CUF yameguka vipande vipande

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WAJUMBE watatu wa Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa wa CUF, wamejiuzulu uongozi na kujivua uanachama huku wakitoa tuhuma kuu sita ambazo zimesababisha kuchukua uamuzi huo.

Tuhuma hizo ni chama kupoteza dira, usalama ndani ya chama, Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ubadhirifu wa fedha, matumizi mabaya ya madaraka na chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni.

Wajumbe hao ni Abubakar Rakesh, Juma Kilaghati na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Vijana Taifa, Omary Costantino.Wakizungumza Dar es Salaam jana, wajumbe hao walisema ni vigumu kuendelea kukaa katika chama ambacho hakijitambui.
Rakesh alisema hivi sasa chama kimepoteza mwelekeo na kwamba, hiyo inatokana na viongozi waliopo madarakani kutumia nafasi hizo kujineemesha binafsi badala ya chama.

“CUF ya wakati huu siyo tena ya wanachama, ila ni ya watu wachache ndiyo maana ukionekana kutetea maslahi ya chama kwa nguvu, utaambiwa unakihujuma chama hivyo uondolewe,” alisema Rakesh.

Aliongeza kuwa kitendo cha Hamad Rashid na wenzake kutimliwa uanachama, ni kutokana na chuki binafsi na kuonekana kutetea haki za chama, kwa nguvu walimfukuza huku akiwa tayari na pingamizi ya Mahakama Kuu.
Rakesh alisema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif na Naibu Katibu Mkuu bara, Julius Mtatiro, walipokea mapema pingamizi ya mahakama hata kabla ya kuanza kwa ajenda ya kuwajadili.

Alisema kumekuwapo na ubadhirifu wa fedha za chama, hasa bara kutokuthaminiwa badala yake, Zanzibar kupewa kipaumbele zaidi katika bajeti.

“Mwaka 2010 mgombe Urais Profesa Ibrahim Lipumba katika kampeni zake zote alipewa Sh70 milioni, ambako alikuwa na jukumu la kuwaomba wapigakura zaidi ya milioni 15, huku Seif akipewa Sh76 milioni kuomba kura kwa watu zaidi 200,00,” alisema Rakesh na kuongeza:

“Mgawanyo wa fedha hizi kati ya bara na visiwani, imekuwa sababu ya sisi kuanza kuamini kuwa CUF ni chama cha Wazanzibari ndiyo maana tunaondoka ili kupisha ubepari utawale wanavyotaka wao.”

Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, alisema wanachama hao wamejua ambacho kinaendela, kwani katika Mkutano ujao wa CUF walikuwa wanakwenda kuwaondoa.

“Hawa walikuwa wamesalia katika mkutano mkuu uliowaondoa wenzao wanne, akiwamo Hamad na kujitoa leo (jana) wamejua ambacho kimepangwa kutokea,” alisema Mtatiro.

SOURCE:MWANANCHI
 
kwa heri CUF, mtatiro tulikuheshimu udsm, sasa unaangukia pua

Alikuwa mpambanaji mzuri sana pale udsm,asingestahili huyu jamaa kuwa ndani chama kinachopotea katika ramani!he was the man of action!Pole sana Julius Mtatiro,the best of mine,waziri wangu wa mikopo!ulipo hapakufai.
 
Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, alisema wanachama hao wamejua ambacho kinaendela, kwani katika Mkutano ujao wa CUF walikuwa wanakwenda kuwaondoa.

"Hawa walikuwa wamesalia katika mkutano mkuu uliowaondoa wenzao wanne, akiwamo Hamad na kujitoa leo (jana) wamejua ambacho kimepangwa kutokea," alisema Mtatiro.

Hii kauli ya Julius Mtatiro inanipa shaka kwelikweli...yaani hawa jamaa wanakuwa wamepanga kuwafukuza watu hata kabla ya kuwasikiliza? Hii ni hatari kubwa sana kwa afya ya chama kama CUF.Kwa maneno mengine wanachama wa hiki chama wategemee kupigwa chini muda wowote bila hata kusikilizwa....Nadhani wanaanza kuonekana kuwa ni watu wasiopenda suluhu,wanafiki na wanataka kuendesha chama kifalme...
 
Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, alisema wanachama hao wamejua ambacho kinaendela, kwani katika Mkutano ujao wa CUF walikuwa wanakwenda kuwaondoa.

"Hawa walikuwa wamesalia katika mkutano mkuu uliowaondoa wenzao wanne, akiwamo Hamad na kujitoa leo (jana) wamejua ambacho kimepangwa kutokea," alisema Mtatiro.

SOURCE:MWANANCHI
Mtatiro, huoni kuwa unathiobitisha maneno kuwa chama kinaendeshwa kiimla? Yaani mmeshapabnga kuwafukuza wakati hata kesi yao haijaanza kusikilizwa?
 
naomba cuf ife kabisa-ibakie historia tu kuwa kulikuwa na chama kinaitwa cuf
 
...Naibu Katibu Mkuu wa CUF bara, Julius Mtatiro, alisema wanachama hao wamejua ambacho kinaendela, kwani katika Mkutano ujao wa CUF walikuwa wanakwenda kuwaondoa.

"Hawa walikuwa wamesalia katika mkutano mkuu uliowaondoa wenzao wanne, akiwamo Hamad na kujitoa leo (jana) wamejua ambacho kimepangwa kutokea," alisema Mtatiro.
Hee! Nimeipenda hiyo. Kumbe uamuzi wa kuwafukuza wanachama huwa unakuwepo kabla ya mkutano? Sasa kura za 'wanaounga na wasiounga mkono' huwa zina kazi gani? Kumbe ni heri Mtatiro akawataja na wengine watakaokuja kufukuzwa baada ya hawa!
 
Hamna jipya, same shit by the same syndicate HR.
CUF ni taasisi hata Lipumba na Seif wakiondoka au wakifa CUF itakuwepo..

Watu walisema hayo hayo wakati Nyerere anaondoka kwenye uongozi na alipokufa, lakini maisha yanasonga mbele!

Jana kulikuwa na mkutano mkubwa wa CUF Temeke, kauli mbiu ilikuwa, "waache waende, Bahari haikai na uchafu"
 
Kauli za wafa maji siku zote ni kutapatapa.Ndio maana Jussa alisema wazi cuf ni kwa ajili ya wazanzibar na waislam pekee
 
Naona gazeti lime ripoti habari nusu . Jana niliwasikiliza live hawa watu, sababu kubwa ilikuwa ni udini ndani ya cuf kwani Jussa na Self walisema wameshindw uzini sababu kuna wa kristo wengi na wa bara. Hovyo waliona bora kujitoa kwani watu wa bara na wakristo wanabaguriwa kwenye chama chenye umwinyi CuF .
 
Kauli za wafa maji siku zote ni kutapatapa.Ndio maana Jussa alisema wazi cuf ni kwa ajili ya wazanzibar na waislam pekee
Vipi CHADEMA nayo ni kwa ajili ya WACHAGA na WAKRISTO pekee???!!!
 
Alikuwa mpambanaji mzuri sana pale udsm,asingestahili huyu jamaa kuwa ndani chama kinachopotea katika ramani!he was the man of action!Pole sana Julius Mtatiro,the best of mine,waziri wangu wa mikopo!ulipo hapakufai.

waziri wangu wa mikopo 2006/2007, na baadaye waziri wangu mkuu 2007/2008. bushi akachukua mikopo, aliwahi kutishia kukesha HESLB, alipomaliza chuo tu, akapewa ajira udsm bila kazi kutangawa wala kufanyiwa interview. amekuwa pale udsm lakini hana msaada kwa wanafunzi.
 
Vipi CHADEMA nayo ni kwa ajili ya WACHAGA na WAKRISTO pekee???!!!
images
 
Back
Top Bottom