CUF yapasuka vipande vipande; waidhinisha malipo ya fedha wako kambi tofauti

Kabla ya taperi mbowe hajamleta Lowasa ukawa ilikuwa moja, gia zilipobadilishwa angani ukawa ikawa ukiwa!
Huwezi kumaliza tatizo bila kugusa chanzo, Kama mnaona Lipumba yupo na ccm, je Seif na akina Mtatiro wapo nyuma ya nani kama siyo mbowe na Lowasa!
Mbowe amekuwa msemaji wa CUF lini kama hakuna ajenda ya siri?
Na hata kama una miwani ya mbao, lazima ujue ujio wa Lowasa ulikuwa ndo mwanzo wa kifo cha ukawa, na ndo kifo cha cuf, na ndo kifo cha chadema, NCCR huyo wanalizia matanga!
Hapo ndo mtamkumbuka Dr aliyetukuka Slaa kwamba Lowasa was an asset or credibility!!!!
 
Muafuka na kamanda aliyeghairi viti aliyesababisha uchaguzi usifanye pale blue pearl aliyeumiza watu buguruni labda akafanye kazi kwa msajili ukweli hauchangamani na uongo hata siku moja
 
J
mtatiro yupo sahihi,embu na wewe tumia akili yako hata ya kula tu,hapa hakuna tatizo ,kisheria baraza kuu la cuf linamamlaka kisheria la kumfukuza mwanachama yoyote ,lipumba kafukuzwa kisheria na barua ya kuitwa kujitetea amepewa na amekataa,anachotakiwa ni kutii tu amri ya baraza kuu la cuf,kitu ambacho hujaelewa na hujajua kutokana na uwezo wako mdogo kufikiri ,CUF haipambani na lipumba ,bali ni CUF dhidi ya serikali ya ccm waliojivisha sura ya lipumba na msajili wa vyama,tatizo lipo wapi hapa

Jambo zito linalohitaj ufikir mkubwa wew unalijibu kwa kurahisisha,LIPUMBA na SEIF wanajua vzur katiba yao bt wanafanyaiv kwa vivuli vya CHADEMA na CCM
 
Lengo kamili la CCM ni kumnyima maalim nguvu, mipango ikapangwa na ndio inatekelezwa kupitia msajili, Le profesel ajifanye anafukuza wakurugenzi haraka haraka apatikane mwingine apewe mandate ruzuku itoke aichukue
 
Kwa mujibu wa Jambo Leo (04.10.2016)


CUF yapasuka vipande vipande; waidhinisha malipo ya fedha wako kambi tofauti.

Lipumba aendesha chama buguruni , Maalim Vuga.

Wenye Mamlaka ya kuidhinisha nyaraka za fedha na benki; Magdalena Sakaya yupo upande wa Lipumba wakati Bashange yupo upande wa Maalim Seif.

Magdalena Sakaya ‘’ Lipumba ndiye Mwenyekiti wa chama anayetambulika ruzuku ya chama inaingia kwenye akaunti za chama, kwa sasa hatujajua utaratibu maana kuna mvutano unaofanya masuala mengi yasiende sawa’’ aliongeza ‘’Msajili wa vyama anaweza kuamua kuzuia ruzuku. Ruzuku ni fedha za walipa kodi na sidhani kama mtu atakubali kuendelea kutoa ruzuku haionekani inakwenda kufanya kitu gani zaidi ya malumbano, sijui ila hali kwa kweli si nzuri’’

‘’alisema hakuna anayeweza kusaini ili fedha za chama hicho zitoke na kusisitiza kuwa mchakato wa kumpata mtu mwingine kwa maelezo kuwa Bashange uteuzi wake umetenguliwa’’

Kwa upande wa Mtatiro ‘’kwa mujibu wa sheria chama lazima kipewe ruzuku yake si ombi ni takwa la kisheria’’ aliendelea ‘’anachofanya sasa (Lipumba) ni kwa mujibu wa polisi na msajili wa vyama hawezi kuathiri shughuli za chama, fedha haziwezi kuleta mtafaruku, maana vikao vya chama. Msajili hata aangushe mbingu ,hawezi kubadili uamuzi wa vikao vilivyoamua kumfukuza uanachama Lipumba’’

Jambo Leo (04.10.2016)

My take;

Hapa kuna tatizo kubwa sana na linahitaji busara kufikia muafaka..kwa sababu kwa sasa siasa za vijembe baina ya kambi mbili zimetawala. Ila Naomba walio karibu na Mtatiro wamshauri awe na tabia ya kuweka akiba ya maneno…anaongea mno kiasi kwamba ‘’silaha zake zinajulikana’’. Pia arejee kilichowapata akina Marando, Leo Lwekamwa, Benson Kagaila na Marehemu Jidulamabambasi pale ambapo Msajili alipositisha ruzuku na kuwapa Mrema na Cheyo ndipo tambo zao ziliisha.

