CUF yataka Eddy Riyami aachiliwe haraka

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
12717343_10153918911474655_8236792988823635452_n.jpg

Chama cha Wananchi (CUF) kina wasiwasi kuwa kukamatwa kwa Eddy Riyami kunatokana na shinikizo la kisiasa ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwakamata viongozi kadhaa wa upinzani visiwani Zanzibar na sasa kinatoa wito kwa jeshi la polisi ama kumpeleka mahakamani au kumuachia huru mara moja kama sheria inavyoagiza.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wiki iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari, 2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.

Bila ya kukosa, Eddy Riyami aliitikia wito huo na kufika Makao Makuu ya Polisi, Zanzibar na kuonana na SSP Simon S. Pasua wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID). Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe 22 Februari, 2016.

Eddy Riyami, akiwa raia mwema, alirudi tena jana kama alivyoagizwa. Alipofika hapo alihojiwa na Polisi na baadaye mwanasheria aliyefuatana naye akatakiwa kutafuta wadhamini wawili watakaomdhamini hadi atakapoitwa tena. Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini, akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016. Mwanasheria na familia yake wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi. Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.

Hadi tunapotoa taarifa hii, hakujapatikana maelezo yoyote ya msingi juu ya kinachoendelea na wala Eddy Riyami hajafikishwa Mahkamani kusomewa mashtaka yoyote.

La ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.

Kutokana na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la wanasiasa.

Itakumbukwa kwamba kwa muda mrefu tokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 tumekuwa tukitoa tahadhari za kuwepo mipango ya kuwakamata viongozi wa CUF na wanaharakati wengine ili kufanikisha malengo ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.

Chama Cha Wananchi (CUF) kinalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumiwa na kutumika kisiasa kufanikisha malengo ya kisiasa ya CCM. Tunashangazwa kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani. CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi iwapo kweli lina kesi dhidi ya Eddy Riyami basi limfikishe Mahkamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake. Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja.

Umefika wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.
 
Pamoja na maajabu mengi yaliyowahi kuripotiwa duniani, bado hakuna ajabu ya mbuzi kulazimishwa kunywa maji. Waweza mpeleka mtoni tu basi, sasa inakuwaje CUF walazimishwe kushiriki uchaguzi uliokosa mantiki ya demokrasia yenye kuzingatia uhuru, haki na sheria?
 
Ndio ubabe wa mkoloni kwa wanzanzibari wanyonge.
 
View attachment 325003

Its getting mo than serious
 
Pamoja na maajabu mengi yaliyowahi kuripotiwa duniani, bado hakuna ajabu ya mbuzi kulazimishwa kunywa maji. Waweza mpeleka mtoni tu basi, sasa inakuwaje CUF walazimishwe kushiriki uchaguzi uliokosa mantiki ya demokrasia yenye kuzingatia uhuru, haki na sheria?
Kwani umeambiwa wamelazimishwa ? hivi mnakaa angalau mkasoma vizuri ama kusikiliza hizi habari zinaporipotiwa? Jecha amewaambia hawajafuata taratibu na ndio maana akawambia tume inawatambua kama washiriki sasa si wafuate taratibu kesi ishe, ata kwenye upatu huwezi kuamka ukasema ati mimi najitoa kuna taratibu zake bhana kubwa..munaendekeza sana siasa za hisia kuliko uhalisia .
 
@: Haijalishi ulaini wa maneno watakayotumia lakini mantiki inabaki ile ile, niwekee hapa kifungu cha katiba kinachoeleza kuwa Mwenyekiti wa ZEC anaweza kufuta uchaguzi na kuamuru urudiwe kwa kadri atakavyo yeye na kama hakipo tusipotezeane muda. Refa aliyeharibu pambano lililopita hana uhalali wa kimaadili kuchezesha mechi ya marudio.
 
Hao Maafisa wote wanaotajwa kuhusika na Swala la Eddy wana Majina ya Watu wa Bara. Hii ni sawa Kabisa Na Ukoloni. Zanzibar inatawaliwa Kimabavu na CCM Kutoka Bara. Hivi hakuna hata Maofisa wa Polisi wazaliwa wa Zanzibar wanaoweza Kusimamia Maswala ya Zanzibar? Kulikoni?
 
Tunasubiri tu magaidi waje ili wahusika wakamatwe maramoja kwani wamesha sema hadharani mipango yao kindakindaki kupitia waandishi Wa habari kuwa magaidi watajipenyeza mgogoro Wa Zanzibar.

Wa kwanza ni mgombea Wa ukawa kwenye urais muungano na Wa Pili ni mgombea urais Zanzibar.

Naamini jeshi limejiandaa ili watuhumiwa watoe ushirikiano.
 
Polisi wasiishie kwa Eddy Riyami tu. wamkamate na Maalim Seif kwa kosa la uhaini pale alipojitangaza kuwa ni Rais wa Zanzibar
 
CUF kuweni makini sana hapo CCM watakamata viongozi wenu na mwisho wa siku ikifikia wakati wa uchaguzi watafanya uchaguzi huku viongozi wakiwa ndani na hiyo ndio itakuwa sababu ya wenyewe kushinda uchaguzi...
 
Kwani umeambiwa wamelazimishwa ? hivi mnakaa angalau mkasoma vizuri ama kusikiliza hizi habari zinaporipotiwa? Jecha amewaambia hawajafuata taratibu na ndio maana akawambia tume inawatambua kama washiriki sasa si wafuate taratibu kesi ishe, ata kwenye upatu huwezi kuamka ukasema ati mimi najitoa kuna taratibu zake bhana kubwa..munaendekeza sana siasa za hisia kuliko uhalisia .

Kwa taarifa yako hYo Jecha mwenyewe vigungu alivyotumia havihusiano na marudio ya uchaguzi ulio futwa n vya uchaguzi ulio ailishwa, achilia mbali kutokuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi..Haya we huyaoni? Nyinyi ndo mnao sababisha Hadi wakina Trump watuwone waafrika wote wapumbavu..Tuache unafiki!
 
@: Haijalishi ulaini wa maneno watakayotumia lakini mantiki inabaki ile ile, niwekee hapa kifungu cha katiba kinachoeleza kuwa Mwenyekiti wa ZEC anaweza kufuta uchaguzi na kuamuru urudiwe kwa kadri atakavyo yeye na kama hakipo tusipotezeane muda. Refa aliyeharibu pambano lililopita hana uhalali wa kimaadili kuchezesha mechi ya marudio.
Bandiko ni kuhusu Eddy Riyami ivoo
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe: 23 Februari, 2016

Wiki iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari, 2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.

Bila ya kukosa, Eddy Riyami aliitikia wito huo na kufika Makao Makuu ya Polisi, Zanzibar na kuonana na SSP Simon S. Pasua wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID). Hata hivyo, hakuhojiwa na badala yake alipewa simu na kutakiwa azungumze na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bw. Salum Msangi ambaye alimwambia arudi tena Jumatatu, tarehe 22 Februari, 2016.

Eddy Riyami, akiwa raia mwema, alirudi tena jana kama alivyoagizwa. Alipofika hapo alihojiwa na Polisi na baadaye mwanasheria aliyefuatana naye akatakiwa kutafuta wadhamini wawili watakaomdhamini hadi atakapoitwa tena. Wakati mwanasheria wake aliporudi na wadhamini, akaelezwa kwamba Polisi imebadili uamuzi wake na imeamua kumuweka ndani hadi leo, tarehe 23 Februari, 2016. Mwanasheria na familia yake wakatakiwa kwenda tena Makao Makuu ya Polisi hiyo leo, saa 3 asubuhi. Walipofika leo asubuhi, wakaambiwa kwamba DCI kaacha maagizo kuwa suala la Eddy Riyami liachwe kwanza na wao warudi tena saa 6 mchana.

Hadi tunapotoa taarifa hii, hakujapatikana maelezo yoyote ya msingi juu ya kinachoendelea na wala Eddy Riyami hajafikishwa Mahkamani kusomewa mashtaka yoyote.

La ajabu zaidi, ni kwamba hata mke wake alipofika kituo cha polisi cha Madema anakoshikiliwa kwa ajili ya kwenda kumuona, hakuruhusiwa kumuona.

Kutokana na mwenendo huu, Chama Cha Wananchi (CUF) kinalichukulia suala hili kwamba ni mwendelezo wa vitendo vya unyanyasaji wa kisiasa dhidi ya wapinzani wa CCM, vitendo ambavyo tunaamini vinafanywa kwa shinikizo la wanasiasa.

Itakumbukwa kwamba kwa muda mrefu tokea wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 tumekuwa tukitoa tahadhari za kuwepo mipango ya kuwakamata viongozi wa CUF na wanaharakati wengine ili kufanikisha malengo ya kisiasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hatua ya kumkamata Eddy Riyami na kumuweka ndani bila ya kumfikisha Mahkamani ni utekelezaji wa mipango hiyo. La si hivyo, ikiwa Eddy Riyami ametenda kosa basi angelishafikishwa Mahkamani ndani ya muda wa saa 24 tokea kukamatwa kama sheria inavyotaka.

Chama Cha Wananchi (CUF) kinalitaka Jeshi la Polisi kuacha kutumiwa na kutumika kisiasa kufanikisha malengo ya kisiasa ya CCM. Tunashangazwa kwamba siku zote wanaoitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani ni wanasiasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wengine lakini hatujawahi kushuhudia viongozi wa CCM kuitwa kuhojiwa, kukamatwa na kuwekwa ndani. CUF imetoa taarifa kadhaa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu matamshi na vitendo vya viongozi wa CCM vyenye mwelekeo wa uhalifu lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa. Hizo ni dalili za waziwazi za Polisi kutumiwa na kukubali kutumika kisiasa.

Tunalitaka Jeshi la Polisi iwapo kweli lina kesi dhidi ya Eddy Riyami basi limfikishe Mahkamani haraka ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake. Na iwapo hawana kesi, basi wamwachie huru mara moja.

Umefika wakati wa Jeshi la Polisi kufanya kazi zake kitaalamu kama sheria na kanuni zao zinavyoagiza badala ya kuwatumikia wanasiasa wa CCM.

HAKI SAWA KWA WOTE

HAMAD MASOUD HAMAD
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
 
Back
Top Bottom