wakuu nakili kuwa sikuwahi kumsikia wala kumjua albert msando wakili wa zitto kabwe kabla ya kesi hii iliyiosha jana. Nimevutiwa na ujasiri wake na mapambano aliyofanya ndani na nje ya mahakama kiasi cha kuwatoa jasho wanasheria nguli TUNDU LISU NA KIBATALA.
Naomba wanaomjua vizuri huyu kijana wamwage detail zake: ni nani: uzoefu wake: ana law firm:kesi maarufu alizoshinda: na mambo mengine including CV yake
Duh! kweli MLIMANI(UDSM) Imefulia Enzi zetu LAW wanasoma wenye Point 3, tena hata hizo tatu zenyewe hazitoshi lazima waone masomo mengine umefanya vipi, maana unaweza ukawa na Point tatu kwenye Combi lakini una A ya Divinity na F za Bam, GS na masomo mengine.
By the way mimi nijuavyo hayo masomo ya NGWIN usipo pata A A A A wewe ni Kilazaa tu. Unless mniambia aliugua wakti wa Mtihani ndio maana akapata B moja badala ya A kwenye Combination.
Kwa nyongeza ni schoolmate wa Mwigulu Nchemba chini ya Mwl Gwaje(RIP)!
Msando na Mwigulu wanafahamiana toka Ilboru enzi hizooo!
wivu wa kike acha mara moja
Umenikumbusha mbali mkuu: Kitemango~ KITEI. Jamaa aliiharibu sana shule.Mwigulu alikuwa Head Prefect hapo Ilboru japo uongozi wake mimi sikuupenda maana haki ya mtu ilikuwa ngumu kusikilizwa na alitumia ubabe mwingi kuongoza watu kwa kiburi cha kutoka Mkoa Mmoja na Head Master Mzee Kitemango..
Umenikumbusha mbali mkuu: Kitemango~ KITEI. Jamaa aliiharibu sana shule.
tragedy of the commons
Baada ya kesi iliyokuwa ikileta sekeseke jijini hapa na hata mikoani kati ya Mwanademokrasia wa kweli Zitto Zuberi Kabwe kwa upande mmoja, na viongozi wa CDM wahafidhina kwa upande mwingine, kutolewa maamuzi huku haki ikiendelea kutendeka na kutawala;
Tafadhari mwenye cv ya mwanasheria machachari mwenye upeo na weledi wa juu wa sheria Albert Msando naombeni aiweke hapa jamvini ili sisi wahanga wa kuonewa na kunyanyaswa na wahafidhina, mafisadi wanyanyasaji na waporaji wake za watu tuweze kujua Msando Gwiji jipya mjini hapa weledi wake kaupata vipi ili aendelee kusimamia kesi zetu.
NB: Kama wewe uko unatoka povu baada ya kunywa mbege na viroba huku ukishushia gongo, huu uzi haukuhusu!!!!!!
Unawahusu tu wale wenye kiu ya demokrasia ya kweli ndani na nje ya CDM.
HAKI ITAINUA TAIFA.
unaelewa lakini ulichokiandika, hata kama busara sio sehemu ya maisha yako, jitahidi japo kidogo, leta habari za kujenga sio za kubomoa.
Watu wanasema Msondo ameshinda wakati Nyuma ya Msondo kulikuwa na ...........................!!!Kwa hiyo haki ni pale tu inapokuwa in favor of cdm.Watz kwa double standards tutafika kweli?
WACHANA na fikra tasa,huna uchungu na nchi yako,huyo baba ametufikisha wapi mpaka sasa?Bei za vitu zinazidi kupanda,achilia mbali ww mwenye uwezo wa kupata mkate wa kila siku,Je,Mwananchi wa kawaida asiyeweza kuafford mnansaidia vipi kama BABA wa Nchi?? CCM inaendelea kuwakandamiza wanyongee,...Wake up to reality!!!
Albert Msando ni DIWANI WA KATA YA MABOGINI. Bhaaaas!
Nakumbuka mkuu. Ila nilichelewa sana kuking'amua hicho kirefu aisee; last yr. mwanzo nilidhani ubwabwa ulikuja na Kitemango ndio maana wakauita Kitei.Mkuu unakumbuka kirefu cha KITEI? KITEII= KIPUNGA IVA TULE ELIMU INATUNGOJA ILBORU..
Usimsahau mzee wa MACHAKURA: "NANI KAMWAGA MACHAKURA HAPA?"
Mwigulu alikuwa Head Prefect hapo Ilboru japo uongozi wake mimi sikuupenda maana haki ya mtu ilikuwa ngumu kusikilizwa na alitumia ubabe mwingi kuongoza watu kwa kiburi cha kutoka Mkoa Mmoja na Head Master Mzee Kitemango..