Neno CV au carriculum vitae linaitwaje kwa Kiswahili?
Hati Nafsi
Maelezo Binafsi ya Mtu Kama Ujuzi n.k (Source Tuki)
Kama ni kuandika katika Heading ni Wasifu kama ilivyosemwa.
My CV - Wasifu Wangu [Kitaalam|Kimasomo|Kimaisha]
Ndiyo mfano Mchungaji Donnie McClurkin ameandika Wasifu wake kwa kirefu sana wa maisha.Hivi mtu anaweza kuandika wasifu wake mwenyewe au unaandikwa na mtu baki?
Nahisi kama hili la wasifu liko mbali kidogo na CV ambayo mtu mwenyewe anajiandikia.
Ndiyo mfano Mchungaji Donnie McClurkin ameandika Wasifu wake kwa kirefu sana wa maisha.
Ukiangalia Biography na CV vyote vinakuwa translated wasifu. mmoja ni wa Maisha mwingine ni wa ujuzi.
Pengine CV inapaswa iwe Wasifu wa Ujuzi na Biography Wasifu wa maisha
Hata hivyo mimi sio nguli wa lugha, ni maoni yangu tu!
Hii ni kwa mujibu wa juha mmoja tunaepigac nae kinywaji haa kitaa.
Cd- country director
Ce- Country editor
Cv- Country volunteer.
Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyoandikwa na R.A Snoxall na H.B. Mshindo inasema kuwa:
Curriculum Vitae ni maelezo binafsi ya kuhusu elimu na uzoefu katika kazi, n.k.
Nyani Ngabu ataongezea.
Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili iliyoandikwa na R.A Snoxall na H.B. Mshindo inasema kuwa:
Curriculum Vitae ni maelezo binafsi ya kuhusu elimu na uzoefu katika kazi, n.k.
Hii ni tofauti na biography ambayo ni maandishi ya habari za maisha ya mtu.
Nyani Ngabu ataongezea.