana mwalimu mwenzangu.
 
Acha kutumika wewe,kama wametumia hyo 240 kwa wilaya zote tanzania still bado naona ni ndogo sana,mgomo upo palepale walimu msimsikilize huyu mtoa pumba hapa anatumika na TISS kuwaaribia moods!!!

Hivi hapa anayetumika ni nani? Kudai haki yako mpaka mlipwe? Pesa zilizopelekwa wilayani kama sio hongo ni kitu gani? Kama kweli una madai ya msingi huitaji kulipwa pesa ili kuhamasishwa ni unafiki mtupu

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…