CWT Mkoa wa Dar-es-Salaama wayatambua makontena 20 aliyoyakana Makonda na yadai Makonda aliwashirikisha yalipowasili

Baada ya mzigo huo kutolewa bandarini nitahitaji kuziona hizo ofisi za Walimu zitakazowekewa Mazuria na samani kutoka nje ya nchi!
 
Naweza sema kwa uwazi.. RC Makonda hahusiki kabisa ..Hizo ni samani za ofisi za waalimu shule za msingi na sekondari Dar...

Sbb watu wengi humu JF na kwingineko mnataka sana kumchafua RC Makonda na sbb anapiga kazi vizuri sana na mfano wa kuigwa, mnajisumbua tu, fanyeni kazi zenu mnapoteza muda wenu bure.. Hahusiki kabisa
makonda hayajui.....cwt ...makonda anayajua...!!!!
 
Utata umeendelea kuandama umiliki wa makontena 20 yaliyotajwa na Mamlaka ya Mapato (TRA), kuwa miongoni mwa yale yatakayopigwa mnada kwa kukaa bandarini muda mrefu, baada ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kukana kuwa sio ya kwake.

Awali, TRA ilitoa tangazo katika gazeti la Daily News, ikisema mtu aitwaye Paul Makonda bila kubainisha kama mtajwa ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au la, anamiliki makontena 20 yenye bidhaa mbalimbali zikiwamo samani katika bandari kavu ya DICD.

Hata hivyo, akizungumza jana wakati akizindua kamati ya mapendekezo kuhusu wanawake waliotelekezwa na wenza wao, Makonda alisema hajui chochote na amesikia habari hizo kwenye magazeti kama walivyozisikia watu wengine.

“Sidhani kama nahusika na jambo lolote lile na sijui chochote, hilo unalolisema hata mimi nimesoma kwenye magazeti kama ulivyosoma wewe. Nafikiri zilikuwa ni habari za jana na leo nimesoma nyingine,” alisema.

Makonda alisema Serikali hufanya kazi zake kwa maandishi na yeye hana nakala yoyote inayohusiana na mzigo huo.

“Sio suala la kwangu kabisa, nimekusikia wewe kama mimi nilivyosikia jana (juzi) na ninafikiri tutaendelea kusikia hivyo hivyo na ndio maana katika hizo habari hakuna sehemu yoyote umeona nimenukuliwa kusema kama ni mali zangu,” alisema Makonda.

Hata hivyo, Februari 16, Makonda alikaririwa katika mtandao wa gazeti la Serikali la HabariLeo kuwa alipokea makontena 20 yenye samani zitakazotumika katika ofisi za walimu zinazoendelea kujengwa ukiwa ni sehemu ya shehena ya makontena 36.

Ilielezwa kuwa samani hizo za ofisini zilizokuwa na thamani ya Sh2 bilioni, zilitolewa na Watanzania wanaoishi Marekani wanaojulikana kama Six Region Diaspora Council.

Mei, 12 kaimu kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA, Ben Asubisye alisema wamiliki wa mizigo hiyo wanatakiwa kuikomboa ndani ya siku 30 kuanzia siku hiyo. Katika tangazo hilo lenye orodha ya makontena zaidi ya 800, jina la Paul Makonda limejitokeza mara 20 akiwa mpokeaji wa makontena 20 yakiwa na bidhaa kadhaa, zikiwamo samani.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo aliliambia Mwananchi juzi kuwa mamlaka hiyo imetoa notisi ya siku 30 kwa waagizaji wa mizigo ambayo imekaa bandarini kwa zaidi ya siku 90.

“Tangazo lililotolewa ni notice (taarifa) kwa wahusika ili wakomboe mizigo yao ndani ya siku 30. Isipokombolewa itanadiwa. Mizigo hiyo inaweza kuwa ni ile ambayo haijalipiwa kodi au hata ile iliyolipiwa lakini haijaondolewa,” alisema.

Alipoulizwa kama shehena hiyo ni mali binafsi ya Makonda au ya ofisi yake, Kayombo alisema: “Majina yaliyoandikwa kwenye magazeti ndiyo taarifa za consignees (wapokeaji) zilizopo kwenye nyaraka.”

CWT wayatambua

Wakati Makonda akikana kuwa hahusiki na mzigo huo, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema kina taarifa za uwepo wa makontena 20 ya mizigo yenye vifaa na samani za ofisini yaliyopo bandarini.

Mwenyekiti wa CWT mkoani hapa, Amina Kisenge aliliambia Mwananchi jana kuwa, baada ya makontena hayo kuwasili bandarini, Makonda aliwachukua baadhi ya walimu na wanafunzi na kwenda kuwaonyesha vifaa hivyo.

Hata hivyo, alisema aliwachukua walimu na wanafunzi na sio chama akisema kwa kawaida katika mchakato huo si lazima CWT ishirikishwe, lakini shule na walimu walishirikishwa kuwasili kwa vifaa.

“Kama ni vifaa vya shule kwa ajili ya walimu tuna taarifa walimu wakuu pamoja na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari tulishirikishwa na mimi nikiwemo kama mwalimu, tulikwenda na mkuu wa mkoa mpaka bandarini na kuviona vifaa hivyo,” alisema Kisenge.

Chanzo:Mwananchi

"Better were JK days"
    
Kwi! Kwi! Kwi!
 
Vichwa vya train havikuwa na mwenyewe lakini serikali imevinunua. Sijui toka kwa nani.
Ambulance hazikuwa na mwenyewe lakini sasa zipo mitaani huko mikoani.
Hayo makontena yatakanwa lakini mwishowe yatapata mwenyewe.
Tukumbuke kila mzigo huja kwa jina maalum. Sarakasi zinaendelea. Only in Tanzania.
 
Alisema "Kisenge"
 
Mkanganyiko kama huo unaweza kuwa na sababu mbili. Kwanza ni uzembe wa mtumaji ambaye badala ya kuleta kama msaada kwa idara ya elimu, ameuleta kama mali ya mwenye jina. Pili mwenye jina hata kama anafahamu ni msaada, lazima kaingiwa na tamaa ya kuteka nyara mali hizo. Hivyo kuna niya mbaya ya kufaidika binafsi na fanicha hizo hata kama anafahamu ni msaada wa idara ya elimu.
 
Hao wanaojiita Six Region Diaspora Council ni akina nani? Waingize kontaina 36 za thamani ya TSh 2 billion bila kufuata taratibu za kiofisi na za TRA watakuwa na akili gani? Sasa kama mali ni ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ukii adress kwa Paul Makonda una maana gani? Unataka huyo Paul Makonda akailipie kodi za TRA kutoka mfukoni kwake binafsi? Una uhakika gani kwamba kontaina hizo zitakapofika Dar, Paul Makonda atakuwa bado ni Mkuu wa mkoa wa Dar?

Ni dhahiri kabisa hao wanaojiita Six Region Diaspora Council wakishirikiana na huyo wa CWT ni wapiga dili. Na inawezekana humo kwenye makontaina yao kuna madudu mengine wameficha hususani magari ya kifahari na unga! TAKUKURU ifanye kazi yake kwa kuanza kumkamata huyo Amina Kisenge ili asaidie upelelezi.
 
Trust me,,,kwa nilivouelewa mchezo ni hivi

Makoñda ameyakana kwa sababu ameona walivomtaja jina lake magazetini wamemkosea heshima,

Na yupo sahihi kusema sio yake sababu ni kweli sio yake ,na lazima hajalipa kodi,,,

Hii movie watatumbuliwa watu wa TRA na bandari pale ambapo commando mkuu atajitokeza na kudai ,kua

Watendaji wa bandari na TRA wamekwamisha mizigo,hivo wanarudisha nyuma maendeleo
 
Naweza sema kwa uwazi.. RC Makonda hahusiki kabisa ..Hizo ni samani za ofisi za waalimu shule za msingi na sekondari Dar...

Sbb watu wengi humu JF na kwingineko mnataka sana kumchafua RC Makonda na sbb anapiga kazi vizuri sana na mfano wa kuigwa, mnajisumbua tu, fanyeni kazi zenu mnapoteza muda wenu bure.. Hahusiki kabisa
Ha haaaa haaaaa Wewe jamaa bwana!
 
Back
Top Bottom