CWT na mitandao ya kijamii kama JamiiForums/facebook

samoramsouth

Senior Member
Jan 16, 2011
191
30
Cwt ingejaribu kujitanua kwa wadau wake kwa kujiunga na mitandao ya kijamii.
Faida ni kuwawezesha walimu vijana ambao wengi wao wamejiunga na mitandao hii kuweza kupata in depth details za shughuli za chama hicho. Lakini pia itakiwezesha chama kupata maoni na response ya walimu katika madai mbalimbali kwani kwa kutumia namba ya uanachama maoni mbalimbali yanaweza kutolewa na hivyo chama kinaweza kujua ni watu wa aina gani kinawasimamia na mitazamo yao.
Nawasilisha.
 
safi kabisa nadhani pia itasaidia kuwabana hawa magamba walipe stahili zao.Dawa ya deni ni kulipa cha ajabu wamefanya sherehe za miaka hamsini ya uhuru kwa pesa mingi kwenye madeni ya walimu wanaleta ngojera!
 
CWT ipi? Labda huwajui viongozi wao. Siku moja nimekaa na katibu wa chama hicho wilaya moja, mtangulizi wake alikuwa analipia huduma ya Internet inayotolewa na TTCL sh 45,000/= kwa mwezi. Huyu mheshimiwa alipokuja, akasitisha huduma ile kuwa ni ghali wakati huo huo ananunua magazeti ya tarehe iliyopita kila siku, magazeti amabayo angeyasoma mtandaoni asubuhi kabla hata hayajafika vibandani. Elimu inahitajika kwa viongozi wa CWT huko mikoani.
 
Hivi hamjui kuwa cwt ni tawi la magamba? safu ya uongozi wa taifa wote ni makada wa ccm isipokuwa mmoja tu naibu katibu mkuu. ndo maana wako kimya ili waendelee kula vinono.
 
Ilobaki walimu wajiengue kwenye hicho chama tu maana hamna cha maana wanachowasaidia
 
Hivi hamjui kuwa cwt ni tawi la magamba? safu ya uongozi wa taifa wote ni makada wa ccm isipokuwa mmoja tu naibu katibu mkuu. ndo maana wako kimya ili waendelee kula vinono.

Sikubaliani na wewe maana ni muongo.
Nawajua vizuri baadhi ya viongozi wengi wa chama hii wasio na mashiko kwenye vyama vya siasa na najua ambao wamewahi hata kugombea ubunge nje ya ccmagamba.
usidanganye watu hapa.
 
Cwt ya Mkoba! Hawa jamaa sioni hata kidogo wakimsaidia mwl kwa sababu wanaitisha migomo na migomo ikikaribia wanaiahirisha huku stahili za walimu hazijatatuliwa,kuna haja ya kuubadili huu uongozi wa Cwt
 
nyie mnafikiria kujiunga na social network wakati scotland UK wanafikiria jinsi gani walimu wao wasiendelee kutumia hizo social networks. kweli binadamu tuko tofauti?

viva la Tehama
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom