Customer Service/Huduma kwa wateja Tanzania

Generally speaking Tz cs ni ndoto ya mchana.
Ingawa si wote kuna baazi ya maeneo wanawavalue wateja.
Juzi line yangu ya Celtel iliblock nikwatumia email na ndani ya Dk 2 nikapigiwa simu na kupewa PUK namba zangu via my altenative number.
Baada ya kuactivate ile namba my line ikawa on,then nikapigiwa tena simu kukonfirm kuwa my number iko okey.Though such things are rare but watz tuna tatizo la kutoreport mambo kwa wahusika.

Nakupa mfano mwingine umeme ulikatika home nikampigia manager wa Tanesco all over sudden akatuma watu wake wakaja fix

Mimi nilivyo nikikutwa na tatizo huwa nareport kwa wahusika wakuu and not otherwise labda ndo maana huwa napata ufumbuzi.

Ila its a fact CS ni poor tz
 
Huu ujinga upo sana, maana ilifikia kipindi nikaona kama wote wajinga. Nilikuwa na Line ya Celtel na nimeitumia kama miaka 3 nikaja kupata safari ya nje ya nchi nikakaa kama baada ya miezi 9 kurudi naona Line yangu imefungiwa nikajaribu kufuatilia pale Kijitonyama kwenye Ofisi zao wakaniambia namba hiyo ina mteja mwingine, da basi kwa mshangao ikabidi niwe Mpole.

Kwahiyo ndio hivyo wala sishangai kuyasikia haya ndio Bongo yetu
 
Huu ujinga upo sana, maana ilifikia kipindi nikaona kama wote wajinga. Nilikuwa na Line ya Celtel na nimeitumia kama miaka 3 nikaja kupata safari ya nje ya nchi nikakaa kama baada ya miezi 9 kurudi naona Line yangu imefungiwa nikajaribu kufuatilia pale Kijitonyama kwenye Ofisi zao wakaniambia namba hiyo ina mteja mwingine, da basi kwa mshangao ikabidi niwe Mpole.

Kwahiyo ndio hivyo wala sishangai kuyasikia haya ndio Bongo yetu

Duh pole sana!

Lakini kwanini wanasababisha inconviniences kwa wateja? I mean, kila mtu anajua kasheshe ya kutoa taarifa ya ubadilishaji wa namba kwa circle yako.

Labda pengine sheria za huduma ya mobile zinasema hivyo. Kama ni hivyo, at least basi wangeongeza muda wa idleness. Inaonekana muda uliopo sasa hivi ni kati ya mwezi 1 na 6. Ni vipi wakifanya angalau miezi 12, ndipo waikate?
 
Halafu inaoneka Vodacom either wamejishindilia wateja wengi zaidi ya uwezo wa mitambo yao or hawana towers za kutosha baadhi ya sehemu.

I mean, ukiwa maeneo ya Mbezi Beach na kuendelea, simu ya kutoka nje inakuwa ngumu sana kuingia. Nimepata matatizo hayo kama wiki nne zilizopita nilipokuwa nyumbani. Simu zangu za kutoka overseas zilikuwa zinaingia kwa tabu kweli. Mwanzo wapigaji walikuwa wanadhani na-screen simu zao...kumbe zilikuwa hata hazingii.

Ilibidi nichukue line ya Celtel, na kui-abandoned ile ya Voda.
 
Nimeipenda sana hii topic ya CS. Nina experience mbili mbaya ambazo zote zilitokea nilipokuwa nyumbani Arusha mwaka jana.

1. Jogoo House:
Kwa wale wakazi wa Arusha mnaifahamu hii grill ya kuku choma. I used to like this joint kabla sijaondoka nchini kwa hiyo niliporudi nikasema ngoja nikakumbukie. Tupo pale mimi na bwana mdogo wangu na washkaji zake, akaja mhudumu akaanza kupiga stori kama vile ananijua. Mimi nikamwambia sio mimi anayemuongelea labda kuna mtu mwingine anafanana na mimi..lakini huyu dada akang'ang'ana kunijua. Basi tuka order vinywaji na msosi..

Yule dada akaomba anunuliwe soda. Kisha akakaa kwenye meza yetu. Mind you hiyo ni saa 12 jioni ndio kwanza bishara inaanza kuchanganya kwa sababu watu ndio wametoka kwenye mihangaiko yao ya siku. Sahani la nyama lilipokuja, na yule dada akajisogeza akaanza kula bila hata kukaribishwa. I was stunned! Nilishindwa kuelewa kuwa ni policies za mwenye biashara au basi ni jeuri ya mhudumu. I was very uncomfortable kwa kweli.

Sasa ikaja saa ya kulipa..kulikuwa na change kama ya shilingi 1,200 ambayo yule dada aliing'ang'ania. Najua kwa utamaduni wa huku kwa wenzetu tunatoa tip kwenye service lakini, ile service ya siku ile pale Jogoo House ilikuwa HOVYO na haikustahili hata senti moja ya tip.

2. BARCLAYS BANK ARUSHA
Nilikuwa nataka ku-withdraw tu hela kidogo kwa ajili ya matumizi kwa kutumia ATM card yangu ya Wells Fargo. Nilikuwa niko na jamaa yangu mmoja mzungu (mwalimu wa Peace Corp. Tukaenda Standard Chartered wakatuambia ATM yao haifanyi kazi. Tukaenda CRDB pale maeneo ya Clock tower wakasema ni mpaka tembo card. Basi tukawa hatuna namna ikalazimu tuende Barclays.