Kama msajili anamtambua Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF ni mahakama pekee ndiyo yenye uwezo wa kutengua na sio tambo. Kama unafikiri Msajili hawezi kubariki au kupinga uamuzi wa vikao vya chama usiishie kujipa haki wewe na Seif pia utambue kuwa akina Bashange hawana kitu kwani Lipumba kama Mwenyekiti aliyewateua mwaka 2014 kawatengua. Sitii neno ila niliweka angalizo tu. Bado naweka akiba ya maneno.
lazima msajili asitishe ruzuku. hizo ni hela za umma haiwezekani kugombewa kama fisi kukuta mzoga. lazima seif awache ujasiriasiasa na kutambua cuf ni chama cha kitaifa sio cha wazanzibari peke yao. wakae wajumbe wa bara wapewe nafasi yao kwenye vikao vya cuf. sio kina seif kula hela za ruzuku wenyewe tofauti na lengo la hela hizo.
 
Kabla ya taperi mbowe hajamleta Lowasa ukawa ilikuwa moja, gia zilipobadilishwa angani ukawa ikawa ukiwa!
Huwezi kumaliza tatizo bila kugusa chanzo, Kama mnaona Lipumba yupo na ccm, je Seif na akina Mtatiro wapo nyuma ya nani kama siyo mbowe na Lowasa!
Mbowe amekuwa msemaji wa CUF lini kama hakuna ajenda ya siri?
Na hata kama una miwani ya mbao, lazima ujue ujio wa Lowasa ulikuwa ndo mwanzo wa kifo cha ukawa, na ndo kifo cha cuf, na ndo kifo cha chadema, NCCR huyo wanalizia matanga!
Hapo ndo mtamkumbuka Dr aliyetukuka Slaa kwamba Lowasa was an asset or credibility!!!!
Aiseeh..umenena sawa kabisa mkuu.
 
mtatiro yupo sahihi,embu na wewe tumia akili yako hata ya kula tu,hapa hakuna tatizo ,kisheria baraza kuu la cuf linamamlaka kisheria la kumfukuza mwanachama yoyote ,lipumba kafukuzwa kisheria na barua ya kuitwa kujitetea amepewa na amekataa,anachotakiwa ni kutii tu amri ya baraza kuu la cuf,kitu ambacho hujaelewa na hujajua kutokana na uwezo wako mdogo kufikiri ,CUF haipambani na lipumba ,bali ni CUF dhidi ya serikali ya ccm waliojivisha sura ya lipumba na msajili wa vyama,tatizo lipo wapi hapa
Suala hili tusilifanye kama la kiushabiki wa "Yanganasimba". Hakuna upande uliosahihi katika mgogoro mkubwa namna hii. Mambo yatawekwa sawa mahakamani kwenye tafsiri sahihi za kisheria. Kambi Mtatiro wanasema wao wako sahihi, kambi Limpumba nao wanasema pia wako sahihi. Mwamuzi sahihi kwenye "game" hili ni mahakama tu, maana hakuna namna nyingine ya kupata suluhu.
 
-->>MSAJILI WA VYAMA NDIYO CHANZO CHA MATATIZO YOTE HAYA,AMEVUKA MIPAKA YA MAJUKUMU YAKE,AWAACHE WANA CUF NA CHAMA CHAO NA WADHAMINI WAO WA CHAMA./
•WAFANYE CHAGUZI ZAO NDANI YA CHAMA / CHAMA NI WANACHAMA.WAO NDIO WENYE MAMLAKA HALALI JUU YA KIONGOZI WAMTAKAYE../
Hivi kweli sakata hili ni la wanaCUF wote, ama ni suala la maslahi binafsi kwa ka-kikundi ka watu wachache wachumia tumbo?
 
politics is a free room,mtu yeyote anaweza kuhama au kuhamia.lowasa kuhamia ukawa sio tatizo,tena lazima tumpongezee lowasa kwasababu amesaidia kuinua aupinzani,kwa mara ya kwanza dar salaam iko chini ya ukawa baada ya ujio wa lowasa,wabunge wameongezeka,ccm imepasuka vipande tumeona wenyewe ,ukawa umefaidika sana na ccm mnalijua hilo yeyote aliyepinga ujio wa lowasa ni adui wa upinzani ni mamluki lipumba na slaa ni mamluki na wameondoka zao
Neno "Mamluki" linafahamika. Hivi umamluki wa Dr. Slaa huwaga ni upi? Maana mzee wa watu alijiuzuru kwa maelezo yaliyoshiba, kwamba hakuridhishwa na viongozi wa Chadema kumpokea Lowasa. Je huo ndiyo umamluki wa huyo mzee?
 
Hapo waelewane tu, Tatizo Mtatiro anatumia akili za kutoka Ufipa na huku Lipumba akitumia akili toka Lumumba....Hapa sioni Lipumba akishindwa kirahisi.

Hawa jamaa wa Lumumba wakishupalia kitu huwa hawashindwi kirahisi.!

Ngoja niweke akiba ya maneno.!

Kwa hiyo unawapongeza lumumba kwa uharamia wao!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom