CUF yakanusha kadi kurudishwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yakanusha kadi kurudishwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Topical, Feb 14, 2012.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni kumekuwa na taarifa za uongo na propaganda zinazoenezwa na Hamadi Rashid kwenye vyombo vya habari kwamba zaidi ya wanachama 1000 wa CUF wa mikoa ya Dar es Salaam na maeneo mengine wamerudisha kadi na kumkabidhi Hamad Rashid.

  CUF imefuatilia na kubaini habari hizi ni za uongo na chama kimebaini kwamba kadi anazoonesha kwa waandishi wa habari si za wanachama bali ni za kutengenezwa ambazo aliziandaa wakati wa Kura za maoni za kuwapata wagombea wa Ubunge na uwakilishi kwa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na Chama kuzuia uingizaji wa wanachama wapya muda mfupi kabla ya kura za maoni.

  Kwa wakati huo Hamadi alikuwa ameandaa Kadi mpya 7000 ziweze kumsaidia katika kinyang'anyiro hicho, hivyo basi hakuna wanachama 1000 waliompelekea kadi kwani wanaCUF wako ngangari na chama kipo imara kwa kuwa wanatambua kuwa wao si wanachama wa UHS (United Hamad Suppoters), bali wao wanachama wa The Civic United Front hivyo hawapo kwa maslahi ya mtu binafsi.

  Chama cha wanachi CUF kinatoa tahadhari kwa wanachama wake kwamba kumekuwa na zoezi la kununua kadi za wanchama wa CUF na Hamad kwa kutumia watu mbalimbali,Hivyo mwanachama yoyote asikubali kutoa kadi yake kwa namna yoyote na kwa mtu yeyote.

  HAKI SAWA KWA WOTE
  IMETOLEWA NA AMINA MWIDAU
  MKURUGENZI WA HAKI ZA BINADAMU NA UENEZI
   
 2. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wadau wa mpira wa mguu huwa tunasema 'mimba hiyo'...umenisoma?
   
 3. KIRUNGI

  KIRUNGI Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sn dadangu mwidau,naona unajitahidi sn kuficha moto wakati moshi unakuumbua.unaposema kadi zinazo rudishwa hamadi rashidi anazo toka kura za maoni huo ni uongo wa utu uzima,siasa zimebadilika jifundisheni kusema kweli.kuna uchaguzi mdogo ARUMERU nendeni then matokeo yata amua kama wanachama wanapungua au wanaongezeka.sifa kubwa ya m2 aliekwenda shule ni pa1 na kujua kusoma nyakati,najua kama sote 2li ipenda cuf lkn bwana ameipenda zaidi
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo wanamkana hata yule kada wao wa tanga aliyejieleza jana ITV.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nawashauri waende Arumeru nadhani hawatakosa kura kama walizopata chadema uzini (282)??? watakuwa wametoa elimu ya uraia; hakuna kukata tamaa kwenye siasa..
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni siasa tu hakuna kingine hapa, na watalielezeaje suala la kushika nafasi ya tatu Uzini?????
  Iweje Chadema mlioiimbia wimbo wa udini, ukabila, ukaskazini, undugu, n.k. ishike nafasi ya pili Zenj, afu mnasema eti ni propaganda za Hamad Rashid Mohamed.

  Kwa maoni yangu ni propaganda zenu ninyi pamoja na hao waliowatuma kutupumbaza, il hali wenye akili wataona kinachofutuka ndani ya chama cha wananchi CUF. Kudanganya muendelee kwa walio na uono wa karibu. Ila kwa wanaoona mbali, poleni....

  Hata hivyo mnakaribishwa Arumeru Mashariki kuchukua jimbo kama alivyosema Mtatiro....wenye akili tunajua wazi ni jitihada zenu za kummega kura za wapunzani, baada ya kufunga pingu za uhasama dhidi ya vyama makini vya upinzani... muendelee... tuone mwisho wenu utakuwa wapi. Ninavyoona mimi. Kifo chenu kiko karibu zaidi kuliko cha hao mabwana zenu ccm.

  MOD naomba usifute haya mawazo yangu, yawapeperukie CUF kama wapo huku, pamoja na washirika wao MS, FF na wengine wenye muono wao.
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,763
  Trophy Points: 280

  A bastard is a liar, Shakrespear wrote a poem.
  Matokeo ya Uzini ni jibu tosha.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Wanachama 1,328 waikimbia CUF  [​IMG]
  Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, wakiangalia kadi za chama hicho zilizorudishwa na wanachama eneo la Mbagala Zakhem wilayani humo jana.(PICHA: MOSHI LUSONZO)


  Chama cha Wananchi (CUF) kimepata pigo baada ya wanachama wanaodaiwa kufikia 1,328 wakiwemo viongozi wakuu wa wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam kujivua uanachama na kurudisha kadi zao.

  Tukio la kurudisha kadi hizo lilitokea eneo la Mbagala Zakhem jana, ambako wanachama hao wakiongozwa na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu Wilaya ya Temeke, Salum Sudi, walieleza kuwa wako mbioni kujinga na chama kipya cha Alliance for Democracy Change (ADC) kinachodaiwa kuwa kiongozi wake ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed.

  Pamoja na kadi hizo, vitu vingine vilivyokabidhiwa mbele ya Mhamasishaji Mkuu wa CUF Mkoa wa Tanga, Salim Dayadaya, ni pamoja na bendera na fulana.

  Akitoa tamko la kuondoka kwenye chama hicho, Sudi, alisema kwa awamu hiyo ya kwanza viongozi pekee walioungana na wanachama hao kurudisha kadi ni 12 wa ngazi mbalimbali wa wilaya ya Temeke.

  Alisema uamuzi wa kujitoa kwenye chama hicho umechukuliwa baada ya kugundua kuwa kuna ukweli katika hoja za Hamad kwamba CUF inaongozwa katika misingi ya usultani na upendeleo.

  Alidai kuwa kabla kuamua kurudisha kadi, walikuwa watiifu kwa kukitumikia chama hicho, lakini walibaini ukweli huo baada ya kuona mambo mbalimbali hayaendeshwi sawa.

  Sudi alisema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, anaendesha chama hicho kifalme pamoja na kufanya upendeleo wa wazi kwa upande wa Zanzibar, jambo ambalo limewafanya uvumilivu wao ufikie kikomo.

  “Maalim Seif alijitengea kiasi kikubwa cha pesa katika Uchaguzi Mkuu upande wa Zanzibar, lakini upande wa Bara alitenga pesa ndogo sana wakati kijografia Tanzania Bara ndio ilitakiwa kuwa na bajeti kubwa kutokana na eneo lake,” alisema Sudi.

  Alisema kuwa hata mawakala wa chama hicho upande wa Zanzibar walipewa posho ya Sh. 15,000 wakati wa Tanzania Bara walipewa Sh. 4,000 na wengine hawakulipwa kabisa.

  “Kwa msingi huo, tumeamini hoja ya Hamad kuwa chama hiki kinafanya kazi kwa upendeleo, tunamuunga mkono na tunamuahidi kuwa nyuma yake ndani ya chama kipya,” alisema.

  Habari zinasema kuwa ADC kipo mbioni kupatiwa usajili wa muda wiki ijayo.

  Alipoulizwa Hamad juu ya kuondoka kwa wanachama wa CUF, alisema kuna kila dalili muda wa kufa kwa CUF umewadia kuanzia Zanzibar hadi Tanzania Bara.

  Alisema wanachama waliojiengua wilayani Temeke ni kama mvua za rashasha tu na kukifananisha chama hicho sawa na kioo kilichopasuka kinachohitaji kuondolewa.

  “Mimi sishangai jambo hilo, nimeeleza toka zamani kuwa CUF imekufa kuanzia Zanzibar hadi huku Bara, hakitakiwi na watu kutokana na uongozi wao mbaya,” alisema Hamad.

  Aliongeza: “Hata Mwalimu Julius Nyerere alisema kioo kikiingia vumbi huwa kinafutwa, lakini kikipasuka kinaondolewa, muda wa kuiaga CUF umefika.”

  Hata hivyo, alikanusha taarifa ya kuanzisha chama kipya cha siasa kwa kueleza kuwa hawezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu anaheshimu maamuzi ya mahakama kwa kuwa shauri lake la kupinga kufukuzwa kwenye chama hicho bado linaendelea.

  Aliongeza kuwa amewahi kusikia kuwa wanachama wenzake wameanzisha chama hicho, lakini hajawahi kwenda wala kuomba uanachama.

  Alipotafutwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, kutoa ufafanuzi kuhusiana na kuondoka kwa wanachama hao, hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuzimwa.