Pale getini..walinzi wakatuzuia baada ya kuwaambia kuwa tunataka kutumia ATM waka assume kwamba mzungu niliyekuja nae ndio mwenye kutaka hiyo huduma na mimi tumbili nisubiri pale geitini. Nikawaambia ni mimi ndio nataka kutumia ATM yao, na sio yule jamaa yangu (mzungu). Mmoja wa walinzi akasema..."kama ni tembo cards nenda CRDB." Nikawaambia nina VISA card, basi waaniacha nikaenda kwenye ATM yule jamaa yangu ambae anakijua kiswahili kwa mbali akawa amebaki anashangaa mvutano wa mimi kuruhusiwa kutumia ATM kitu ambacho ni so simple..machine ile pale, nenda kaitumie. Najua walinzi ni watu wadogo sana kwenye organizations yeyote lakini wao ndio face ya kampuni.

Yawezekana perception ya ma benki yatu mengi ya kigeni kuwa ni ya watu wealthy...which is true. Lakini nafikiri mimi nilidharauliwa kwa sababu nilikuwa nimevaa jeans..t-shirt na tulienda kwa miguu pale Barclays kwani tulichukua kipanya kutoka pale Clock tower.
All in all...waajiri wanahitaji kuwa train hawa wafanyakazi wao. Kwa mimi kutumia ATM ya Barclays kulikuwa na charges ambazo ni revenue ya hiyo kampuni. Waki discourage users kwa sababu ya jinsi wanavyo appeal then hawatafanya biashara.

Ndio maana hapa marekani in most shopping areas hawa angalii umevaa nini au unaendesha nini. Kazi yao ni kuwa nice kwako (mteja) na kukupa information tena saa nyinge wanazidisha chumvi na mbwembwe ili uingie mkenge ununue biashara yao.
 
Heshima zenu wadau! Mimi kuna kitu kinanikera sana hapa nchini kwetu katika eneo hili la Huduma kwa Wateja - Customer Service. Sielewi pale mwenye biashara au ofisi yake kwa mfano anaajiri watu ambao hawana vision aliyonayo au ameshindwa kuwatrain au wanadharau kazi yao. Inaudhi na pia kushangaza pale unapoingia katika duka hupati hata 'karibu' na watu wameuchuna tu au wanapiga stori zao bila kujali kuwa wewe ni potential customer na unaweza kuchangia kwenye mishahara yao. Wakiona unaelekea kununua kitu ndo wanaanza kujivuta na pindi unalipa na kuacha tips basi kila mmoja atakuchangamkia na kutaka kukujua hadi nyumbani kwako!!!

Next time ukirudi watajikwaa kwa kukukimbilia kumbe wakikuona wanaona 'tips' na pia hata wanaweza kukushawishi kwenda kinyume utaratibu (waibe na kukuuzia kwa bei ya chini...). Serikalini ndo usiseme, kuchafu kabisa. Unaenda kutaka huduma ambayo by the way unailipia lakini mtu anajivuta kama vile alilazimishwa na ukisisitiza atakwambia umpe hela (rushwa) au ndo hatakuhudumia kabisa!
Kuna baadhi ya maduka ya wahindi mjini maeneo ya posta ukiingia utakaribishwa kama mfalme yani utaona hata aibu kutoka mtupu utanunua walai hata socks!! Na wanaokukaribisha ni wahindi wenyewe na maduka yetu wazawa ni hovyo tu..

Ndio maana kuna mashirika yakija nchini yanaleta watu wao au wanaajiri wakenya au waganda au watu ambao si watanzania kwani sisi hatuko makini na wao wana uchungu na investment yao. Natamani sometimes waajiriwe wamachinga kutokana na kujitahidi kwao katika kushawishi wateja ila shida ndo hiyo elimu ndogo waliyonayo na lugha za kigeni ni shida.

Tufanye nini maana tunakoelekea sio kuzuri na tunachekwa na wageni wanaokuja nchini kwetu yani ni aibu.
 
Pole sana mkuu,
Hii kadhia nilishakutana nayo mie mwenyewe, Celtel wamezuia namba yangu kwa sababu sikuitumia kwa muda mrefu sana. Angalau Tigo wana adabu, ila Celtel kimeo sana, wakali mno. Niliamua kuhamia Tigo, huku mabo yanaenda.
Sina uhakika na sababu zinazowafanya wazifungie laini hizi ambazo zinakuwa hazijatumika kwa muda mrefu!

mbaya zaidi Chip ya Airtel usipoitumia zaidi ya miezi mitatu wanaifuta kabisa ...hii imenitokeas !
 
Inakera sana aisee, juzi juzi imenikuta NSSF nimeenda pale na issue yangu mtu aliye ni attend akaniambia kwamba nimuachie namba yangu halafu atanipigia within 2 days. Siku mbili zimepita kimyaa. Nikaenda tena pale siku ya tatu nakuta mtu mwengine completelly tofauti ikabidi nianze upya process ya niliokuwa nakifuatilia . Na huyu mpya akaniambia system hamna na hajui itakuja saa ngapi.

Issue ya kufuatilia siku moja nili mark time wiki 2 kwa sababu unaenda office A wanakwambia nenda office B lakini hasemi tatizo nini. Office B wanakurudisha A wanakwambia tatizo lako ilitakiwa litatuliwe office A. Mind you kwamba between office hizi mbili ni umbali wa kuendesha gari kama 1 hr kipindi cha mchana na foleni.
 
Back
Top Bottom