CV za Profesa Assad na Profesa Mbarawa

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Nimepitia CV ya Proffesa Makame Mbalawa nikaikumbuka CV ya Proffesa Assad ..former CAG..

Hebu mwenye CV za watu wengine impressive atuwekee.

Ya Mbalawa hii..

WASIFU WA PROFESA MAKAME MNYAA MBARAWA

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa alizaliwa mwaka 1961 Chokocho Kisiwani Pemba na kupata elimu ya msingi na sekondari katika Skuli ya Chokocho ambayo kwa sasa ni Skuli ya Mkanyageni iliyopo Wilaya ya Mkoani, Pemba na baadae aliendelee na elimu ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Karume huko Mbweni, Zanzibar na kuhitimu mwaka 1981.

Mwaka 1985 Prof. Mbarawa alipata nafasi ya kusoma nje ya nchi huko Urusi akisomea Uhandisi wa Mitambo ya meli (Marine Engineening) ambapo alijiunga na Chou cha “Astrakhan Technical Institute of Fisheries” sasa kinatambulika kama Astrakhan State Technical University (ASTU) ambapo mwaka 1992 alihitimu shahada ya uzamivu katika fani ya uhandisi Mitambo ya meli. Mwaka 1994 alijiunga na Chuo Kikuu cha New South Wales, Sydney, Australia na kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD), mwaka 1999.

Kati ya mwaka 2000 na 2014 Prof. Mbarawa alihudhuria programu za mafunzo mbalimbali kama vile mafunzo ya usimamizi wa miradi huko Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Bussiness School, Afrika ya Kusini mwaka 2000; Mafunzo ya stadi katika ustadi wa kufundisha (Competence in teaching skills), Pretoria Tecknikon, Afrika ya Kusini mwaka 2001; Mafunzo ya “Innovation for Economic development”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani mwaka 2014; Mafunzo ya “Cybersecurity: Intersection of Policy and Technology”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu nchini Marekani mwaka 2015.
Kati ya mwaka 1981 na 1985 alifanyakazi Idara ya Usafiri Baharini, wakati huo ilikuwa chini ya Wizara ya Mawaswiliano na Uchukuzi, Zanzaibar na Shirika la Meli Zanzibar. Aidha baada ya masomo yake ya uzamili kati mwaka 1993 na 1994 alifanyakazi tena kwenye Shirika la Meli Zanzibar.

Mwaka 1999, Prof. Mbarawa alijiunga na Chuo Kukuu cha Stallenbosch, Afrika ya Kusini kama Mtafiti katika Kituo cha Uhandisi wa Magari. Baadae Prof. Mbarawa alifanyakazi katika Chuo cha Technikon Pretoria kwa sasa kinatambulika kama Chuo kikuu cha Teknolojia cha Tshwane (Tshwane University of Technology), Pretoria, Afrika ya Kusini mwaka 2000 akiwa kama Mhadhiri Mwandamizi katika idara ya Uhandisi Mitambo. Mnamo mwaka 2005 alipandishwa na kuwa Profesa Mshiriki (Associate Professor) na mwaka 2009 alipandishwa na kuwa Profesa Kamili (Full Professor) na Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mitambo. Kutokana na taaluma, utafiti na kazi yake ya uhadhiri Prof. Mbarawa amefanya tafiti mbalimbili kwenye maeneo ya “alternative fuels, filtration combustion, soot formation”, n.k. Aidha, amesimamia Wanafunzia mbalimbali wa shahada ya uzamili na uzamivu na ameandidika machapisho ya kitafiti zaidi ya 50. Kati ya Wanafunzi hao wa Uamivu na Uzamili ambao Prof. Mbarawa aliwasimamia sasa hivi wanafanyakazi kwenye Taasisi mbali hapa nchini.

Kwa upande mwengine, mwaka 2010 aliteuliwa na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Jakaya Kikwete, kuwa Mbunge na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Katika kipindi hicho alisimamia miradi mbalimmbali ya sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia kama vile: ujenzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano (NICTBB), Ujenzi wa kituo mahiri cha kuhifadhia data (Nation Data Cente), Mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analogia na kuhamia mfumo wa kidijitali, Uanzishwaji wa mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS), n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka mwaka 2015.

Aidha mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, alimteu Prof. Mbarawa kuwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kwenye Wizara hii chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof. Mbarawa alisimamia kwa mafanikio makubwa miradi mbalimbali ya kimkakati kama vile: Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salam mpaka Dodoma ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ufufuaji wa Shirika la ndege la ATCL ambapo ndege 7 mpya zilinunuliwa, Uboreshaji wa Bandari ya Dar es salam, Ujenzi wa gati mpya huko Mtwara ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ununuzi na Ufungaji wa Scanners 6 mpya Bandari ya Dar es salam, Ununuzi na Ufungaji wa Rada 4 za kisasa kwenye viwanja vya ndege vinne, Ujenzi wa Jengo la Abiria No. 3 Uwanja wa ndege wa Dar es salaam; Usimamizi wa mnada wa kwanza wa masafa ya 700Mhz nchini, Ujenzi wa mabarabara na madaraja, Uanzishwaji wa Shirika la Reli na Shirika la Wakala wa Meli, n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka tarehe 30 June mwaka 2018.

Prof. Mbarawa aliteuliwa tena na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, kuwa Waziri wa Maji tarehe 1 July mwaka 2018. Kwenye Wizara hii chini ya Uongiozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof Mbarawa amefanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji. Kwanza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imeanzishwa ili kukabidiliana na changamoto kubwa ya usimamizi wa miradi ya maji hasa Vijijini. Pili kutokana na changamoto za gharama kubwa ya miradi na kuchelewa kukamilika kwa miradi, utaratibu mpya wa utekelezaji wa miradi ya maji kwa kutumia utaratibu wa force account umeanza kutumika. Tatu, Prof. Mbarawa amesimamia miradi mikubwa ya maji ya kimkakati kwa mafanikio makubwa kama vile mradi wa maji wa jiji la Arusha ambao unagharimu Shilling Bilioni 520 unaendelea kutekelewza kwa sasa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka Tabora ambao unagharimu Shillingi Bilioni 622, miradi wa maji wa miji 28 ambao unagharimu Shillingi Trilioni 1.2 unaendelea kutekelewza kwa sasa, n.k. Kutokana na maboresha mbalimbali yaliyofanyika takwimu zinaonesha kuwa wastani wa idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama vijijini imeongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwezi Machi mwaka 2020. Kwa upande wa mijini, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 84 mwezi Machi mwaka 2020.
Kwa upande wa harakati za kisiasa Prof. Mbarawa, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea 2007 mpaka mwaka 2017 na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kuanzia mwaka 2012 -2017.
 
CV ya Makame na Anachofanya Ni mbingu na ardhi............

Maji tu yamemshinda....

Africa bana
We unasema Maji yamemshinda, wenzako washampamba tayari. Soma hapo chini.
Tatu, Prof. Mbarawa amesimamia miradi mikubwa ya maji ya kimkakati kwa mafanikio makubwa kama vile mradi wa maji wa jiji la Arusha ambao unagharimu Shilling Bilioni 520 unaendelea kutekelewza kwa sasa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka Tabora ambao unagharimu Shillingi Bilioni 622, miradi wa maji wa miji 28 ambao unagharimu Shillingi Trilioni 1.2 unaendelea kutekelewza kwa sasa, n.k.
 
Cv ya Jecha inatakiwa
Alisimamia uchaguzi wa 2015 na kuhakikisha wahuni hawauchezei na kujitangazia matokeo watakavyo. Akaufutilia mbali. Huyu ni kiongozi shupavu mwenye maono ya mbali na mapenzi ya dhati kwa waZanzibar na Tanzania kwa ujumla wake
 
Tatizo ni kwamba watu hawaweki kwenye sekta za taaluma zao ndo maana wanafanya vibaya
Sasa engineer wa meli,kwa nini awekwe kwenye wizara ya maji jamani?
Ndo maana wanafeli kazi
 
Hujui kitu weweee,maji, mitambo na meli hta mwenye degree Moja Ana fiti,sembuse prof kabisa na research kibao Tena na kuandika vitabu na kusimamia project kibao!Mbarawa yupo vizuri Sana Tena hata hapendi makiki
 
Tatizo ni kwamba watu hawaweki kwenye sekta za taaluma zao ndo maana wanafanya vibaya
Sasa engineer wa meli,kwa nini awekwe kwenye wizara ya maji jamani?
Ndo maana wanafeli kazi
DJ wa muziki Bilicans Club MBOWE si angeendelea tu na muziki sasa hivi yeye ndiye angekuwa Diamnond.Kwa nini awekwe mwenyekiti chadema?
 
Nimepitia CV ya Proffesa Makame Mbalawa nikaikumbuka CV ya Proffesa Assad ..former CAG..

Hebu mwenye CV za watu wengine impressive atuwekee.

Ya Mbalawa hii..

WASIFU WA PROFESA MAKAME MNYAA MBARAWA

Prof. Makame Mnyaa Mbarawa alizaliwa mwaka 1961 Chokocho Kisiwani Pemba na kupata elimu ya msingi na sekondari katika Skuli ya Chokocho ambayo kwa sasa ni Skuli ya Mkanyageni iliyopo Wilaya ya Mkoani, Pemba na baadae aliendelee na elimu ya ufundi katika Chuo cha Ufundi cha Karume huko Mbweni, Zanzibar na kuhitimu mwaka 1981.

Mwaka 1985 Prof. Mbarawa alipata nafasi ya kusoma nje ya nchi huko Urusi akisomea Uhandisi wa Mitambo ya meli (Marine Engineening) ambapo alijiunga na Chou cha “Astrakhan Technical Institute of Fisheries” sasa kinatambulika kama Astrakhan State Technical University (ASTU) ambapo mwaka 1992 alihitimu shahada ya uzamivu katika fani ya uhandisi Mitambo ya meli. Mwaka 1994 alijiunga na Chuo Kikuu cha New South Wales, Sydney, Australia na kuhitimu shahada ya uzamivu (PhD), mwaka 1999.

Kati ya mwaka 2000 na 2014 Prof. Mbarawa alihudhuria programu za mafunzo mbalimbali kama vile mafunzo ya usimamizi wa miradi huko Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Bussiness School, Afrika ya Kusini mwaka 2000; Mafunzo ya stadi katika ustadi wa kufundisha (Competence in teaching skills), Pretoria Tecknikon, Afrika ya Kusini mwaka 2001; Mafunzo ya “Innovation for Economic development”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani mwaka 2014; Mafunzo ya “Cybersecurity: Intersection of Policy and Technology”, Harvard Kennedy School, Chuo Kikuu nchini Marekani mwaka 2015.
Kati ya mwaka 1981 na 1985 alifanyakazi Idara ya Usafiri Baharini, wakati huo ilikuwa chini ya Wizara ya Mawaswiliano na Uchukuzi, Zanzaibar na Shirika la Meli Zanzibar. Aidha baada ya masomo yake ya uzamili kati mwaka 1993 na 1994 alifanyakazi tena kwenye Shirika la Meli Zanzibar.

Mwaka 1999, Prof. Mbarawa alijiunga na Chuo Kukuu cha Stallenbosch, Afrika ya Kusini kama Mtafiti katika Kituo cha Uhandisi wa Magari. Baadae Prof. Mbarawa alifanyakazi katika Chuo cha Technikon Pretoria kwa sasa kinatambulika kama Chuo kikuu cha Teknolojia cha Tshwane (Tshwane University of Technology), Pretoria, Afrika ya Kusini mwaka 2000 akiwa kama Mhadhiri Mwandamizi katika idara ya Uhandisi Mitambo. Mnamo mwaka 2005 alipandishwa na kuwa Profesa Mshiriki (Associate Professor) na mwaka 2009 alipandishwa na kuwa Profesa Kamili (Full Professor) na Mkuu wa Idara ya Uhandisi Mitambo. Kutokana na taaluma, utafiti na kazi yake ya uhadhiri Prof. Mbarawa amefanya tafiti mbalimbili kwenye maeneo ya “alternative fuels, filtration combustion, soot formation”, n.k. Aidha, amesimamia Wanafunzia mbalimbali wa shahada ya uzamili na uzamivu na ameandidika machapisho ya kitafiti zaidi ya 50. Kati ya Wanafunzi hao wa Uamivu na Uzamili ambao Prof. Mbarawa aliwasimamia sasa hivi wanafanyakazi kwenye Taasisi mbali hapa nchini.

Kwa upande mwengine, mwaka 2010 aliteuliwa na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Jakaya Kikwete, kuwa Mbunge na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Katika kipindi hicho alisimamia miradi mbalimmbali ya sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia kama vile: ujenzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano (NICTBB), Ujenzi wa kituo mahiri cha kuhifadhia data (Nation Data Cente), Mabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka analogia na kuhamia mfumo wa kidijitali, Uanzishwaji wa mfumo wa mawasiliano ya simu (TTMS), n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka mwaka 2015.

Aidha mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, alimteu Prof. Mbarawa kuwa Mbunge na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Kwenye Wizara hii chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof. Mbarawa alisimamia kwa mafanikio makubwa miradi mbalimbali ya kimkakati kama vile: Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme (SGR) kutoka Dar es Salam mpaka Dodoma ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ufufuaji wa Shirika la ndege la ATCL ambapo ndege 7 mpya zilinunuliwa, Uboreshaji wa Bandari ya Dar es salam, Ujenzi wa gati mpya huko Mtwara ambao unaendelea kutekelewza kwa sasa, Ununuzi na Ufungaji wa Scanners 6 mpya Bandari ya Dar es salam, Ununuzi na Ufungaji wa Rada 4 za kisasa kwenye viwanja vya ndege vinne, Ujenzi wa Jengo la Abiria No. 3 Uwanja wa ndege wa Dar es salaam; Usimamizi wa mnada wa kwanza wa masafa ya 700Mhz nchini, Ujenzi wa mabarabara na madaraja, Uanzishwaji wa Shirika la Reli na Shirika la Wakala wa Meli, n.k. Alihudumia Wizara hiyo mpaka tarehe 30 June mwaka 2018.

Prof. Mbarawa aliteuliwa tena na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari John Pombe Joseph Magufuli, kuwa Waziri wa Maji tarehe 1 July mwaka 2018. Kwenye Wizara hii chini ya Uongiozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Prof Mbarawa amefanya mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji. Kwanza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imeanzishwa ili kukabidiliana na changamoto kubwa ya usimamizi wa miradi ya maji hasa Vijijini. Pili kutokana na changamoto za gharama kubwa ya miradi na kuchelewa kukamilika kwa miradi, utaratibu mpya wa utekelezaji wa miradi ya maji kwa kutumia utaratibu wa force account umeanza kutumika. Tatu, Prof. Mbarawa amesimamia miradi mikubwa ya maji ya kimkakati kwa mafanikio makubwa kama vile mradi wa maji wa jiji la Arusha ambao unagharimu Shilling Bilioni 520 unaendelea kutekelewza kwa sasa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka Tabora ambao unagharimu Shillingi Bilioni 622, miradi wa maji wa miji 28 ambao unagharimu Shillingi Trilioni 1.2 unaendelea kutekelewza kwa sasa, n.k. Kutokana na maboresha mbalimbali yaliyofanyika takwimu zinaonesha kuwa wastani wa idadi ya watu wanaopata huduma ya maji safi na salama vijijini imeongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.1 mwezi Machi mwaka 2020. Kwa upande wa mijini, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 84 mwezi Machi mwaka 2020.
Kwa upande wa harakati za kisiasa Prof. Mbarawa, alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kutokea 2007 mpaka mwaka 2017 na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi kuanzia mwaka 2012 -2017.
Tz tuna hadhina kubwa Sana ya viongozi Ila basi tu hawajajitokeza.Isingekua huyu Mbarawa kuteuliwa na Kuna kuonyesha uwezo wake basi hata leo tusingeweza kumtaja Katja baadhi ya nafasi kubwa za uongozi was kinchi.Binafsi naamini bado wapowengi wanahitaji kuibuliwa Zaid kwa kuteuliwa kuliko kusubir waende majimboni kugombea ambapo kumejaa fitini kubwa kupata nafasi huku wengi wakishinda na kuacha pembeni wenye uwezo kisa tu wanachapaa na wameandaa watu mapema.
Ninatamani Sana viongozi Kariba ya Kuna Mbarawa wawe bungeni kuliko wale wanaoingia kuchangamsha bwege tu
 
Al Gore alikuwa kielimu pamoja na ukubwa CV hakushinda kwenye primaries za democrats 1992 na kupelekea Bill Clinton kumshinda; na kumfanya awe VP candidate wake akiacha kazi ya Useneta wa Tennesse.
Sina maana ya ku-discredit CV ya Prof; ila kuna nyakati siasa huwa inaangalia mvuto/kukubalika kwa wapiga kura kama karata ya kumfanya mtu achagulike.

Ni kama 2005; Dr. Salim was far better kwa CV na uzoeufu kuliko JK. Hali kadhalika Prof. Mark Mwandosya alikuwa na CV bora kuliko JK, yet kimkakati na mbinu na "mvuto wa sura" JK akalamba dume.

It take a lot of issues to look at pale candidate anapokuwa na sifa ya "kuteulika/kuchagulika".

Julai sio mbali; mbivu na mbichi zitajulikana.
Unaweza kushangaa yule alikuwa mtangaza matokeo 2015 "akawa ndiye"

Tusubiri moshi wa kijani toka visiaa vya karafuuu
 
Back
Top Bottom