  Hamad alitimuliwa katika chama hicho mwishoni mwa mwaka jana kwa madai kuwa anachochea mgogoro, lakini alifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kupinga maamuzi hayo, anayodai kuwa yalikiuka amri ya mahakama. Bado anaendelea na ubunge wake.  CHANZO: NIPASHE
   
 9. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Akilki nyengine mtu unashindwa kuzielewa,

  Watu wanarudisha kadi zenu kuanzia Mwanza hadi Temeke halafu wewe unamng'ang'ania hamad rashid tu.

  Kwahiyo unataka kutuambia hata wale viongozi 12 wa temeke walikuwa na kadi feki? na wale viongozi wa mwanza nao walikuwa na kadi feki? kama ndivyo basi sitoshangaa kwamba hata maalim seif na justa ismail nao wana kadi feki!!
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Kazi kwelikweli, siye yetu macho
   
 11. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kushnei cuf pole yao kwa kukataa ukweli
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana dada yangu Amina Mwidau, Uhishimiwa kazi kweli kweli huna jinsi inakulazimu uongope tu maana ukienda kinyume kidogo tu na SULTANI baaasi kale kamkopo ulikochukua kule bungeni itakula Kwako.
  Vipi safari hii mtawaandalia shilingi Ngapi kina Mtatiro na Mketo Kama imprest kule Arumeru? Maana kumbukumbu zangu zinanipa mliwapatia Mketo(milioni82), Mtatiro (milioni120 na vijisenti kadhaa) kule Igunga ambazo return yake nina hakika huna na bado mkagalagazwa....(namba 3), Vipi juzi Uzini? (namba 3).
  Na sasa Nendeni Arumeru kuudhihirishia umma maneno ya MHE. Hamad Rashid kwamba Chama Bara kimekufa na hata Wewe unajua kwani ushahidi unao fika mkoani kwako Tanga.....daiya daiyaa!!
  Ni vyema mkijibu hoja kuliko kuongopea Watanzania.
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Pembe la ng'ombe hilooooo.
   
 14. t

  thesolomon Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyie semeeniiiii na kibaraka wenu hamad rashid lakini cuf twasonga mbele
   
 15. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Nipashe la jana tarehe 14/2/2012 limetoa mpaka picha za viongozi wa CUF wakiwa wameshika rundo la kadi zilizorejeshwa na wanachama, sasa sielewi huyu dada wa CUF anakanusha nini hapo juu. C*R*A*P
   
 16. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Yale yale eti?: "Mwanasiasa yeyote muongo; anachoweza kusema kweli ni jina lake tu!"
   
 17. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu aliyetoa hii ripoti CUF anastahili kushtakiwa Huyu, haiwezekani aongope 2 that extent! Yani anatudanganya hivi hivi hadharani duh! Siamini halafu Ni mheshimiwa sana Huyu wa pale mjengoni.....Dah! Kweli jela Ni noma yoote ni kwa sababu wanasubiriwa tar.13-03-2012 na Jaji Shangwa......lazima watapetape.
  Uongo wenu viongozi CUF ndio unaomaliza chama.
   
 18. Z

  Zahor Salim Member

  #18
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nimeulizwa sana kuhusu matokeo ya Uzini. Bahati mbaya kama ilivyo kawaida ya Watanzania walio wengi huwa hatufanyi utafiti, uchambuzi wala upembuzi na badala yake tunakuwa wepesi wa ku-draw conclusion. Kumekuja analysis kuwa Chadema sasa inaipiku CUF kwa kushika nafasi ya pili na wengine wakadiriki kusema kufukuzwa kwa Hamad Rashid kunakiathiri Chama. Niwarejeshe kwenye matokeo ya 2010 kwa nafasi ya Ubunge jimbo la Uzini ambapo CCM ilipata kura 6,651, Chadema 617 na CUF 524. Aliyekuwa mgombea wa Chadema kwa nafasi hiyo ni huyu Ali Mshimba Mbarouk ambaye amegombea Uwakilishi mara hii. Sasa kutoka kura 617 hadi 281 amepoteza mvuto kiasi gani? Isitoshe, CUF kwa kuzielewa siasa za Zanzibar hatukusumbuka kutumia fedha nyingi. Tumetumia milioni 7 tu wakati Chadema wamenambia wametumia milioni 60 (haidhuru mimi naamini wametumia zaidi kwa mambo tuliyoyaona kule). Sasa katika hali hiyo, kuna lipi jipya? Nani aliyepoteza? CUF inajua inachokifanya.


  Source Jussa from face book
   
 19. k

  kanjanja Member

  #19
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anajifariji
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naona unafurahia kweli ...aisee ..kwann?
   
Loading...