CWT kimekuwa chama cha siasa au Kuna mambo hayako sawa?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,124
2,092
CWT jitafakarini,
leo rais JPM pamoja na kwamba hakuwa open sana lakini bango la asilimia 2% liliwalenga ninyi.

Najiuliza sana kama CWT nacho kimekuwa chama cha siasa maana si kwa "bango" lile tena mbele ya wafuasi wenu (walimu). Najiuliza, ni nini kilimkera Rais wetu mpaka aamue kuwashukia hadharani?
Wajuzi wa mambo hebu tujitafakarishe kidogo:

1. Hivi kweli mheshimiwa anawaonea huruma sana walimu kukatwa 2% (about 14 elfu kwa mwalimu wa degree anayeanza kazi AU mwalimu ngazi ya - TGTS D?

2. Kama asilimia 2% ni kubwa, vipi asilimia 15% inayokatwa na heslb (zaidi ya laki moja)?

Rais wa wote, CWT wamekukosea nini? Nini hakiko sawa kwao au ulitaka wafanye nini kupitia hiyo 2%?
 
Yawezekana lakini kama ni tawi la ccm na yeye ni m/kiti wa ccm kwa nini aliumbue tawi lake?
Kama sisonje anawaumbua mawaziri sembuse hilo tawi uwt ccm?hawa walimu utumika katika kupiga kura tu na kupewa sukari na mkate kisha wanarudi kwenye matatizo vilio kwa miaka 5

$wissme
 
Niliwahi kusema humu juu ya cwt kukaa kisiasasiasa. Na mifano ni mingi kupita kiasi kama baadhi ya viongozi wa kitaifa kuteuliwa kwenye nafasi za kisiasa kama ukuu wa wilaya, wabunge wa bunge maalum na wajumbe wa rasimu ya katiba na hata kugombea ubunge na unec kupitia ccm.
Ilisemekana katika uchaguzi uliopita waliinject zaidi ya bilioni 22 tshs kama mchango kwa ccm tuhuma ambazo hazikuwahi kutolewa majibu.
Isitoshe, asilimia kubwa ya viongozi wa wilaya, mikoa hadi taifa ni wazee wa system ambao husaidiwa au kuchomekwa eneo hilo kwa ajili ya kuinform central govt kinachojiri na ndio maana migogoro na migomo mingi kutokufanikiwa.
Najuta kuwa mwanachama wa chama hiki kisichojali maslahi ya wanachama wake zaidi ya kujijali wao tu hapo makao makuu. Sijui wanajisikiaje pale wanachama wao wanavyodhalilika na mazingira duni na vipato hafifu?
 
Umewahi somewa mapato na matumizi ya CWT ,hapo ndo utajua Hamna kazi rahis tz kama kuongoza,MTU anakatwa mapesa miaka nenda rudi lakini Hamna chochote anachokipata
 
CWT, ni wezi sana, chama kipo kiwizi wizi, pesa zinazokatwa hakuna Editor, mfano wilaya ya serengeti, mr. nyoyooo aliyekuwa mwenyekiti alipiga milioni 40, akaonga milioni 15 viongozi wenye kieleele, ameishia tu kuvuliwa cheo
 
mimi niwaulize kuna chama wafanyakazi ambayo haikati wafanyakazi wake 2% kabla ya kuilaumu mje muitaje hapa. Ninyi hamjui jambo moja pale kuiaandama cwt ni kwa sababu ya kuanzisha benki kitu ambayo kinawapa hofu mbele ya safari na kiiua NMB acha kupelekwa kama gari bovu na hao misukule wa kumumba.
 
Mimi nimeshajitoa cwt nyinyi wengine mnangoja nini?Mikakati yao siku hizi ni ya kisaccos zaidi badala ya kupigania haki za wafanyakazi
 
Ccm imewateka kweli cwt kwa kuwa makatibu wote ni ccm kuanzia katibu mkuu, makatibu wa wilaya na mikoa na hao ndo wanafanya shughuli za chama ikiwemo kuhamasisha migomo nakalika wanakula fedha za chama maruprupu ya chama.
 
Mimi nimeshajitoa cwt nyinyi wengine mnangoja nini?Mikakati yao siku hizi ni ya kisaccos zaidi badala ya kupigania haki za wafanyakazi
huwezi kujitoa cwt usidanganye watu soma kwanza sheria iliyounda vyama vya wafanyakazi inasemaje labda uhame na ubadili kazi nje hapo utakatwa tu
 
Kati ya vyama vyote sioni chama kinachojitahidi kutetea wafanyakazi kama cwt. Kitendo cha rais kuwasifia TUCTA na kuuliza eti asilimia 2 wanapeleka wapi? Kwani vyama vingine vinapeleka wapi? Chama gani kina majengo? Chama gani kina bank. Walimu msikatishwe tamaa na wanasiasa. Uwepo wa cwt ni tishio kwao hasa viongozi kama mkoba na olochi.
 
worse enough majority ya hao waliotumbuliwa vyeti feki, ni waalimu. zaidi ya 70%
 
Yawezekana lakini kama ni tawi la ccm na yeye ni m/kiti wa ccm kwa nini aliumbue tawi lake?
Yeye pamoya na Nkewe wameshaKATWA sana Njuruu za CWT...Leo KALIKUWA KA HASIRA ka makato ya siku za nyuma..Kumbuka mama Jane kakatwa hadi mwaka juzi tu...
 
Kati ya vyama vyote sioni chama kinachojitahidi kutetea wafanyakazi kama cwt. Kitendo cha rais kuwasifia TUCTA na kuuliza eti asilimia 2 wanapeleka wapi? Kwani vyama vingine vinapeleka wapi? Chama gani kina majengo? Chama gani kina bank. Walimu msikatishwe tamaa na wanasiasa. Uwepo wa cwt ni tishio kwao hasa viongozi kama mkoba na olochi.
Uko sahihi mkuu, hapendi kupingwa.
 
CWT jitafakarini,
leo rais JPM pamoja na kwamba hakuwa open sana lakini bango la asilimia 2% liliwalenga ninyi.

Najiuliza sana kama CWT nacho kimekuwa chama cha siasa maana si kwa "bango" lile tena mbele ya wafuasi wenu (walimu). Najiuliza, ni nini kilimkera Rais wetu mpaka aamue kuwashukia hadharani?
Wajuzi wa mambo hebu tujitafakarishe kidogo:

1. Hivi kweli mheshimiwa anawaonea huruma sana walimu kukatwa 2% (about 14 elfu kwa mwalimu wa degree anayeanza kazi AU mwalimu ngazi ya - TGTS D?

2. Kama asilimia 2% ni kubwa, vipi asilimia 15% inayokatwa na heslb (zaidi ya laki moja)?

Rais wa wote, CWT wamekukosea nini? Nini hakiko sawa kwao au ulitaka wafanye nini kupitia hiyo 2%?
Mbona serikali wanakata PAYE 30%?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom