CV ya Issa Ponda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CV ya Issa Ponda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanaukweli, Sep 21, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Tumesikia kauli ya mufti nanukuu, (maneno yote hapa ni ya Mufti si yangu):

  "Nawatahadharisha Waislamu wote nchini kwamba Ponda Issa Ponda si mwanazuoni, si Sheikh, hakusoma elimu ya msingi ya kidunia wala ya kidini, hata Qur'an hajui kusoma. Anajaribu kuwatumia Waislamu kwa manufaa yake binafsi. Hatujawahi kushuhudia kutoka Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania jambo lolote la maendeleo zaidi ya ghasia za maandamano, kupora misikiti na kudandia matukio na kuwachangisha Waislamu fedha, mwishoni mwa maandamano hayo huishia kuwatapeli waumini fedha zao ambazo huishia mifukoni mwa Ponda na wenzake."

  "Ni kigenge cha watu wachache wenye kufuata madhehebu ya Mawahabi ambao kwa mujibu wa itikadi yao wanaamini kwamba Muislamu yeyote asiyefuata itikadi yao basi huyo siyo Muislamu na hafai kuwa kiongozi kwa ngazi yoyote ile"

  "Vurugu, chokochoko na ghasia za uvamizi hazikuanzia Bakwata, wamekuwa wakifanya hivyo sehemu mbalimbali mikoani kwa kuvamia na kuteka misikiti na kuwaondoa viongozi waliochaguliwa kihalali kwa nguvu na udhalilishaji mkubwa na hatimaye kupora na kuhodhi rasilimali za misikiti hiyo."

  "Wamekuwa wakiendesha mafunzo ya karate kwenye misikiti hiyo waliyoiteka na kuikalia kimabavu ili waweze kuendeleza dhuluma yao ya uporaji wa Misikiti na vituo vingine vya Kiislamu."

  "Ni vitendo vinavyokiuka maadili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo nawaonya na kuwatahadharisha Waislamu wa madhehebu yote kuepuka vitendo vya uvunjaji wa sheria unaofanywa na kikundi hiki cha watu wachache."

  Source: Mwananchi 21.09.2012

  Mimi najaribu kutafuta ukweli katika haya anayosema mufti. Naombeni wanaofahamu vizuri CV ya Ponda watuwekee hapa.
   
 2. M

  Maulid Daniel Senior Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Muft ameishiwa labda tumuulize yeye kama kiongozi amefanya nn ktk maendeleo ya Waislamu ktk nchi hii. Analolijua ni kuuza viwanja vya Waislamu kiongozi mkubwa kama yeye ameishia kuomba msaada wa kujengewa mskiti mfano hai dodoma{msikiti wa ghadafi} sasa hebu jiulize hivi kabla ya ule msikit waislamu wa dodoma walikuwa hawamuabudu mungu wao. Kama ulicheck EATV alionyesha dhahir kwamba anajitenga na watu wake anaowaongoza pale aliposema waliovamia wizarani sio waislamu bali ni kikund cha wahuni sasa hiyo ni lugha ya kutolewa na Muft au yeye alikuwa anafurahi waislamu kuwekwa rumande kwa kugomea sensa. Mimi siijui CV ya Ponda lakini fikra zake tu anamzidi Muft kielimu
   
 3. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ummati uliohudhuria kwenye maandamano na mkutano wa leo mbele ya sheikh ponda ni jibu kwa huyo anaejiita mufti. Na hilo tamko la mufti ni tamko aliloandikiwa na maaskofu alisome nilimuona alivo akilisoma kwa kunesanesa.
   
 4. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Je ni kweli kuwa Sheikh Ponda ni wa dhehebu la Wahabi?
   
 5. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Tumekusikia Bw. Luis Sendeu, msemaji wa Mufti wa Bakwata !
   
 6. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wewe Wahabi unawajua ?
   
 7. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  kama hadi linacheza karate msikitini litakuja kuwa gaidi hili.. Namsihi mufti kama huyo ponda hajasoma bakwata waandae ilmu ya UPE ili type hzo za ponda wapelekwe
   
 8. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hujajibu swali.
   
 9. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo kuna shule nyingi kama kunduchi , shule ya ubungo , kirinjiko,al muintazir.hizi na nyengine zinaongozwa njee ya bakwata na hisi zinafanya uzuri zaidi ya shule za bakwata ya mufti
  Pia kuna chuo kikiuu cha kiislaam morogoro waislam hawakutaka kabisa bakwata kushirikishwa na hawana chao pale
  Hivyo waislam njee ya bakwata wamefanya mengi mazuri kuliko wao
  Kuna hospital pale magomeni na mifuko ya misaada nje ya bakwata
  Hivyo wimbi la kumkataa mufti aondoke halizuliki tena linakuja hata magazeti yote mpambeni kwa shere

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 10. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Niwarudishe kwenye topic: Anayejua CV ya Ponda naomba atuwekee hapa.
   
 11. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Una uhakika na hilo? au ndo yale yale ya kusema matatizo yote ya waislam yanasababishwa na wakristo! hata hii conflict ya wazi baina ya waislam wenyewe nayo mnasingizia maaskofu! huku si kujidhalilisha jamani! au ndo kutafuta sababu za kuchoma makanisa na kuchana biblia!? Isije ikawa huu ugomvi wenu ukawa ni mchezo wa kuigiza au mpango mahsusi wa kutaka kuingia mitaani na kuchoma makanisa huku bara kama walivofanya uamsho kule zanzibar! kwa kuwa upeo wa kiintelijensia na uwezo wa nguvu za dola unaishia kwenye maandamano ya chadema hayo yanaweza kutokea na watu msije shangaa! matukio yanavyozidi kujiri ndipo itakapodhihirisha nchi inaongozwa na mfumo kristo au hofu dhidi ya waislam! wapi kamanda KAMUHANDA...! je angeuweza muziki huo?
  YANGU MACHO NA MASIKIO!
   
 12. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mbona issue ni ndogo sana: ni CV ya Sheikh Ponda. Huko kwingine mnatoka nje ya mada.
   
 13. C

  Caesar1 Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha usenge maaskofu wameingiaje kwenye dini yenu?shetani mkubwa!usipotoshe
   
 14. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mgalatia bana ! Wewe umemnukuu mufti hapo na amekupa CV ya Ponda, sasa unauliza nini ? Hebu tafuta msalaba uuombe kisha ulale, usisahau kukojoa !
   
 15. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Sheikh Ponda ni mtu maarufu na ana mvuto mkubwa hapa Tanzania.

  Watu maarufu wa namna hii huibua maswali mengi: nini siri ya mafanikio yake? Amesoma wapi? Amefanya nini kabla ya hapa alipo leo.

  Kutuwekea hapa CV ya Ponda ni kujaribu kuongeza mvuto wa mtu huyu maarufu.

  Kwa hiyo tafadhali mtujulishe huyu mtu alizaliwa wapi? lini?

  Alikulia wapi? Alisoma shule gani? Mwaka gani? Amehitimu nini?

  Ana uzoefu gani wa kazi? Wapi? Kwa miaka mingapi? ndio CV tunaomba ya Sheikh Issa Ponda.
   
 16. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Mapovu ya nini? Hoja hujibiwa kwa hoja.
   
 17. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  umeinukuu hapo juu !
   
 18. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kama huna jibu si lazima upost.
   
 19. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  mtumie sms mufti atakuji maswali yako !
   
 20. m

  mpasta JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 383
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  CV mambo ya kikafiri,sheikh ponda sheikh wetu mkubwa sisi waumini tunamkubali,,huyo sheikh wa serikali kibabu simba atoke zake huko,,asubirie kifo mtu wenyewe yupo dakika za majeruhi saa na wakati wowote malaika mtoa roho atamgongea hodi mnafiki mkubwa huyu
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...