CWT ipi? Labda huwajui viongozi wao. Siku moja nimekaa na katibu wa chama hicho wilaya moja, mtangulizi wake alikuwa analipia huduma ya Internet inayotolewa na TTCL sh 45,000/= kwa mwezi. Huyu mheshimiwa alipokuja, akasitisha huduma ile kuwa ni ghali wakati huo huo ananunua magazeti ya tarehe iliyopita kila siku, magazeti amabayo angeyasoma mtandaoni asubuhi kabla hata hayajafika vibandani. Elimu inahitajika kwa viongozi wa CWT huko mikoani.